stata mzuka
JF-Expert Member
- Nov 25, 2012
- 4,834
- 1,765
Habari zenu wakuu!
Huwa kuna jambo linanichanganya kweli!unakuta kijana wa kiume amemaliza chuo kikuu,anafanya kazi kwa miaka kama mitatu hivi ila cha kushangaza bado anakaa kwa wazazi!kibaya zaidi wengine unakuta wanakaa kwa ndugu very comfortable!
Kinachonikera hawa vijana ndo wa kwanza kujishaua mjini hapa kwenye starehe!
Anyway labda mimi najudge vibaya ila wenzangu kijana kama huyu mnamchukulia kama mwanaume au mvulana?!
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Mkuu inaelekea Wazazi wako walichelewa kuja mjini au katika familia we ndo mkubwa pekee ambaye baada ya kuchaguliwa chuo mjini ndo ukabahatika kuishi mjini.
Au labda Baba ako alicheza Golori na Mama Mdako wakajisahau wenzio walivyokuwa wanatafuta Pesa.
Turudi kwenye Topic mi binafsi Mzee wangu M/Mungu kamjaalia nyumba kama 4 hapa mjini,,wakati nilipomaliza masomo na kutaka kuanza maisha amenipa nyumba moja ambayo nakaa hadi sasa hivi na sharti alilonipa ni mpaka nihamie kwangu kwani haoni sababu ya Mimi kwenda kupanga ubavu 180,000 wakati nyumba zipo na ukizingatia Mimi ndio mtoto wa kiume peke yangu na dada zangu watatu wapo kwao.
Hela ya kujenga naifanyia mambo mengine binafsi,,nakushangaa ukisema mzee akifa tunategemea mali sasa hizo Mali azitegemee nani kama sio mtoto wake au unataka tuziache?
Mkuu inaelekea wewe ulishaambiwa Soma sana kwani Urithi wako ni Elimu Wazazi hawana kitu,,,Walaumu wazee wako wakati wa kutafuta hela wenyewe wanachunga Ng'ombe.