PostGE2025 Mwandishi wa habari wa Ayo Tv afutiwa mashtaka ya uhaini na DPP

PostGE2025 Mwandishi wa habari wa Ayo Tv afutiwa mashtaka ya uhaini na DPP

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru na kuwafutia mashtaka ya uhaini washtakiwa wanne akiwemo Mwandishi wa Habari wa Ayo Tv, Godfrey Ng’omba. Wengine walioachiwa ni watoto watatu wa kiume wenye umri wa miaka 13, 16 na 17 (waliokuwa mahabusu ya watoto) ambao kwa pamoja walikuwa wakishtakiwa kwa kesi ya uhaini.

Uamuzi huo umefikiwa leo Jumanne Novemba 25, 2025 na Hakimu Mkazi Regina Oyier, baada ya Wakili wa Serikali kuieleza Mahakama kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hana nia ya kuendelea kuwashitaki washtakiwa hao. Upande wa Jamhuri uliieleza Mahakama kuwa mashauri hayo mawili yamepangwa kwa ajili ya kutajwa ila DPP kwa niaba ya Jamhuri hana nia ya kuendelea kuwashitaki washtakiwa chuni ya kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA),sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Washtakiwa hao wanne walikuwa wakishtakiwa na wenzao 59 katika kesi ya uhaini ambapo wanawakilishwa na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Arusha, Khamisi Mkindi.

Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa mawili ambayo ni kula njama ya kutenda kosa kinyume na kifungu cha 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Wanadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba mosi hadi 29,2025 walifanya njama mbalimbali za kutenda kosa la uhaini.

Kosa la pili linalowakabili washtakiwa hao ni uhaini kinyume na kifungu cha 39 (2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Hakimu Regina alifikia uamuzi huo wa kuwaachia huru washtakiwa hao baada ya Jamhuri kueleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea kuwashitaki,ambapo pia wameachiwa bila masharti yoyote. Jana Jumatatu Novemba 24, 2025, washtakiwa 24 wa kesi za uhaini mkoani Arusha waliachiwa na Mahakama hiyo na kuwa watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja na kutakiwa kuripoti mara moja kila mwezi katika Kituo cha Polisi.

Chanzo: Mwananchi
 
Ukitaka kujua kuwa tunaishi kwenye banana republic na jeshi la polisi ni jeshi la vilaza jiulize huyo mtoto wa miaka 13 aliingiaje kwenye kesi hiyo!

Hawa watu ni wauaji wasiofikiri kabla ya kutenda na matendo yao ya ile siku ya uchaguzi ndio yatasababisha watu waandamane wakiwa wamejihami. Yaani itakuwa moto kwa moto na ikifika hali hiyo ujue hatuna nchi tena!
 
Maana yake walikuwa wanaokota kila waliyemuona
 
Hata wangenyonga au kumfunga maisha ile picha ya mauaji ya mama na kichanga chake tumboni kwa risasi imeonekana dunia nzima
 
Hapo ni biashara ya kuuza uhuru mwenye pesa unarudi kwenu
 
Back
Top Bottom