Mwandishi wa Habari wa ITV Austere Malivika

Nasakadoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
343
Reaction score
169
Sina hakika saana kama jina nitalipatia, maana huwa analitaja haraka saana akiwa anajitambulisha kila akiripoti habari…

Jina lake la mwisho kama sikosei ni Marivika…
Huyu Baba nataka nimjue na nijue… je huwa ujasiri wa kuripoti habari za mapigano yanayotokea huko Kongo anautoa wapi?
Je ni mwajiriwa wa ITV ya Tanzania? Maana ndo huwa anaripoti habari zoote za Kongo kwa ITV… je ni mtanzania?
Leo alikuwa amepanda ndege(helikopita) ya jeshi la Congo DRC wakiwa na Jeshi la UN, Walikuwa wanafurumua kwa makombora wale wapiganaji wa Burundi/Rwanda walio kwenye milima ya Congo huko Kivu…
Huyu Mwandishi huwa anaripoti hzi habari za mapigano akiwa ndani ya wapiganaji… sijui huwa anajiamini vipi! Na je ni ITV ndo mwajiri mkuu??
Karibu wadau… naomba nijuzwe!
10917835_830445003683773_3663862521575043882_n.jpg
 
an aitwa Austere Malivika, hua namkubali sana na ndio mwandishi wa habari mahili kattika wandishi wa habari ITV. Msimu wa Christmas alikua dar. Juzi kati gari yake ilishambuliwa kwa risasi bahati nzuri risasi hakuna iliyo mpata. Hali hiyo ilipelekea vyombo vya habari kugoma kwa kusitisha matangazo siku nzima. Jamaa namkubali sana. ana uwezo wa kureport kwa lugha zaidi ya nne. Mia
 
Huyo ndio James Bay wa Itv.

Ahaaa kumbe…
naanza kumpata sasa! ITV walimpata pataje huyu jamaa…
Is a Tanzanian?
 
Sina hakika saana kama jina nitalipatia, maana huwa analitaja haraka saana akiwa anajitambulisha kila akiripoti habari…

Jina lake la mwisho kama sikosei ni Marivika…
Huyu Baba nataka nimjue na nijue… je huwa ujasiri wa kuripoti habari za mapigano yanayotokea huko Kongo anautoa wapi?
Je ni mwajiriwa wa ITV ya Tanzania? Maana ndo huwa anaripoti habari zoote za Kongo kwa ITV… je ni mtanzania?
Leo alikuwa amepanda ndege(helikopita) ya jeshi la Congo DRC wakiwa na Jeshi la UN, Walikuwa wanafurumua kwa makombora wale wapiganaji wa Burundi/Rwanda walio kwenye milima ya Congo huko Kivu…
Huyu Mwandishi huwa anaripoti hzi habari za mapigano akiwa ndani ya wapiganaji… sijui huwa anajiamini vipi! Na je ni ITV ndo mwajiri mkuu??
Karibu wadau… naomba nijuzwe!

Huwa ni reporter wa sauti ya Amerika.Nadhani na itv wanamtumia tu, ndio kazi za ma reporter wa kimataifa wanatakiwa kuwa kifo nje inje, sio hapa sam mahela anaripoti kwa mbwembwe!!!
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha…
 
Namii huyu jamaa namuaminia sana, bila shaka pia analipwa hela ndefu, unajiamini na anajituma sana, lkn napendekeza ingefika mahala wana wa exchange, mmoja wao hapa bongo anapelekwa Congo kwa mwezi mmoja hivi kuripoti na malivika anakuwa hapa bongo, inawezekana eti wakuu, mwaonaje.
 
Bila shaka atakuwa Mkongoman.

Hilo jina la mwanzo tu utagundua ni Francphone, yaani majina ya lafudhi ya Kifaransa. Hivyo inaonyesha live ni Mkongo! Austere- Haiwez kuwa ni jina la Kitanzania. Ila jamaa ni jasiri. Lakini Watanzania wanapaswa kumsifu pia Suzane Mungi( sasa yuko TBC). Wakati yuko BBC aliripoti vita vya Iraq Fallujah, Mosul na Baghadad akiambatana na US Forces. Kama kuna mtu ana video clip yake atuwekee, au kama mwenyewe yupo humu awasiliane na Mods. Anastahili sifa. Amerudi nyumbani naona kapwaya.
Nadhan mfumo wetu hapa Tanzania hauko vizuri. Watu wote walioletwa wakiwa wamedeliver vizuri kwa wazungu huko, wakija hapa Tanzania wanaishia vibaya kabisa. Mifano ni mingi kama:-
Omari Nundu, Tiddo D Mhando, Prof Tibaijuka,Prof Muhongo, Mama Mungi Suzane( japo yupo ila umahiri ule akiwa BBC hapa hauonyeshi), kutaja Watanzania wachache ambao walituwakilisha vema ughaibuni lakini hapa nchini mchango wao ukaishia pabaya.

Hapa yapasa tukubali tu kwamba MFUMO wetu wa kuendesha mambo yetu ni mbovu. Watu walewale haiwezekani Ulaya wanadeliver na kuacha legacy, wakija hapa wanakuwa incompetent! Sorry katika list nilimsahau Balal Daud( R.I.P- citation needed to prove his death)!
 
Namii huyu jamaa namuaminia sana, bila shaka pia analipwa hela ndefu, unajiamini na anajituma sana, lkn napendekeza ingefika mahala wana wa exchange, mmoja wao hapa bongo anapelekwa Congo kwa mwezi mmoja hivi kuripoti na malivika anakuwa hapa bongo, inawezekana eti wakuu, mwaonaje.

Akitoka hapa kwenda kule itamuwia vigumu kutokana na lugha, Kiswahili chao kule kina utofauti na cha Dar kiasi pia kinachanganywa sana na kifaransa. kimbisi mbisi mfano wa kiswahili cha kule

Kuuza=kununua
Kuuzisha=kuuza teh teh teh,umeona kazi hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Huwa ni reporter wa sauti ya Amerika.Nadhani na itv wanamtumia tu, ndio kazi za ma reporter wa kimataifa wanatakiwa kuwa kifo nje inje, sio hapa sam mahela anaripoti kwa mbwembwe!!!

Nimecheka sana hapo kwa sam mahela.
 
Back
Top Bottom