Watoto hawapimi upendo kwa sababu hizo tuu...Baba mwenye upendo kwa watoto ni zaidi ya hayo ya fedha za matumizi au ada..upendo haujifichi au hauwezi kufichwa na maneno fulani ya mama. Mwanaume mwajibikaji hahitaji kujionesha kwa mtoto ni nini katoa au hajatoa.. isipokuwa wale irresponsible fathers wanahitaji sana huo ushauri wako ili wajioneshe kuwa na wao wapo.MWACHIE MBELE YA WATOTO NA UMWAMBIE NA MATUMIZI YAKE, NA WATOTO WASIKIE, USIJE KUISHI MAISHA YA UPWEKE UZEENI.
[emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427]
MWANAUME
Unamwachia mkeo hela ya chakula chumbani. Mke anatoka na kapu, anaenda kununua chakula. Anapika, anawaambia watoto, "njooni wanangu mle. Nimewapikia chakula kitaaamu!" Watoto wakishakula Wanasema "Asante Mama".
MWANAUME
Unamwachia mkeo hela ya nguo za sikukuu chumbani,
Kesho yake anatoka kwenda kununua nguo. Akirudi anawaambia, "wanangu nimewanunulieni nguo za sikukuu, njooni mjipimie!" Watoto wakishajipima, anawaambia, "Wanangu mmependeza eeeh! Si mnaona ninavyowapenda!?" Watoto wanafurahi na kusema, "Asante Mama".
MWANAUME
Kila aina ya pesa ya matumizi unamwachia mkeo chumbani...
MWANANUME
Ukifika muda wa kutoa ada unamkabidhi mkeo hela chumbani. Kesho yake mkeo anawaambia watoto kuwa anaenda kuwalipia ada ya shule. Akirudi anawaambia, "Wanangu nimeshawalipia ada, na gari za shule zitakua zinawapitia. Nataka msome wanangu ili baadae mje mnitunze". Watoto wanasema, "Asante Mama".
KIBAYA ZAIDI:
Ukifika muda wa kutoa adhabu, mkeo yeye hatoi adhabu. Anawaambia Watoto, "ngoja baba yenu arudi!" Na wewe ukirudi unaelezwa na mkeo matatizo ya wanao. Unachukua bakora unawaadhibu watoto bila kujua kuwa unazidi kujenga uhusiano M'BAYA na Wanao.
NGUMU KUMEZA
Ukifika uzeeni, watoto wako hawana KUMBUKUMBU yoyote Ya mema uliyowafanyia.
NA UKUMBUKE KUWA:
MTOTO ANAANZA KULISHWA SUMU YA MANENO KUTOKA KWA MAMAYAKE KUANZIA UMRI WA MIAKA 9 HADI 15.
MWANAUME KUWA MAKINI SANA
ZINGATIA HAYO KWA MAISHA YA UZEENI.
Upendo wa baba kwa watoto huwa haujifichi hata iweje..utaonekana tuu.
Watoto wanao uwezo mkubwa mna wa kumtambua mtu anayewapenda na huwezi kumdanyanya hata iweje.mtoto akikuangalia usoni tuu anajua unampenda au unazuga tuu.
Baba unawahi kurudi nyumbani..unacheza na watoto ...unawasaidia homework..unatoka nao mazoezi au matembezi madogo madogo..unaenda nao kanisani au msikitini..unawafundisha kwa vitendo study za kazi..mf.wanakuona unapenda bustani..mifugo..nk watakuiga na kukupenda sana..
Yaani ukirudi tuu kutoka kazini utaona wanavyokukimbilia mpaka wanaanguka ili walao kila mmoja awe wa kwanza kukupokea..
Ukirudi lazima utakuwa umebeba chochote mkononi..mboga..vitafunwa..mahitaji mahitaji madogo madogo ya nyumbani..
Sabuni,sukari,gesi..hata kamfuko ka matunda tuu..sio kila siku bali kila unapojaliwa..
Watoto watakupenda sana tuu..watoto wa kiume watatamani wakiwa wakubwa wawe kama baba yao.
Watoto wa kike watatamani sana wakija kuanza familia Basi wapate mwenzi ambaye anaupendo kama baba yao kwa familia.
Huhitaji kujionesha onesha kwa watoto eti wewe ni baba ndio uliotoa hiki wala kile..
Hata kama mama angekuwa na kipato kikubwa kuliko wewe lakini watoto wanajua unawapenda aaa watakupenda tuu hata mama awafundishe ubaya gani..labda mmoja tuu anaweza akawa against wewe but wengine watakuheshimu tuu..
Wanaume wengi ni timeless na familia..hawana muda na watoto eti kujifanya wapo bize na utafutaji..akipata nafasi anaona ni heri akautumie huo muda..bar, kuangalia mpira,kucheza bao,vijiweni au hata kuzurura tuu kwa marafiki zake eti wanampa dili..
Kuwa Baba wa familia ni zaidi ya kuprovide matumizi au ada..