MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,009
- 2,173
Gazeti la NIPASHE, leo Tar 18, ukurasa wa 14 lina habari inayosema;
"Chadema yaapa kula sahani moja na Profesa Mwandosya"
Ni maelezo jinsi Mwandosya anavyokihujumu chama hicho kwa kuwarubuni viongozi wa CDM mkoni Mbeya. Anahusishwa pia na tukio la Shitambala kuhamia CCM na katibu wa CDM anasema ataanzisha operesheni kupambana naye kwa kuanika mabaya yake serikalini na ktk chama.
Mwandosya alijibu malalamiko kwa kusisitiza kwamba wakati Shitambala anahama, Kikwete alisema kahama bila shinikizo.
--------
Maoni yangu ni kwamba, nadhani tunahitaji sheria ya kuvilinda vyama juu ya mbinu/hujuma (conspiracy). Imekuwa ni kawaida kutumia pesa ili kukiharibia chama fulani. Iwe CCM, CDM, CUF, nk. Huu ni mtindo wa kitoto ambao unastahili kukomeshwa kwa sheria.
Kuhusu Mwandosya nadhani anajijengea tatizo. Baada ya kuwa amekaa serikalini muda wote huo naamini kuna mengi ambayo yakitajwa ni ya kumuangusha kisiasa na tumeyasikia sana na udhaifu wake ni mwingi.
Mbaya zaidi namuona kama anatengeneza udhaifu kwa makusudi maana anajifahamu kabisa kwamba ktk CCM yeye bado ni dhaifu. Ndo maana hata nafasi ya kamati kuu aliipata kwa taabu. Najua ni tamaa ya kurudi kwenye mbio za urais lakini angeachana na CDM kwa sasa aone jinsi Upepo unavyovuma ndani ya CCM. Tatizo lake amekuwa haonyeshi kabisa kwamba ni profesa, mtu aliye na sifa za kujifunza na kuiga siasa za mafanikio.
Shauri yake!