Mwanaume mwenzangu, soma haya kuyaokoa maisha yako

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,790
3,020
Habari za asubuhi wakuu.
Wanaume matatizo yanayotukabili mbele ya wanawake nimeona niandike walau tusaidiane kwa sababu sisi ni dhaifu kwa wanawake hilo halina ubishi na huwezi ishi bila mwanamke labda kama huna mpango na familia au watoto na haja zako unajinyima hivyo ni bora tubadilishane mawili matatu kwa faida yetu sote.

Nimekua nikitizama namna ya kuhandle stress za mapenzi kati ya mwanamke na mwanaume na kufahamu mambo kadhaa.

KWA MWANAMKE
-Mwanamke kisalitiwa hutafuta furaha nyingine badala ya kujutia, hii njia humsaidia sana kusahau matatizo yaliyomkuta.

-Mwanamke hulia machozi hii husaidia kutoa sumu iliyoko moyoni na huwa mwepesi moyoni hivyo kuwa tayari kutafuta furaha nyingine ili kuponya kidonda chake.

-Mwanamke huwa na list ya watu wake kadhaa ambayo anajua shida ikitokea basi ata move na hiyo list madam anajua hawezi kataliwa muda wowote kwa maana yeye ni mwanamke basi mambo kwake ni fresh. Anapopata tatizo lets say la kusalitiwa ata move kwa ile list yake namba mbili hivyo hivyo mpaka apate faraja.

KWA MWANAUME
-Mwanaume hujutia, huweka mambo moyoni, hujikaza na kujishusha thamani ya uanaume wake. Hili ni tatizo kwani huwezi sababu sumu yote hiyo moyoni ni lazima itakuangusha tuu. Hivyo kwangu mimi nakushauri fanya yafuatayo.

· Kwanza ikubali hali, kama umesalitiwa we kubaliana na hali jua sio jipya duniani. Yes umia, lia pia jua huwezi zuia tukio ambalo lishatokea hivyo kubaliana na hali halisi.

· Usishindane na mtu ambae unajua huwezi mshinda! Kutokana na jinsi mioyo ya wanaume ilivyoumbwa ni ngumu sana kushusha uanaume wao hivyo hii huwafanya hata kupigana au kuchukua maamuzi magumu kama kujiua, kuua na kuuana . Mimi nawaambie badilisheni mioyo yenu! Kubalini kushindwa. Hata mataifa makubwa duniani kabla hayajaamua kwenda kupigana huchunguza kwanza adui ana silaha gani hasa, je anaweza pigana nae? Kama hana silaha imara au atapoteza basi anatulia na kukubaliana na hali kwamba ni hatari hivyo bora akae kimya kuliko kupoteza. Mfano jifunzeni mgogoro wa Marekani na Korea ya kaskazini mnaweza jifunza kitu kikubwa sana kitakacho wasaidia maishani. Plz usipigane na mtu ambae unajua humuwezi au kakuzidi uwezo… utapoteza!

· Tafuta kitu cha kukufurahisha na kukupoteza mawazo, jua lililokukuta sio jipya hivyo move on mda unavyozidi kwenda kidonda kitapona, wazungu wanasema time heal!

· Ishi na watu kwa amani! Usimlaumu yoyote kuishi na aman na watu hata wabaya wako ni mtaji! Hii itakupunguzia maumivu zaidi na mitafaruku.

· Binadamu tuna wivu hata Mungu ana wivu. Yes kubaliana na hali… jipe mda ukifikiria kitu kingine bora zaidi. Mwanamke ni changamoto sana kwa mwanaume yeyote yule so lazima uumie, usiidanganye nafsi wapo wanawake wapo wengi noo… Hata kama wapo lazima uumie kwanza ndio uwe tayari kwa mwanamke mwingine bila hivyo huwezi furahia mapenzi sababu bado una uchungu moyoni. Huo uchungu ni sumu so ufute kwanza ndipo usonge mbele.

· Usimwamini mwanamke, wachukulie easy hata baya litakalotokea halitakuumiza kwa sababu hu tarajii ukamilifu wa mwanamke. Hata biblia inasema wanawake ni viumbe dhaifu! Hivyo basi expect nothing there sana sana wao ni vyombo vya starehe tuu na kulea wanao. Mwanaume piga kazi mjomba epuka kumtegemea mwanamke kwa asilimia 100% soma Mwanzo 3:6, Mwanzo 3:13, 1Petro3:7 Mungu kasema tumtawale mwanamke 3:17 yani kwa maana nyingine mwanamke anapaswa akusikilize wewe. Ukiwa mzembe kama adamu utaangamia, soma Mwanzo 3:12 Adamu angepaswa asikilize yale Mungu aliyomwambia na sio amsikilize mwanamke! Mwanzo 2:16-17 Adamu ndio chanzo cha matatizo yote hapa duniani, fikiria angetii yale ya Mungu ungekuta tunakufa? Hapana ungekuta mambo ni mazuri hapa duniani. So wale wanaume wanaoendeshwa na mwanamke mnakosea sana, Yes mnakosea sana na familia hizi huwa na migogoro kwa sababu msingi wa nyumba “Baba” hauko imara

