Mwanaume Saudi Arabia ampa mkewe talaka kwa kosa la kupuuza meseji zake WhatsApp

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
alalam_635357783784925161_25f_4x3.jpg

Pamoja na mwanamke kujitetea sana, lakini mwanaume alikataa katkata kumsmehe mke wake ambaye walidumu katika ndoa miaka miwili.

Mwanaume alisema kwamba muda wote akimtumia meseji whatsApp, Mke wake huyo alikua hajibu hata meseji moja wakati muda wote anamuona online na akituma meseji anaona blue tick kwamba meseji imesomwa.

Mwanamke alijitetea akisema muda mwingi anakuwa yupo anaongea na simu hata Meseji zinapoingia anakua yupo kwenye maongezi na rafiki zake, hivyo hapati muda wa kuzijibu, hata akipata huo muda ujumbe unakua ushaisha muda wake.

Mwanaume aliishiwa uvimilivu kwa kile alichodi kwamba si mara ya kwanza au yapili hajibiwi meseji zake whatsapp, Hivyo ameamua kumpa talaka ili akaongee na hao ndugu zake na Marafiki Vizuri.

Inasemekana huko Saudi Arabia, Mitandao ya kijamii inaongoza kwa kuvunja ndoa za watu

=======================

A man in Saudi Arabia has been granted a divorce because his wife ignored his WhatsApp messages.

Despite the fact she was constantly using her cell phone, reports Gulf News, the wife would not respond to messages from her husband.

The pair had been married for two years.

Gulf News reports that the husband, in his 30s, became exasperated because his wife spent so much time on her phone.

He claimed she neglected looking after the home and taking care of their child.

The wife claimed she needed her cell phone to keep in touch with her friends and family.

So, in desperation, the husband used WhatsApp to try and talk to his wife but she ignored his messages because, she claimed, she was too busy talking to her friends.

That was the final straw for the husband who sought and got a divorce.

Chanzo cha habari ni Nydailynews
 
Naichukia sana whatsapp esp. Yale ma group! Wenzetu kina dada wanayachukulia serious sana.. Utakuta mtu yuko busy masaa 24 na whatsaap , hana time na mumewe.. Mtoto wa kike ana magroup 10
 
Naunga mkono hoja. Mume kwanza, marafiki baadae. At least angejitetea kuwa kazi zimemzidia, ila kuongea na marafiki.....
 
kumbe tuachane kwa sababu yeyote? kwa wale wanaoachana na wana watoto, ni malezi gani watoto wanapata? watoto wanajifunza nini? hadhi ya mwanamke inashuka kwa kuachwaachwa! ndiyo maana Yesu alikataza kabisa talaka. inajeruhi sana. familia zinachukiana, yaani we acha tu! natambua machungu wanayopata wanaoamua kutoa talaka. kama hii ya whatsapp kwakweli inauma mtu kutomjibu mwenzie, ni tabia mbaya sn. inaumiza kutokuwa msikivu japo kumpa talaka inaumiza zaidi. nawasihi ndugu zangu tusiwe vikwazo kwa wengine na tusiachane kiholela. utaoa mwingine naye atakukera kwa jambo fulani. utaacha wangapi?
 
Back
Top Bottom