Mwanaume mpumbavu ni yule anaye mfukuza binti yake kisa kapata ujauzito au kumlazimisha binti yake aolewe na jamaa aliyempa ujauzito

Mwanaume mpumbavu ni yule anaye mfukuza binti yake kisa kapata ujauzito au kumlazimisha binti yake aolewe na jamaa aliyempa ujauzito

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
11,250
Reaction score
24,084
Bwana ni mwema wakati wote.

Wewe mwanaume mpumbavu unayemfukuza nyumbani binti yako kwa sababu kapata ujauzito akiwa nyumbani nakukumbusha tu kuwa DUNIA HAINA HURUMA.

Iwapo wewe mzazi umeamua kumtimua na kumbwaga aende mtaani kumbuka huko ndo ataharibikiwa zaidi na hakika machozi yake hayataenda bure!!

Iwapo huyo aliye mpa huo ujauzito hataki kumuoa kwanini ulazimishe amuoe?
hadi unafikia hatua ya kumfukuza je umekaa naye chini mara ngapi ukimuonya kuhusu madhara ya mimba za utotoni au hta kupigwa mimba akiwa nyumbani bado?

Sikia mwanaume na ukumbuke kuwa mtoto ni mtoto tu huwezi ijua kesho yake kupata mimba siyo sababu ya kumtimua nyumbani!

Nikuulize kati ya kutoa mimba na kuzaa ipi dhambi na laana kwenye familia yako?
Kwa dunia ya sasa inabidi tu tuwe wapole maana hiki kizazi kinajua mambo ya wakubwa kuliko hata wakubwa wenyewe!!

Wewe pale unapodhani labda binti yangu bado hajamjua mwanaume kumbe kaanza muda ambao hata wewe hukuwahi fikilia!!

Njia sahihi ya kumuonya pale anapopata mimba akiwa kwako kaa naye tena kwa upendo mkubwa sana muonye kwa hekima na upole hadi ajutie baada ya hapo onyesha mapenzi ya upendo kwakwe.

Mshawishi amuite jamaa aliyempiga mimba kaa naye sikiliza malengo yake na mwonekano wa yule kijana
muulize kazi yake inayomuingizia kipato kisha fanya maamzi ya busara kulingana na mazungumzo hayo.

Nipo hapa na kukuhakikishia huyo binti hatakuja kupata mimba tena akiwa nyumbani kwako lakini ukimtelekeza duniani asee hapo utakuwa umepoteza kwa 80% na atapa mimba zingine na watoto utaletewa nyumbani hapohapo ukumbuke akipata maradhi atakuja hapohapo kwako na hutakuwa na cha kumfanya lakini angekuwa nyumbani asingepata hayo.

Kuwa mbabe sana haitakusaidia kwa lolote kuna tofauti kubwa mno kati ya kuheshimiwa na kuogopwa!!
unaweza ukaogopwa ila huheshimiwi asilani! Lakini kama anakuheshimu hakika atakuheshimisha pia!

Ukiogopwa kumbuka kila nafasi atakayo ipata ataitumia kwa 100% kwa ufanisi na uhakika haijarishi yupo siku za hatari au lah.

Mwaka 2019 nilikuwa nasimamia ofisi fln kama Agent wa sigara,vocha na mpesa (float) nikiwa kazini muda kama saa7 alikuja binti na begi la mgongoni jeusi akanisalimia kisha akakaa kwenye bench la wateja maana nilikuwa na wateja wengi baada ya muda aliniomba hela ya kula ana njaa sana vile nilikuwa na jamu mingi ya wateja basi nilimpa kama buku2 tu akaenda kula.

Nikijua ndo ameenda mazima lakini baada ya muda akarudi kushukuru huku akasimama dirishani kwa muda kidogo maana sikuwa na wateja kivile nikamuuliza dada vipi mbona huna raha un aumwa?

