Mwanza: Afariki dunia baada ya kuigonga ndege ya FastJet

Mwanza: Afariki dunia baada ya kuigonga ndege ya FastJet

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,276
b93fa7536f5816caa530cd32f8d8612c.jpg
Mkazi mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya FastJet iliyokuwa ikiruka katika uwanja wa ndege wa Mwanza kuelekea Dar es salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 18, 2018 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.

Alisema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea Dar es salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.

"Ingawa ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo treni", amesema Mayongela.

Amesema kabla ya ndege hiyo kuruka, taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna chochote.

"Haijulikani mtu huyo alitokea wapi, vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi utakapokamilika", amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Amesema kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalamu wa usalama uwanjani hapo.

"Pengine tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukubaliana nalo kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia njia ya kurukia ndege", amesema.

Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanza .Mkazi mmoja wa mkoani mwanza Afariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet iliyokuwa inaruka kutoka uwanja wa ndege mwanza kuelekea jijini Dar es salaam
Akizungumza na Mwananchi leo Januari 18, 2018 Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.



Afariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hatari kwa hiyo uwanja wa ndege unakatisha kama barabarani!
 
Alienda kutafuta nn hapo? Maanna si mfanyakazi wa hapo it seems, au kuna barabara ya shortcut hapo uwanjani? Na kwani hakuna uzio?
 
kula LIKE yangu mkuu kwa kuchagua kuwa mzalendo bila shuruti.

mgonga ndege huenda alikuwa mr Simbambiti mdogo wake MBITIYAZA. au naye alikuwa na ndege ya asili baada ya plug kusumbua!


hahahaahha huenda pia!watu wa ccm utawajua kwa comments zao za kulazimisha mambo !lol
 
Back
Top Bottom