· Fanyia kazi madhaifu yako, tafuta ukweli kile kitu kilichokua kinakusumbua moyoni kitatue next time utakua strong! Usikubali kitu kikae moyoni mwako kwani kitakutafuna milele! Kitafutie ufumbuzi ili ubaki na amani na utajiamini na kuwa na furaha maisha yako yote. Uzuri ukishakielewa kitu unakua unakiendesha wewe utakavyo yani kinakua chini yako hivyo ni wewe tuu unajimwaga… Mfano kuna maneno makali sana haya mwanamke akisha mtamkia mwanaume basi mwanaume hijihisi hudharaulika na kuathirika kisaikolojia au kujishusha thamani kabisa… hivyo wanaume fanyieni kazi hayo maneno ni magumu mno hata kuyaweka hapa ila mnayajua. Yani likitamkwa hapa unajihisi kama kitu kinauchoma moyo na maini… hahahaha hilo ni tatizo kubwa nawambieni myatatue mapema sana kwa afya ya nafsi zenu. Pia mwanamke akikusaliti au ukisikia kafanyiwa mambo mabaya aaaah mwanaume huumia sana especially ukute mwanaume aliemfanya kakuzidi ubora na shughuli… Hapo kwa wengi najua mna mioyo hafifu sana, hapo hutamani kufa kwani unahisi umeshushwa thamani na utadharaulika daima… Namna ya kutatua tatizo sio kujiua bali ni kukubali yes hapa nimepigiwa so mtafuta mnyonge wako uupoze moyo wako ila asiwe mke wa mtu kwa sababu huyo mwanaume mwenzio akijua naye ataumia, ni bora uoe kabisa kuliko ufanye uzinzi maana maandiko yanasema azinie na mwanamke hana akili kabisa. Na kama mwanamke kakusaliti makusudi mwache kama huwezi kuikubali hali hata Mungu kasema muwaache wake zenu kwa uzinzi… anajua sisi wanaume (Viumbe vyake) tuna mioyo migumu mno kamwe hatuwezi samehe labda tunaweza kusahau, Soma Mathayo 19:8-9 . Kama unaona aliekula tunda lako hafikii level yako naamini unaweza kuendelea na mkeo kwa amani… Kwa upande wa wanawake wao wanaweza samehe na mambo yakasonga smoothly kwa sababu wao wana mioyo mepesi ila na wao wanaumia pia so isiwe sababu ya nyie kuwaumiza wake zenu! Hiyo ni dhambi, kama hakutoshi oa mwingine.



· Trust is dangerous game! USIMWAMINI MWANAMKE HATA AKUPENDE VIPI. KUMUAMINI MTU NI KUMPA UHAI WAKO! KWANINI USIMPE MUNGU UHAI WAKO UNAMKABIDHI MWANADAMU AMBAE MUDA WAKE WA KUISHI NI MCHACHE HAPA DUNIANI? PLZ KWA AFYA YA MWILI NA ROHO YAKO USIMPE MTU YEYOTE MOYO WAKO HATA AWE NANI! ANAEPESWA KUAMINIWA NI MUNGU TUU NA SII YEYOTE YULE. WANAUME HATA WANAWAKE WENGI WALIOJIUA WALIWAKABIDHI MIOYO YAO WAPENZI WAO HIVYO USALITI ULIPOTOKEA HAWAKUWEZA KUHIMILI MAUMIVU HALI ILIYOWAFANYA KUUA, KUUANA AU KUJIUA WENYEWE! MIFANO MNAYO… YES EXPECT NOTHING AND YOU WILL NEVER BE HURTED! MOYO WAKO USIMPE YEYOTE YULE KWA USALAMA WAKO, HAPA DUNIA HAKUNA MWENYE SIFA YA KUPEWA MOYO. MUNGU WAKO NDIO UNAEPASWA KUMKABIDHI MAISHA YAKO. MOYO WAKO NI UHAI WAKO… SO USICHEZE NA UHAI KWANI UTAKUFA MARA MOJA.

· Never limit your self, usijibane sana kuwa na uwanja mkubwa wa machaguo ya wapendwa wako! Likitokea la kutokea una move kwa chaguo la pili hadi mwisho. Ishini kama wanawake wanavyoishi nawaambia na hamtakaa muumie kiivo maishani na mtakua na maisha marefu. Kama umechunguza familia nyingi toka babu na hata wazazi wako ni nani anaetangulia kufa? Hata kama walikua na umri sawa? Kwa nini asimia kubwa iwe huyo mtu? Jibu utalitafuta mwenyewe nisikupe kila kitu kwani utashindwa kujisaidia ukiwa mwenyewe.