Mara akaanza kulia kwa asili mimi mwanamke siwezi msikiliza akiwa analia awe anaigiza au iwe kweli huwa si sikilizi.Basi nikamwambia mwenzangu tuliyekuwa tunafanya nae kazi pale akaenda kukaa naye huku anamsikiliza

Alimsikiliza wee kisha akarudi na akaanza kuniambia alivyoambiwa japo binti yupo pale bado.
Nikamuita na nikamwambia kama ataweza kuniambia pasipo kutoa machozi basi aongee.........

Nilimsikiliza kwa umakini sana pale japo mimba ilikuwa si kubwa sana kimuonekano.Aliniambia story ndefu sana. lakini nitaifupisha sana.

Binti yule alikuwa na mahusiano na kijana wa lika lake uko kwao kijiji X Basi wakanogewa mara mimba hiyo huyu jamaa muda huo alikuwa hana maisha yoyote yale hivyo akamwambia wazi sikatai mimba ila kuhusu kukuoa sitaweza kwa sasa na kijana kuepusha lile akatoroka na kubadirisha laini za simu!

Baada ya familia kujua ikamuuliza mwenye mimba ni nani ? akamtaja asee alipigwa na kaka zake na akapigwa tena na mzee wake. Na kisha kuambiwa mfuate hukohuko aliko hatutaki tukuone hapa. Kumbuka hana nauli wala hela yoyote ile aliiba nguo za mama yake k vitenge3 sijui ndo pair mnaita lakini alisema hivyo na akaenda kuuza kwa washona cherehani kwa bei ya bure akapata kama 35k kwa maelezo yake.

Basi akaja mji X kwa lengo la kutafuta kazi nauli ya kutoka kijijini hadi mjini kwa boda ni 5000 baada ya hapo tena upande basi kuja huku alikonikuta mimi ni 6000 alifika akaenda gest ya ten akala na akalala baada ya siku2 hela akaishiwa ukumbuke ndo anatafuta kazi akiwaambia ana mimba wana mkataa hasa wa mama wa hoteli ndo alikuwa anaenda zaidi.

Baada ya kuchoka sana ndo akaja kwangu kuomba hela ya kula wala sikumuuliza nikampa buku2.

Muda ukawa unayoyoma sana mi kwenda bank maana tyr ilikuwa saa9 na ushee hivi nikamwambia mdogo wangu nimekusikia lakini msaada wangu kwa sasa nitakupa hela ya kula na pakulala hadi kesho tena na ukalale sehemu nzuri angalau basi nilimwambia akale tena chakula chochote anachojisikia kula akasema hela hiyo nimpe itamsaidia hata kesho maana kama kula amekula na ameshiba.

Nikamwambia nenda kale kuhusu hela nitakupa tu.Basi nikafungasha pesa nikaenda bank yeye akaenda akala hadi narudi basi nikamkuta naye kamaliza kula.

Tuliweka sawa ofisi tukafunga maana tulikuwa tunafunga saa10:30 au zaidi. Baada hapo sasa nikabeba begi lake tukaanza kutembea nae walikuwa wakiniuliza nani yako huyu nawaambia dada yangu .Moja kwa moja nikamfikisha lodge moja ya kati nikalipia kisha nikamuachia hela kiasi(40k)

Nilipofika geto kwangu wakaja na wafanyakazi wenzangu wa ile ofisi maana tulikuwa wa3 tulipiga story tukaenda kula kwa mama ambae alikuwa mteja wetu wa nguvu sana mama mchangamfu sana.

Baada ya kula nilimuomba mama yule nizungumze nae na nikamuomba sana ampe kazi yule binti afanye kazi bure pale kwa mwezi mmoja nitakuwa namlipa mimi na geto nitampangishia mimi. Yule mama akaniuliza ni mtu wako au vipi ikabidi nimwambie ukweli A-Z yule mama alikubali akasema pia kwake kuna chumba atamuhifadhi iwapo atakuwa na tabia njema basi ataishi hapo bila shaka yoyote kwa shart moja tu abadili dini na awe mkatoliki.

