Mimi ninayofahamu Surname ni jina la ukoo ambalo hata katika nchi za matrilineal majina ya ukoo bado yanabaki kuwa ya wanaume. Kwa hivyo hata mwanamume atapobadili jina la ukoo la mkewake, hii haina maana kuwa ataitwa jina la kike bali jina la kiume la upande wa mkewake. Mfano, badala ya Michael Suzana, ataitwa Michael Peter ikiwa surname ya kewake ni Peter.
Nimewahi kuona mifano kutoka nchi za Latin Amerika na Spain ambako mtoto anakuwa na surname mbili, moja kutoka kwa mama na nyengine kutoka kwa baba. Kwa hiyo kama utakuta mtu anaitwa kwa mfano Maria Carmona Castellano basi surname ya kwanza ni ya baba na ya pili ya mama. Mpangilio wa surname ipi ije mwanzo ni uamuzi wako.