Mwanaume kujiuza!, ah! Haa!haaah!

NITIKE NDOSI

Senior Member
Jan 15, 2013
153
86


Na Mwandishi Wetu

AMA kweli dunia imekwisha! Kila kukicha Wabongo wanabuni mbinu mpya ya kujipatia mkate wa siku bila kujali kama ni halali au haramu ambapo baada ya kusikia habari za wanawake kufanya biashara haramu ya kuuza miili au ukahaba kwa muda mrefu, sasa wanaume nao wameingia kwenye mkondo huo, Amani lina ripoti kamili.
Uchunguzi wa muda mrefu wa gazeti hili ulibaini kuwa katika klabu, kasino na sehemu nyingi za starehe jijini Dar es Salaam, kuna idadi kubwa ya wanaume wanaojiuza kwa mijimama ya mjini yenye ‘mihela’ yao.
ISHU NI KUWA NA MWILI WA MAZOEZI
Uchunguzi wetu ulibaini kuwa vijana wanaojihusisha na biashara hiyo ni wale walio fiti kwa mazoezi ya ‘gym’ au wababeba vitu vizito wanaosifika kwa kutunisha vifua.
YAJIPANGA KLABU
Katika utafiti huo, midume hiyo ilibambwa laivu ikiwa imejipanga kwenye kasino maarufu iliyopo maeneo ya ‘ushuani’ Upanga Mashariki, Dar es Salaam wakisubiri wateja.
Mwanzoni shuhuda wetu alidhani ni mabaunsa wa kasino hiyo, lakini alitolewa matongotongo na mmoja wa askari aliyekuwa na bunduki aliyevalia sare ambaye alimtonya kuwa vijana hao siyo sehemu ya ulinzi wa eneo hilo bali wako kwenye biashara hiyo.
“Siyo walinzi bwana, hao ni watu wako kwenye biashara ya kujiuza, kama upoupo utaona kinachoendelea,” alisema mlinzi huyo kwa shari la kutochorwa jina kwenye ukurasa huu.

MIDUME YATONGOZWA LAIVU
Katika hali ya kushangaza, ndani ya kasino hiyo inayochezesha kamari, walizama wanawake wawili kisha wakawafuata washikaji hao waliokuwa wamejibanza ukutani na kuanza kuwatongoza.
Hakupita muda mrefu, jamaa wawili waliondoka na wanawake hao waliotakata ambapo ‘shushushu’ wetu aliwashuhudia wakiingia kwenye gari na kuondoka eneo hilo huku wakiwadekea mijimama hao.
Ilibidi kuchunguza wanakoelekea ambapo gazeti hili lilitonywa kuwa wanakwenda kuwapa ‘dozi’ na wakimaliza watarejea kwa ajili ya kujipatia wateja wengine.

MWINGINE ACHUKULIWA,
MMOJA AREJEA
Haukupita muda mrefu ambapo alifika mwanamke wa makamo aliyetapakaa dhahabu shingoni, mikononi na miguuni ambapo alionesha ishara ya kumwita kijana mmoja, ndipo washikaji hao walipoanza kupigana vikumbo kumuwahi lakini alichagua mmoja akatimka naye kusikojulikana.
Wakati huyo akichukuliwa, mmoja wa wale walioondoka awali alirejea ‘kijiweni’ na kuendelea na biashara hiyo.

SEHEMU NYINGINE ZA STAREHE
Katika klabu na sehemu nyingine za starehe biashara hiyo kwa sasa imeshamiri kwani haina kificho.

WAMO WAKE WA VIGOGO
Kuna madai kuwa, baadhi ya wanawake wanaowachukua vijana hao ni wake wa vigogo (wanasiasa) na watumishi wa serikalini ambao ndoa zao hazijatulia.
 
Eee Mungu usinipe usingizi kabla sijaiona Tanzania ya kesho na hata ya kesho kutwa..Awali nilipuuza nikifikiri ni mashoga, sasa kama ndio hii loooooooooooooooh!. Ndio maana sasa hivi siwaoni tena wanalinda milango ya kumbi za starehe na sherehe.
 
Duuh, sasa hawa tutawaitaje ?ni machangudoa wa kiume au tuwatafutie jina lingine?hahahaaa

Inabidi tusubiri watohoa lugha watuletee jina kwani hata Changudoa lililetwa na hao hao. Kazi kwelix2.
 
Eee Mungu usinipe usingizi kabla sijaiona Tanzania ya kesho na hata ya kesho kutwa..Awali nilipuuza nikifikiri ni mashoga, sasa kama ndio hii loooooooooooooooh!. Ndio maana sasa hivi siwaoni tena wanalinda milango ya kumbi za starehe na sherehe.
Hii ndo habari ya mjini mkuu!!
natamani kurudi kijijni nisiyaone haya yakitendeka kwa kweli!
 
Hii ndo habari ya mjini mkuu!!
natamani kurudi kijijni nisiyaone haya yakitendeka kwa kweli!

Ukirudi utakosa historia bora tubaki ili tuje kuwaeleza wajukuu....Si unakumbuka babu zetu walivyotuambia walipotoka.
 
yaani kidume mzima nalipwa hela na jimama nikamt0ml3e. Kongosho ataniachia radhi :<
 
Last edited by a moderator:
Wanaume wanaojiuza hata mitaani wapo wengine wanakodi magari na kujitembeza katiti ya mji na sehemu maharufu na kwenye maofisi makubwa na mawizara kuwawinda wadada wenye kazi mzuri ili wapate unafuu wa maisha kwa naija wanaitwa majigolo kama ni wengi na akiwa mmoja anaitw jigolo makubwa haya hapa waitweje?
 
Wanaume wanaojiuza hata mitaani wapo wengine wanakodi magari na kujitembeza katiti ya mji na sehemu maharufu na kwenye maofisi makubwa na mawizara kuwawinda wadada wenye kazi mzuri ili wapate unafuu wa maisha kwa naija wanaitwa majigolo kama ni wengi na akiwa mmoja anaitw jigolo makubwa haya hapa waitweje?
Duh!!!!! kuna njia nyingi kweli za kujipatia kipato!!!
 
Back
Top Bottom