Mimi nilikuwa sijajua binti yule anaabudu dhehebu gani. Basi tulitoka pale na washikaji japo wao hawakujua nilikuwa naongea nini na yule mother.Moja kwa moja nilienda kwa binti yule lodge usiku ule nikamkuta amelala ilikuwa saa3 au 4 hivi nikagonga kisha nikamwambia nimekutafutia kazi ambayo utakuwa unalippwa buku3 kwa siku kulala na kula bure.Yule binti alifurahi sana kisha nikamwambia kesho aamke asbh sana nimpeleke pale kabla mimi sijaenda job.

Ikumbukwe mama yule aliniambaia ni mfuate usiku uleule nikakataa nikamwambia acha tu alale nimeshalipia tyr.Asubh ile yule binti nilimfuata na kweli alikuwa kajiandaa na baada ya kumkabidhi kwa mama yule alinipa zile pesa zote 40k nikamwambia hapana kaa nayo utanunua mahitaji yako madogo madogo kama mashuka na dawa za meno nk.

Basi siku moja nilimpigia simu baba yake maana mama yake hakuwa na simu nikaongea nae yule mzee nikamwambia binti yako ninae mimi.....SIJAPATA KUONA MZEE MNGESE ,MPUMBAVU NA FALA KAMA YULE ...ALINITUKANA VIBAYA MNO AKISEMA MIMI NDO NILIHARIBU NDOTO ZA BINTI YAKE ZA KUOLEWA NA WANAUME WENYE HELA (MALI)

Nilimsikiliza hadi akamaliza kisha nikamuomba mzee nisikilize akaniuliza unasemaje? kiasili mimi huwa nakigugumizi hivyo kulingana na hasila nilizokuwa nazo nilishindwa kuongea nikakata simu kwanza nikanywa maji ndo nikapiga tena muda huo yule binti analia anasema nimeku-sababishia haya yote.

Yule mzee bana akanisikiliza wee kisha akasema sawa nimekusikia unasemaje sasa? nikamwambia naomba niongee na mama pia basi yule mama nikamwambia alivyonifikia yule binti na namna nilivyo mpokea hapo ni miezi 2 imepita mimba inaenda miezi6 ishakuwa kubwa tu na hotelin haji amekuwa kama mtoto wa ple tu kwa yule maza.

Mama akasema angekuwa na nauli angekuja kuonana na binti yake nikamwambia tafuta namba nyingine yenye mpesa nitakutumia siku yoyote.Kweli alipata na nikamwambia aje jpli maana mimi huwa sifungui ofisi na alikuja kweli tukaongea mama yule alifurahi sana kumuona binti yule.

Muda wakujifungua ukafka yule mama akaniambia tusaidiane mahitaji ya kujifungulia kumbuka hata clinic niliwahi mpeleka mimi kama mme wake ili asisumbuke tukapima ngoma kisha tukarudi.

Tulinunua vitenge gloves nk hakika tulitimiza vyote vinavyohitajika tukasubiri siku ya kujifungua ya yule binti.
Mwezi haukupita akajifungua mtoto wa kike!! Alikuja tena mama yake akakaa kama wiki na ushee akarudi

Mama yule akamfungulia ofisi ya mpesa hapohapo nyumbani kwakwe kulikuwa na flemu hivo nikawa msaada tena wakati akiishiwa float mimi nikawa namuwekea tu jioni nafata hela zangu maana haikuwa mbali...ofisi ile ya mama ikakua kuwazidi pale mtaani maana hakuna mtu alikuwa akija anakoswa chash au salio.

Nilikuwa nawapa hadi m5 kulingana na uhitaji....Mungu huyu huyu yule binti akaolewa na kutolewa mahali na mtoto wa mfanyabiashara mkubwa hapo mtaani.


Hiki kisa nilikuwa nimeshasahau kabisa Leo nimepigiwa simu kama mara7 na no ngeni bahati mbaya nilikuwa nimelala nimekuja kufuatilia ile no ndo yule dada baada ya kupotezana kuanzia 2021 hadi leo... Tumeongea na akanitumia kiasi flani cha pesa yeye anasimamia duka la spea za pkpk kwa sasa mme wake naye ana maduka mawili ya jumla ya takataka.
 
MWANAUME MPUMBAVU ZAIDI NI YULE ANAYEWEZA KUKAA NA MKE WA MTU NA KUMHUDUMIA KAMA MWANAE WAKATI AKIJUA NI MJAMZITO!

KITENDO CHA KUPEWA UJAUZITO HUYO NI MKE WA MTU HAPASWI KUKAA KWAKO,INAPASWA AENDE KWA MUMEWE ALIYEMPA UJAUZITO
 
MWANAUME MPUMBAVU ZAIDI NI YULE ANAYEWEZA KUKAA NA MKE WA MTU NA KUMHUDUMIA KAMA MWANAE WAKATI AKIJUA NI MJAMZITO?

KITENDO CHA KUPEWA UJAUZITO HUYO NI MKE WA MTU HAPASWI KUKAA KWAKO,INAPASWA AENDE KWA MUMEWE ALIYEMPA UJAUZITO
Umeandika kama mtu aliyekatwa kichwa mkuu jipe muda utafakari nilicho Andika basi au kama umefikia kabisa kikomo Cha kufikiri basi muulize mkeo atakufafanulia
 
MWANAUME MPUMBAVU ZAIDI NI YULE ANAYEWEZA KUKAA NA MKE WA MTU NA KUMHUDUMIA KAMA MWANAE WAKATI AKIJUA NI MJAMZITO?

KITENDO CHA KUPEWA UJAUZITO HUYO NI MKE WA MTU HAPASWI KUKAA KWAKO,INAPASWA AENDE KWA MUMEWE ALIYEMPA UJAUZITO
 
Mimi sitatia neno kwa sababu na mimi nimezaa,ila usiombe hii mitihani ikukute.

Kuna baadhi ya mambo yanahitaji kuwa na kiasi kuyazungumza nayo ni kama hili la watoto kupata mimba hali wadogo au hawajaolewa.
Mkuu hatuombi kamwe yatokee lakini kama Kwa wenzio yanatokea elewa hata kwako inawezekana sana ikatokea. Jenga urafiki na wanao wa kike hasa waambie bila kificho na sio Kwa u babe kama wanakushemu lazima wakuheshimishe lakini kama wanakuogopa tegemea lolote.

Mwanao ukimtupa duniani ujiulize anaenda Kwa nani kama jamaa hataki kumuoa?

Fikiria kama Mimi ningeomba nimsadie Kwa lengo la kunipa ngono muda ule angekataa vipi? Fikiria nimeenda lodge saa4 na akafungua nikaingia tukazungumza ningetaka angeninyima? Fikiria Kwa mara nyingine kama ningekuwa na HIV si mtoto wako angeambukizwa ndani ya siku3 -5 tangu atoke kwako?

Hapa mkuu pamoja na Kwamba inaumiza mno lazima uonyeshe uanaume wako na busara zako ukitumua muhemko utapoteza hakika.
 
Nakumbuka mzee wangu mkubwa, yeye alikuwa anasema hawezi kulea mama na mtoto na yoyote akipata mimba kwake ataondoka.

Sista akapata mimba, alimsepesha
Sikatai mkuu Kila mwanaume Huwa anajua namna ya kuendesha familia yake. Lakini usipotumia hekima huyo mtoto atahribikiwa mno na hata akiugua basi atarudi nyumbani na utamtibia tu au akizalishwa Tena mtoto atamleta na utampokea.
 
Wazazi wengi hatuzungumzi na watoto kuhusu maisha wakiwa tangu wadogo na pengine hatuonyeshi matendo mema mbele yao.Lakini kuwafukuza wakipata mimba nyumbani ni worst option. Yatupasa kuzuia mlango aliopitia ili wadogo zake wasijepata kadhia hii
100%✓✓
 
Back
Top Bottom