Ukimtegemea mtu mmoja itakula kwako. Kwa wale watu wa Mungu najua nyinyi ni waaminifu hivyo basi hamna tatizo likitokea la kutokea bado hamjapoteza GOD is there viumbe vyote kaumba yeye atakupa kingine. Uzuri unapomkabidhi maisha yako Mungu wako hutakaa utaabike kamwe. IMANI NI MSINGI WA MAISHA, MUNGU WETU ANATUPENDA MNO NA ANAJUA MAHITAJI YETU. HIVYO KWA MTU WA MUNGU RELAX NAKWAMBIA MAMBO MAZURI YANAKUJA BAADA YA MATAABIKO, YES MUNGU ANAPENDA WATU WAVUMILIVU!



NB: BAADA YA KUFANYA YOTE HAPO TAFUTA KITU CHA KUKULIWAZA ASIWE MWANAMKE LAKINI KWA SABABU UTAKUA BADO NA UCHUNGU HIVYO MAPENZI HAYATA NOGA VILIVYO, UTAFURAHIA UKIWA UME RELAX KIMWILI NA KIAKILI. HIKO KITU KINAWEZA KUWA BIBLIA, MUVI, KITABU KIZURI, MUZIKI MZURI WA KUKUFURAHISHA NA KUKUCHANGAMSHA AU KUKUMBUSHA JAMBO FULANI ZURI WAKATI WA NYUMA! PLZ USIWE MZIKI WA MAJONZI AU KUKUMBUSHIA MATUKIO MLIOKUA PAMOJA, KULA CHAKULA KIZURI, JOGGING, MAZOEZI KIASI YA KUKUCHANGAMSHA, VICHEKESHO, MARAFIKI N.K

KIPINDI HIKI KIGUMU HUPASWI KUWA MWENYEWE WALA KUUGULIA MOYONI. VUMILIA IKUBALI HALI TAFUTA KITU CHA KUKUWEKA BIZE. AVOID LONELINESS PLZ! UPWEKE/DEPRESSION INAUA!


BAADA YYA HAPO NAWASHAURI NDUGU ZANGU MUSOME SANA SAIKOLOJIA!

KWANGU MIMI SAIKOLOJIA NI DAWA, Ni dawa kwa sababu inanisaidia kutatua matatizo mbalimbali maishani na hivyo nafsi yangu huwa huru muda wote.

Sio kwa wanaume tuu bali hata wanawake nawashauri musome sana saikolojia kwani itawasaidia maisha yenu yote.

Ukisoma saikolojia utaelewa tabia, miendendo, mfumo wa akili ya watu na vitu mbalimbali kutokana na mazingira ya kitu/mtu mwenyewe hivyo vitakua chini hayo!

Kwa kizungu Pychology is the scientific study of behaviour and mental process in a given context!

Lengo la saikolojia ni kukifahamu kitu kwa kina, hivyo mtu akikifahamu ataweza kukitafiti na kukielezea, kubashiri na kuki control hiko kitu kwa maana anakielewa nje ndani na baada ya yote hapo step ya mwisho ni kuboresha ubora wa maisha ya mwanadamu! Basi hilo ndilo lengo la saikolojia/Pschology.

Hakuna kitakacho kuendesha basi wewe utakiendesha. Wanaume wengi pamoja na mimi laiti tungeelewa kiundani wanawake basi haya matatizo yanayotukumba tungesha yatatua na furaha ingetawala daima. Maandiko yanasema “ishini na wake zenu kwa akili’ mkiufata huo mstari vizuri nawaambieni maisha yenu yatakua na furaha na mtaishi kwa amani.

MUNGU AWE NANYI NDUGU, SHARE NA MWENZIO TULIOKOE JAHAZI LISIZAME.
 
Kitu kimoja nilichojifunza kuhusu wanawake,ukiwa na mwanamke mmoja tu tena na yeye akajua unaye yeye tu...atakusumbua sana na hii sio kosa lao wanajikuta tu wanajisikia kukusumbua kichwa...na cha pili kwanini wanawake wanalalamika wanaume maskini wakipata hela wana badilika..jibu ni moja tu tunasimangwa sana na tunavumilia huku tuki focus kwenye malengo yetu..sasa pesa ikija ndo hapo tunaona haina haja tena ya kuvumilia makero ya zamani...nipo hapa sio kwenye umaskini ila nina ndoto kubwa sn sasa huyu mwanamke niliye nae analeta gubu za kijinga na kuni block kwa mawazo yake mgando nisifanikiwe...nkifanikiwa huyu atashuhudia dharau ambayo hajawahi kuiona toka kanifahamu...namchora tu mi naimba halelluyah ya diamond..yeye anaimba dume suruali ya Mwana fa...na share vision zangu yee anawaza kunipa plan za kutumia hela kijinga
 
Hata sisi HATUWAAMINI wanaume kabisaaa hata kama mtaonyesha kutupenda sana.
 
