Mwanaume wa kweli anabaki na mwanamke mmoja

Mwanaume wa kweli anabaki na mwanamke mmoja

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,678
Nasema na wewe mwanamke

Usitafute upendo kwa Mwanaume kwani ni wajibu wake kukupenda. Ila ukiona hakuna upendo juu yako na upo nae ujue kwamba kuna anayependwa.

Msijidanganye kwamba wanaume hawana upendo bali jiulize kwanini hakupendi wewe?

▪ Kukuhudumia ni wajibu wa Mwanaume.
▪ Matunzo ni wajibu wa Mwanaume.
▪ Kukulinda ni wajibu wa Mwanaume.
▪ Haki ya tendo la ndoa wajibu wa Mwanaume.

Wala usijitaabishe kulazimisha hayo, kwani ndiyo sehemu ya uhalisia wa mume lakini ikiwa ili uyapate hayo ni mpaka upige kelele rafiki unakula upepo hapo.

Wanawake mnajidanganya katika mabadiliko kwamba unayoyaona leo ni changamoto na yatakayokuja baadaye mnayatarajia pengine hiyo ni imani lakini kwenye ishu ya mapenzi hatuna sababu ya kutarajia Kwani hilo sio fumbo la Mungu.

Mapenzi ni utashi wa ki bin adam, kukubali ama kukataa ni uwezo wa akili na Moyo. Kwanini hakuna mwanzo mbaya kwenye mapenzi? Siku zote Mwanzo unakuwa mzuri kwani kila mmoja na shauku ya hitaji lake kutimia ila siku zinavyokwenda ikiwa wawili waliingia kwa sababu zao penzi linakwenda mrama.

Ishi kwa uhalisia wako na ukubaliane na uhalisia uliopo ili akija Mwanaume akaonyesha kukupenda mshike huyo, Maana ni nadra sana kukuta Mwanaume ametoa package yake ya upendo ila ni rahisi kwa aliyeandikwa kwa moyo wake.

Wanawake wengi mnaolewa na wanaume wa watu. Yaani badala ya kuolewa na mwanaume wako kwa sababu ya muda kuyoyoma unajitwalia mume wa mwingine rafiki itabaki historia kwamba uliolewa ila kwa uhalisia utakuwa unaishi na mume wa mtu kutwa anatanga kumtafuta wa kwake na wewe unabaki ukilalama kama ndama wa mbuzi

▪ MUME wako hawezi kukuacha ukilia.
▪ MUME wako hawezi kukudharau.
▪ MUME wako hawezi kukuwekea mipaka.
▪ MUME wako hawezi kukupa UPWEKE.
▪ MUME wako hawezi kukusaliti.
▪ MUME wako hatajaribu kukuacha PEKE yako.
▪ MUME wako hawezi kukulinganisha na kazi zake.
Na mengine yanayofanana na hayo, Sasa wewe endelea kungojea NDOA IREJEE KWENYE MISINGI YAKE huku aliyekuoa sio MUME wako ila haraka zako ukaparamia MUME wa watu, Kumbuka mkewe YUPO ANAMNGOJEA muda ukifika ndipo utabaini MBIVU NA MBICHI. 😎
 
Mwanamke mmoja Ni mama yako peke yake.!!
Wengine wooote wanaweza kuwa zaidi ya mmoja.
Ni uwezo wako tu wa kuwahudumia.
Upungufu wa nguvu za kiume na umaskini na uvivu wa kutafuta hela usihalalishe uongo.
Unaweza kuamua kuoa wote pamoja au ukawa serial polygamist Kama Trump, Mengi nk.
Haya mengine ya kutishiana sijui biblia au Nini Ni mambo ya binadamu tu.
Hakuna sehemu Mungu kaweka sharti la kuwa na mke mmoja.
Hakuna.!!!
Watu wamechukua relative words na kuziunganisha unganisha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke mmoja Ni mama yako peke yake.!!
Wengine wooote wanaweza kuwa zaidi ya mmoja.
Ni uwezo wako tu wa kuwahudumia.
Upungufu wa nguvu za kiume na umaskini na uvivu wa kutafuta hela usihalalishe uongo.
Unaweza kuamua kuoa wote pamoja au ukawa serial polygamist Kama Trump, Mengi nk.
Haya mengine ya kutishiana sijui biblia au Nini Ni mambo ya binadamu tu.
Hakuna sehemu Mungu kaweka sharti la kuwa na mke mmoja.
Hakuna.!!!
Watu wamechukua relative words na kuziunganisha unganisha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee...mbona unasikitisha sana kama vile Adamu aliumbiwa Wanawake wawili na Mungu?

Umeniudhi sana kumuhusisha Mungu ktk tamaa zako za anasa, usirudie tena[emoji35]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee...mbona unasikitisha sana kama vile Adamu aliumbiwa Wanawake wawili na Mungu?

Umeniudhi sana kumuhusisha Mungu ktk tamaa zako za anasa, usirudie tena[emoji35]

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwanza Kuna maswali mengi hayajajibiwa kuhusu binadamu wa mwanzo.
Na hakuna anayeweza kujibu. Watu wanaleta hisia zaidi. Tukifuatilia kwamba kilichoandikwa ndio sahihi,
Adam alikuwa na watoto wawili wa kiume, walioa Nani?
Baada ya kaini kumuua habili imeandikwa aliwekwa alama "amelaaniwa kaini, mtu asimguse" ujumbe ulikuwa kwa ajili ya nani?
Na baada ya Eva kufa tunaambiwa Adam alioa mke mwingine, alitoka kizazi gani!?
Biblia na dini sio Mungu aliyeviweka.
Ni namna tu wanadamu waliamua kumtafsiri Mungu na kuwaongoza wengine.!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom