Mwandishi wa Habari wa ITV, Renatus Mtabuzi Avamiwa njiani, avunjwa bega na kunyang'anywa Simu zake na pesa, akimbizwa MOI

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,126
Mwandishi wa habari Renatus Mutabuzi(pichani) amevamiwa na watu wasiojulikana na ( 608 X 640 ).jpg

Je, watekaji na wauaji bado wapo? na je ni nini kosa lake?

====

Mtangazaji wa ITV Renatus Mtabuzi, akiongea kwa Uchungu na Maumivu, ameiambia JamiiForums kwamba, Jana muda wa saa mbili na nusu Usiku, amevaiwa na Watu Wawili waliokuwa kwenye pikipiki na kupigwa sana hadi akavunjwa bega.

Amedai kuna Mtu alimfuata nyumbani kwake Madale Nguzo (Jina limehifadhiwa) wakatoka naye waende kutoa hela kwenye kwenye simu Dukani. Huyu mtu aliyemfuata alikuwa na Pikipiki lakini wakati wanaenda Dukani akakata kuondoka na Pikipiki hivyo ikabidi waende kwa Mguu.

Walipofika Sehemu yenye giza Wakavamiwa na Watu Wawili waliokuwa kwenye Pikipiki wakaanza kumpiga na kumkagua Mfukoni. Baada ya hapo wakaondoka. Yule jamaa aliyekuwa naye hakutoa msaada wowote, wala hakupiga kelele wakati alikuwa eneo la tukio.

Baada ya Kuondoka ikabidi waende Polisi kutoa taarifa na kuvamiwa, ajabu huyo mtu aliyekuwa naye alipofika Polisi akabidisha mjadala kwamba Renatus amevunjika bega wakati anakimbia. Kauli hiyo limfanya Renatus kuhisi huyo mtu aliyemfuata anahusika.

Kwa sababu Renatus alikuwa ana maaumivu, alikimbizwa Hospitali ya Kitengule Tegeta ambao nao Wakamuamishia MOI Muhimbili kutokana na kwamba hawakuwa na Uwezo ya kumudumia kutokana na jinsi alivyo Vunjika.

Baada ya Kupata huduma MOI waliweza kumruhusu arudi nyumbani leo asubuhi.

Hivyo hajui kama yule mtu Polisi bado Wamemshikilia au Wamemuachilia.

Tutaendelea kuwajulisha kitakachojiri.

Pole sana Renatus.
 
Moderator sijawahi kuzusha , naomba uwe na imani na mimi , huu uzi uliuficha bila sababu ya msingi
Si kila siku humu mnasema ITV imekuwa kama TBC kwa sasa??

Au labda utuambie huyo bwana katoa habari gani ambayo imemchanganisha na hao unaodhania ndio wamemshambulia
 
Si kila siku humu mnasema ITV imekuwa kama TBC kwa sasa?

Au labda utuambie huyo bwana katoa habari gani ambayo imemchanganisha na hao unaodhania ndio wamemshambulia

Sisi kazi yetu ni kutoa taarifa tu mjomba
 
Baada ya Kuondoka ikabidi waende Polisi kutoa taarifa na kuvamiwa, ajabu huyo mtu aliyekuwa naye alipofika Polisi akabidisha mjadala kwamba Renatus amevunjika bega wakati anakimbia. Kauli hiyo limfanya Renatus kuhisi huyo mtu aliyemfuata anahusika.

ANAJULIKANA
 
Back
Top Bottom