Hapo umeongea mambo mengi kwa wakati mmoja. Umevuruga,vuruga tu. Lakini nije kwako kihivi
1. Umesema wanaume hawazeeki ni kama mengi,azam na mo. Lakini vipi wengine? Wewe unahisi matajiri wote wanajitangaza?
2. Umesema wanaume wasiozeeka ni wale waliowekeza. Umewataja,lakini umejisifia kwamba babaako aliwekeza wewe na kakaako mtakula miaka mingi. Katika hao uliowataja,mengi,mo babaako ni yupi?
3. Umesema wanaume watafute halafu uje utumie wewe kwa kujisifia?
4. Mbona huyo kakaako anatumia walivyotafuta wengine?
5. Mwisho wewe kabinti ka juzi,hamjui hata mali zinatafutweje? Hapo hujui hata huyo babaako uliuza nini ndio akapata hizo mali. Zaidi ya yote usije ukajidanganya kwamba kuna mali ambayo haishi hasa zikiwakuta nyie watumiaji tu,wapenda sifa. Uliza Mabutu seseseko kuku wa zabanga,aliwekeza nini? Na nini kimebaki?. Hakuna utajiri unaodumu hata uwekeze kwa mawe na dhahabu,hasa zikiwakuta nyie wapenda sifa