Kitu kimoja nilichojifunza kuhusu wanawake,ukiwa na mwanamke mmoja tu tena na yeye akajua unaye yeye tu...atakusumbua sana na hii sio kosa lao wanajikuta tu wanajisikia kukusumbua kichwa...na cha pili kwanini wanawake wanalalamika wanaume maskini wakipata hela wana badilika..jibu ni moja tu tunasimangwa sana na tunavumilia huku tuki focus kwenye malengo yetu..sasa pesa ikija ndo hapo tunaona haina haja tena ya kuvumilia makero ya zamani...nipo hapa sio kwenye umaskini ila nina ndoto kubwa sn sasa huyu mwanamke niliye nae analeta gubu za kijinga na kuni block kwa mawazo yake mgando nisifanikiwe...nkifanikiwa huyu atashuhudia dharau ambayo hajawahi kuiona toka kanifahamu...namchora tu mi naimba halelluyah ya diamond..yeye anaimba dume suruali ya Mwana fa...na share vision zangu yee anawaza kunipa plan za kutumia hela kijinga
mvutie upepo mkuu maake hata mm yupo tu nimemueka kipolo ila naina siku yake bado
 

Attachments

  • 949AABA7-C419-4424-83E8-4139D545205A.jpeg
    949AABA7-C419-4424-83E8-4139D545205A.jpeg
    209.3 KB · Views: 40
Mtoa Post Nilichoona umeandika sana ila kila Point unayoandika haina Mashiko
 
Umesoma thread Yote lakini?
Nimesoma mr Zombi. Kuna sehemu amesisitiza kuwa wanaume wasituamani hata kama tunaonyesha upendo wa hali ya juu. It means hamtuamini na sisi ndivyo hivyo hivyo
 
Nimesoma mr Zombi. Kuna sehemu amesisitiza kuwa wanaume wasituamani hata kama tunaonyesha upendo wa hali ya juu. It means hamtuamini na sisi ndivyo hivyo hivyo
MI namuamini mwanamke nikiwa Sina hela tu.
 
Kwaiyo umeandika yote hayo lengo ni kukabiliana na mwanamke..yaani umekosa 'theme' nyingine zaidi ya mwanamke??empty set kabisa
Ila wewe mkaka mbona una dharau sana? Yani haijawahi kutokea mtu humu akawa na full set kila siku ni watu wakianadika thread kwako ni empty set tuu
 
mwanamke ndio amekusukuma kuandika yote haya.......wanawake tuliumbiwa wanaume....kuwa mpole,,,,msome,,,akikusaliti jua amekuepusha na mengi......maisha yanapinda pinda broo....
 
Kitu kimoja nilichojifunza kuhusu wanawake,ukiwa na mwanamke mmoja tu tena na yeye akajua unaye yeye tu...atakusumbua sana na hii sio kosa lao wanajikuta tu wanajisikia kukusumbua kichwa...na cha pili kwanini wanawake wanalalamika wanaume maskini wakipata hela wana badilika..jibu ni moja tu tunasimangwa sana na tunavumilia huku tuki focus kwenye malengo yetu..sasa pesa ikija ndo hapo tunaona haina haja tena ya kuvumilia makero ya zamani...nipo hapa sio kwenye umaskini ila nina ndoto kubwa sn sasa huyu mwanamke niliye nae analeta gubu za kijinga na kuni block kwa mawazo yake mgando nisifanikiwe...nkifanikiwa huyu atashuhudia dharau ambayo hajawahi kuiona toka kanifahamu...namchora tu mi naimba halelluyah ya diamond..yeye anaimba dume suruali ya Mwana fa...na share vision zangu yee anawaza kunipa plan za kutumia hela kijinga
Hapo mi naona shida sio kua na mwanamke mmoja tu, shida kubwa sana ni pale mwanamke anapojua kua kwake umekufa na umeoza kabisa, hakyanani atakuchezesha singeli mpk utajuta kuzaliwa.
Chausiku MUNGU anakuona ujue jinsi unavyonifanyia mtoto wa mwanamke mwenzio, na tokea ulivyojua vyuma vimekaza kwenye mishe zangu ndio unazidi kuninyanyasa.
Walahi we endelea tu kuunyanyasa mtima wng maana ni kiherehere cha moyo wangu mwenyewe kuacha kazi yake ya msingi ya kusukuma damu.
Ila wakati mwingine hua nnahisi kuna kitu umenifanyia wewe sio bure, maana sio kwa ukondoo huu nlionao sasa hivi.
 
Back
Top Bottom