Mwanaume kukaa kwa dadako ....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume kukaa kwa dadako ....!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Safety last, Aug 18, 2011.

1. Safety last

Safety last JF-Expert Member

#1
Aug 18, 2011
Joined: Mar 24, 2011
Messages: 4,224
Likes Received: 164
Trophy Points: 160
Katika harakati za kujipanga na kujiandaandaa,mwanaume kukaa kwa dadako aliyeolewa, wengi hawapendi na jamii inamchukulia kama "he is not man enough"yuko tayari kuishi hata kwa rafiki kuliko kwa dada yake, kwanini huu mtizamo upo??

2. Lizzy

Lizzy JF-Expert Member

#2
Aug 18, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 22,224
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Nani kakudanganya?!

Labda kama umri wake umevuka 25-27 umri ambao anatakiwa awe na kazi.Ila chini ya hapo sio vibaya kwasababu wengi wanakua wanasoma kwahiyo badala ya kupanga wakati hana mshahara anakaa kwa dada vile yuko karibu.

3. Karnoon

Karnoon Senior Member

#3
Aug 18, 2011
Joined: Jul 9, 2011
Messages: 106
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Dah!ni kama mmeolewa wote hv?

4. arabianfalcon

arabianfalcon JF-Expert Member

#4
Aug 18, 2011
Joined: Oct 19, 2010
Messages: 2,292
Likes Received: 9
Trophy Points: 135
Dada umeolewa na wewe mtoto wakiume ushafikia umri wakujishughulisha unajipweteka kwa shemeji inaonyesha kama mmeolewa nyote,,

5. Safety last

Safety last JF-Expert Member

#5
Aug 18, 2011
Joined: Mar 24, 2011
Messages: 4,224
Likes Received: 164
Trophy Points: 160

sijadanganyika mpendwa ni mambo nimeyashuhudia hata kwa hao unaosema ni wanachuo wengi hawako huru, ni kama huyo mmeo kawaoa wote.

6. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#6
Aug 18, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,506
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
huwezi kuwa huru kwa watu! kama una sababu ya msingi ya kukaa kwa dadako na shemeji yako hakuna tatizo. ila shida ni kujibweteka. tafuta kazi kwa bidii na uwaoneshe kuwa ww sio mzigo. wapo vijana wanakaa kwa dada zao wakipata kazi na kuondoka hata shemeji yao anasikitika kwa jinsi ambavyo watammisi. ila kama kijana ni mtu wa kusalandia hgeli, hajitumi kusaidia issue ndogo ndogo walau kupeleka magari ya watu gereji na kusimamia mafundi, au kama sio muaminifu, siku akiaga kila mtu anashusha pumzi. ugali wa shkamoo shurti uutumikie atii!

7. BlackBerry

BlackBerry JF-Expert Member

#7
Aug 19, 2011
Joined: Mar 22, 2011
Messages: 1,844
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
Hili nalo neno, sio unakaa kwa watu remote zote umeshikilia wewe, watoto wao wanataka cartoon network wewe ss3, kwako???

8. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#8
Aug 19, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
Hamna kitu nachukia kama kukaa kwa watu, nashukuru nimezoea kujitegemea toka nasoma. Wengi wanapenda mteremko, na ndiyo maana ukipata kazi mkoa wa mbali na ulipo, utaulizwa "una ndugu huko?", ndugu for what?

9. Engager

Engager JF-Expert Member

#9
Aug 19, 2011
Joined: Jan 12, 2011
Messages: 329
Likes Received: 10
Trophy Points: 35

what about the 27+, ruksa??

10. Rutashubanyuma

Rutashubanyuma JF-Expert Member

#10
Aug 19, 2011
Joined: Sep 24, 2010
Messages: 157,528
Likes Received: 414,921
Trophy Points: 280
mashemeji ndiyo huzima taa........kwa kuchongea ndiyo wenyewe...................yupo mdada mmoja alilalamikiwa na mtoto wake wa kike ya kuwa baba mdogo alikuwa anamshikashika nyeti zake yule mama alilia sana lakini akaogopa kumtonya mumewe kwa kuhofia kugeuziwa kibao...................kuwa anamchukia shemejiye na kuwa anamjengea mazingira ya kumtimua mdogo wa mumewe.............................watu wajenge mazingira ya kujitegemea tu hakuna suluhishi hapo...........

11. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#11
Aug 19, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
hapo umenena, hakuna kitu kibaya kama utegemezi kwani uhuru haupo na unakaa ukiishi kimachale.

12. A

Aine JF-Expert Member

#12
Aug 19, 2011
Joined: Nov 1, 2010
Messages: 1,613
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
Mimi nafikiri hapa tuzungumzie pande zote mbili, yaani mwanamke/mwanaume kukaa kwa dada/kaka yake aliyeolewa/oa, ukifanya utafiti utagundua ndoa za aina hii mara nyingi ugomvi hauishi, mashtaka kibao kila siku. Ila mtu akae kwa kaka/dada yake kwa malengo jamani, mfano mtu ana miaka 27.... yupo tuu kwa dada/kaka anakula anaamka, na mkienda kazini yeye ndiye ana-control almost kila kitu hapo kwenu hadi watoto wanajenga chuki dhidi yake. Mtu akikaa kwa malengo kama shule kutafuta kazi mimi sioni kama ni tatizo lakini kukaa tuu yaani kkb (kula, kulala, bure) hapo hata akili ya kujitafutia haitakuwepo coz kila kitu anapata bure anashtuka ana miaka 33 au 35!!

13. K

Kakalende JF-Expert Member

#13
Aug 19, 2011
Joined: Dec 1, 2006
Messages: 3,259
Likes Received: 33
Trophy Points: 135
Sasa haya ni mausi ya rejereja, kwa taarifa yako, wengi wetu humu jamvini tumesoma kwa njia hiyo na kauli kama hizi zinatukera sana, hasa yule jamaa 'Mkandamizaji' wa Ze komedi hupenda kurudiarudia haya maneneo.

14. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#14
Aug 19, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

hili swala ni gumu sana je kwa wale wanaosomeshwa nao wameolewa au ni wale kamaliza kusoma halafu bado king'ang'anizi..

15. d

dkalu Member

#15
Aug 19, 2011
Joined: Aug 12, 2011
Messages: 42
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Kwani kaolewa dada au kaka?

16. Edson

Edson JF-Expert Member

#16
Aug 19, 2011
Joined: Mar 7, 2009
Messages: 9,200
Likes Received: 714
Trophy Points: 280
mimi nilikataa hii kitu toka zamani sana ,,,,maana toka asubuhi wewe ni mtu wa kushukuru tu..karibu chai..karibu chakula....karbu maji ya kuoga...washa tu tv.....na vyote unasema asante........hayo sio maisha......

Loading...