Mwandishi wa habari wa Mwananchi afariki dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi wa habari wa Mwananchi afariki dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mayenga, Jan 23, 2012.

 1. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,758
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 23 January 2012 08:00[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][​IMG] Beatus Kagashe

  Mkinga Mkinga na Aidan Mhando
  MWANDISHI wa habari wa Kampuni Mwananchi Communications Limited (MCL), Beatus Kagashe (31), amefariki dunia juzi usiku.Kifo cha mwandishi huyo aliyekuwa akiandikia gazeti la The Citizen, kilitokea katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya damu baada ya kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Aga Khan kwa miezi miwili.

  Msemaji wa familia ya marehemu Gasper Mikimba alisema, Kagashe alifariki mnamo saa 2:45 usiku na kwamba familia iko katika mipango ya mazishi ambayo yatafanyika Bukoba mkoani Kagera. Alisema mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda huko Jumanne na mazishi kufanyika Jumatano.

  "Bado tunaendelea na mipango ya mazishi... lakini nadhani tutasafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Bukoba siku ya Jumanne kwa ajili ya mazishi," alisema Mikimba.

  Alisema kifo cha Kagashe kimeacha mshtuko mkubwa katika familia,jamii pamoja na taifa kwa ujumla hasa ikizingatiwa kwamba alikuwa bado kijana aliyetarajiwa kulijenga taifa lake.

  Marehemu Kagashe alizaliwa Februari 23, 1981 mkoani Kagera na alipata elimu ya msingi katika Shule ya Bilele iliyoko Bukoba Mjini kati ya mwaka 1990 na 1996, alijiunga na Shule ya Sekondari Ihungo kuanzia mwaka 1997 mpaka 2000 kabla ya kujiunga na Shule Sekondari Mpwapwa kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

  Mwaka 2004, alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusoma kozi ya uandishi wa habari (Bachelor ofn Arts Journalism) katika Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (IJMC) alipohitimu mwaka 2007. Alijiunga na masomo ya shahada ya uzamili katika masuala ya utawala (Masters in Public Administration) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2010 na kuhitimu Novemba mwaka jana.

  Mhariri Mtendaji wa Gazeti la The Citizen, Bakari Machumu alisema amepokea kifo cha marehemu Kagashe kwa masikitiko makubwa. Alimwelezea kama kijana aliyekuwa mpenda watu na mwenye kusimamia alichokiamini.

  "Tulidhani alikuwa anaendelea vizuri na matibabu... nimepata mshtuko kusikia kwamba Kagashe ameaga dunia. Nilikutana naye hospitali wiki moja iliyopita alionekana kuwa na nguvu ya kupambana na ugonjwa wake," alisema Machumu.

  Alisema idara yake imepoteza hazina ambayo Mwananchi Communications Limited ilikuwa imewekeza kwa manufaa ya kampuni pamoja na gazeti.

  Alisema marehemu Kagashe alikuwa ni zao la utaratibu wa kusaka vipaji kutoka vyuo vya elimu ya juu, programu iliyoanzishwa na Kampuni ya Mwananchi mwaka 2007 akiwa miongoni mwa vijana watano wa kwanza wa kundi la kwanza la programu hiyo.

  "Kagashe alitokana na mpango wa kusaka vipaji katika vyuo vya elimu ya juu...mamia ya wahitimu wa vyuo vikuu nakumbuka walijitokeza lakini Beatus Kagashe alikuwa miongoni mwa wanafunzi watano bora, hivyo kujiunga na kozi maalumu huko Nairobi,Kenya," alisema Machumu.

  Kagashe aliajiriwa aliajiriwa na Mwananchi Communications Limited, kampuni inayochapisha magazeti ya The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti mnamo mwaka 2008. Ameacha mjane, Doroster Kagashe na mtoto Emmanuel Mujuni ambaye ana umri wa mwaka mmoja.

  Chadema wamlilia


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa, taarifa za kifo cha Kagashe. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Tumaini Makene imesema: "Kwa wale waliokuwa wakimfahamu marehemu Kagashe, watakubali kuwa alikuwa mmoja wa waandishi makini, waliokuwa wakiamini jamii ya Watanzania inaweza kufanya mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii."

  Alisema kwa kutumia vema taaluma yake, akiongozwa na maadili ya tasnia ya habari, alishirikiana na Watanzania wenzake katika kuelimisha, kuhabarisha, kuhamasisha na kuburudisha umma, katika masuala mbalimbali kupitia kalamu yake.

  "Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake na kuwaombea kwa Mungu awape moyo wa subira katika wakati huu mgumu wa majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao," alisema Makene
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Source Mwananchi.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  RIP mkuu
  roho yako ipumzike mahali pema peponi
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  ukiangalia vizuri academic and career profile yake ilikuwa inaenda vizuri sana na angeongeza miaka 10 angeliweza kuonyesha makubwa zaidi.
  Lakini mipango ya Mungu, haipingwi wala kubishaniwa!
  RIP Beatus
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,034
  Likes Received: 747
  Trophy Points: 280
  RIP Kagashe.
   
 5. I

  Igwachnya Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  RIP bro. Wewe mbele, sisi nyuma yako tunafuata
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Poleni sana ndugu na wafanyakazi wenzake
   
 7. papason

  papason JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wafiwa

  Mwenyezi Mungu awape nguvu Ktk kipindi hiki kigumu
   
 8. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  we kimelea bwana.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  R.I.P mwandishi
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  kazi yake mola haina makosa. naamini kama Mungu angeuliza nani afe, halafu tukapiga kura za siri, LOWASA angeibuka kidedea, KIKWETE angefuata, Mkandala na maboko wangekufa siku nyingi. Sasa badala ya waovu kufa, MUNGU anamchukua kijana mwenzetu, ambaye bado anahitajika na familia yake n.k
   
 11. M

  Malaika12 Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa aman.amina
   
 12. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  RIP... hivi hakuwa member humu???
   
 13. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Too soon umetuacha R.I.P
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  naomba kuuliza
  mayenga wewe na yule mbunge wa ccm ni mtu mmoja?????/
   
 15. M

  Malunde JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mwenyezi Mungu awafariji wafiwa wote, ampe nguvu mjane na amlinde mtoto na kuumpa neema ya kufikia utu uzima afikie mahali pa kulitumikie taifa hili kama baba yake alivyo kuwa analitumikia
   
 16. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,758
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  hapana mkuu,wala hatufahamiani
   
 17. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,784
  Likes Received: 593
  Trophy Points: 280
  Mungu akulaze mahali pema peponi ndugo beatus kagashe...nakumbuka jinsi tulivyokua tukicheza wote mpira wa miguu tumaini shule ya msingi nakumbuka jinsi tulivyochaguliwa ihungo sec school na tulivyokua tukiaamka mapema kwenda shule napia nakumbuka jinsi tulivyokua tukifanya mazoezi ya kubeba vyuma any way mengi ya kukumbuka......may god rest ur soul in eternal peace......amen
   
 18. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  r.i.p ndugu
   
 19. I

  Igwachnya Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Toka nianze kufiwa sijawah kukutana na umati mkubwa vile kwenye ibada ya mazish. Kweli marehem alikuwa mtu wa watu. Nape aliongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa masters Mzumbe.
   
 20. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Rest in Peace Kagashe...! Pole kwa familia na marafiki zake na Mwananchi!
   
Loading...