Mbona kuna barabara ya nyasala nyakato na imekamilika kwanini watu wasitumie hiyo hasa wanaotoka maeneo ya buzuruga igoma maana wengi nahisi wanapitia town afu foreni mwanza si kivile bado magari hayajawa mengi sijawah kaa zaidi ya robo saa unless kuwe na ajali au msafara
Mkuu inaonesha weww unaishi mitaa ya Uhuru/Pamba road/Kenyatta road/Nyerere road.
Waulize akina Marire, Eiyer na wakazi wa Igoma huwa wanatumia muda gani kufika town!.... Foleni Mwanza imeanza kuwa kero hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Nionavyo mie hiyo barabara ya Nyasaka - Nyakato ingewekewa route ya daladala make ingepunguza foleni kwani watumiaji wengi wa route ya Ilemela - Nyasaka - Nyakato mpaka Igoma ni abiria qa daladala.
Kingine kuna mradi niliona katika gazeti fulani kutakuwa na route ya majini kutoka Kirumba mpaka Luchelele... Sasa sijui mradi huo utaanza lini?
Damn .........
Foleni siku hizi ipo sana na nyakati za nyuma ulikuwa unaweza kutumia dakika 20 kufika mjini,siku hizi unatumia hadi saa nzima na pengine zaidi
Sijui kwanini serikali haiwekei mkazo barabara hii ya Nyasaka iweze kuwa na rout za Hiace
Baada ya miaka kama mitatu hivi foleni itakuwa ni balaa!
Ngoja niseme na Sumatra kisha nitaleta mlishonyuma kuhusu hiyo route!!