Ni hulka ya viongozi dhaifu kutumia nguvu pale inapotokea kwamba wameshindwa kuwashawishi watawaliwa kwa maneno kupitia majukwaani. Kwa kuwa CCM hivi sasa haina tena uwezo wa kuwashawishi watanzania wakaikubali, njia rahisi na ya mkato kwake ni mabavu.
Amini nawaambieni CCM ndo itakayoleta vita katika nchi hii. Maana ndiyo yenye polisi, jeshi na bunduki. Kwa hiyo kwao kuanzisha vita haitakuwa shida. Wakati wenzetu kule Rwanda waliuana kwa misingi ya ukabila, sisi tutauana kwa misingi ya vyama na dini. Na waanzilishi wa haya yote ni CCM, ndiyo hawa CCM waliopanda mbegu ya udini ambayo hivi sasa imeota na kupevuka sana mijini na mashambani huku BAKWATA wakiajiliwa kuimwagilia maji mbegu hii ili ikue na kutoa mazao. Hatujui mazao hayo yatakuwa ya aina gani na yenye madhara kiasi gani hapo yatakapokomaa.
Ni CCM hao hao walianzisha utaratibu wa kuchelewa kutangaza matokeo katika majimbo yale yote ambayo upinzani ulielekea kushinda au ulishinda. Kigugumizi hiki ndicho kilichopelekea vurugu kwenye baadhi ya majimbo huko Arusha, Mwanza na Mbeya.
Ni CCM pia ambayo imewageuza watanzania wa Mbagala na Gongolamboto kuwa specimen za kufanyia mazoezi ya jeshi, huku mamia ya watu wakimwaga damu bila sababu. Mwisho wa ubaya huu, hapatatosha, nyie subirini tu. Nawaambieni hapatatosha. Kama mnaona hii nchi ni kubwa sana, basi hapatatosha.