Elections 2010 Mwanza City on Fire!

Nimeongea na rafiki yangu anayesoma St. Augustine ameniambia hali ni mbaya huko. Anasema mabomu yako nje nje tu, mmmh Tanzania tunaenda wapi?
 
hizi habari za leo....tutashindwa hata kuamua ipi ni ya ukweli au uongo....kwa nini watu msiwe serious kidogo
 
Kwa mujibu wa Star TV,jengo la CCM limewashwa moto,barabara zimefungwa.
Hali si shwari
 
Mungu wangu,hawa CCM wanataka kuona damu inamwagika tu.nasikia hali ya hatari imetangazwa mjini Mwanza.
 
Matokeo yanachakachuliwa, na habari nazo zinachakachuliwa...leo lazima vichwa viume.
 
True hali si shwari Mwanza nimeongea na mama yangu huko hali ni mbaya na hofu tupu
 
Mi nadhani Masha anataka kuwe na mtafaruku ili apeleke mapambano mahakamani maana huko ana ujuzi zaidi wa kuchakachua sheria. Ni kama ujanja wa kuzima taa uwanjani ili mechi irudiwe
 
kama hawajui ccm watajuta kujaribu kuchakachua matokeo, kwani masha ni kitu gani hapa nchini, ajue hatakuwa salama kwa namna yoyote, mungu atatupigania, kwani yupo upande wetu.
watu wote na waseme AMEN.
 
Masha si mbunge tena Nyamagana.......Wenje juuuuuu....CHADEMA juuuuuuu.....CCM chaliiiiiiii.......hongereni sana watanzania mnaohitaji mabadiliko Nyamagana na Tanzania nzima....aluta continua.....!!
 
Kweli hali ni tete huko MZA nimeongea na mtu wa huko ila hilo la shule kuwaka moto na ofisi ya ccm, hajanijulisha.
 
Ikulu kupitia damu na maiti za watu. Laana, laana. Laaaaaaaaaaaana. Jk ni lazima utufanyie hivi?
 
Mdogo wangu amenipigia simu sasa hivi na kuconfirm kuwa shule moja karibu na jengo la manispaa imechomwa moto.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom