Mwanaume bila kazi nyumbani:

Mwanaume bila kazi nyumbani:

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,755
Reaction score
2,303
Nianze kwa Kusema Habari wapendwa Marafiki wana Jf, Binafsi nawapongeza wajumbe wa humu tunajifunza mengi kupitia nyinyi amini usiamini. Huku kuna Great thikers kwelikweli:


Nataka tuongee kitu kimoja tu jioni hii. Ivi ikitokea kama baba wa familia akiwa mtu wa nyumbani kula kulala Baada ya kazi au biashara alokuwa akitafuta liziki kukwama kuna ubaya?!
Mama unao uwezo wa kuihudumia familia vizuri tu,
Je mume huyu ni halali kunyanyapaliwa na mkewe na kuambiwa akatafute kazi kila kukicha wakati hajui akaanzie wapi na pa kuishia? Na tuna weza sema huu ni uzembe?!
Note that: Imetokea kwa mpangaji mwenzangu hapa hom
ametemeshwa kibarua, Sasa mkewe amekuwa gumzo kumsema jamaa Inaniuma sana sometime najiuliza ningekuwa mimi sijui ningemfanya nini huyu mwanamke...! Sizani kama yuko sawa kabisa!
¤WEWE UNAMZUNGUMZIAJE HUYU MAMA¤
 
Ukiachishwa au ukifukuzwa kazi haina maana ndo ukae tu nyumbani ule, ulale, na unye.

Badala yake inatakiwa uchakarike kutafuta kibarua ama riziki ingine.

Vile vile, usiruhusu na usimpe mwanya mwanamke akunyanyase kwa maneno ya dharau.

Lakini unapoachishwa kazi na kukaa tu nyumbani bila kuchakarika unampa mwanamke wako nafasi ya kimaadili ya kukusema huo uzembe wako.

Kuachishwa kazi si mwisho wa dunia. Ukiachishwa hapa tafuta kazi kwingine.
 
ni kukosa akili tu mbona kuna wanawake wameolewa na hawana kazi wanakula na kulala lakini husikii mwanaume akimsema mwanamke ndio tatizo la kuoa mwanamke mfanyakazi kazi ikiisha huna chako
 
Ni halali kwa mwanamke kufanya anayo fanya, hamnyanyasi ila anacho kifanya ni kumkumbusha jamaa wajibu wake.

Ni hivi, women are for intimacy and not direction and purpose (feminine energy),

men are for direction and purpose (masculine energy).

Unaposahau/ acha wajibu wako mkeo anakukumbusha kwa njia mbali mbali.

Hapo huyo mwanamke anafanya wajibu wake. Binafsi nampa big up 100%
 
Kama una binti wa watu na mshakua na watoto kua na kazi nilazima, kama huna mtakula nini? Mpangaji wako anatatizo, kama si mvivu, mzembe basi hapendi kazi
 
Sasa huyo mwanamke ana mpango wa kukaa tu nyumbani mpaka lini???
 
tatizo mwanamke hatafuti. mambo ya kuachshwa kazi ni ya kawaida sio tz bali duniani kote. ila dunia ya sasa watu hawana mashamba kama zamani kuwa mchicha ukihitajika unaambiwa kaokoteze shambani,mahindi yako ndani,maharage yako, na alizeti iko mkitaka mafuta . sasa ni hapana hizo basic zinahitaji pesa, mwanamke anatakiwa kufanya kazi/biashara ya kipato na mwanaume hivyi hivyo akikusa mmoja mwingine anaendelea angali mwingine anatafuta sehemu mpya ya kujishika. kazi kama afisa utumishi usitegemee kujiajiri au upate kazi fasta inahitaji muda.
 
Huyo mwanamke hana akiri! Hajui kuwa Maisha hayana formula?
 
Back
Top Bottom