Mwanaume unamchukuliaje mwanamke wa aina hii

Mwanaume unamchukuliaje mwanamke wa aina hii

Mimi nikishajua kiumbe anakojoa kachuchumaa, kwangu ni Mwanamke tu. Haijalishi ana Elimu, Pesa au wadhifa gani.

Ni Mwanamke tu kwangu
 
Ni kweli Mkuu, walio wengi pasua kichwa, na ikitokea amenunua gari kwa pesa yake atakunyanyasia mpaka ujione hufai, yaani ni wachache sana eti ananunua gari halafu akupe heshima na uhuru na gari lake, oa mwanamke maskini ndio utafurahia ndoa, mpaka aje kubadirika na umri wenu unakuwa umesonga mbele
Si kweli Mkuu. Kuna Wanawake Masikini ila.Kiburi na dharau kama.wamechanjia. Nina Mifano hai kabisa na inayonihusu.
 
Mkuu....
Hata uwe na kipato kunizidi, pesa kunizidi, elimu kunizidi yooote hayana maana ikiwa Kama Mimi mume wako sinto weza kuitambua nafasi yangu kusimama Kama kichwa cha familia.
Pamoja na yote hayo uliyo yataja, ikiwa mimi Ni mumeo basi tambua kwamba nafasi na wajibu wangu lazima uwe palepale kama mume na baba wa familia.
One way or another, najaribu kukuelewa kwamba wanaume wengi wa leo wanawahofia/wanawaogopa kuwatongoza wadada wenye wamewazidi elimu, kipato, maendeleo na kadhalika....
 
Back
Top Bottom