Mwanaume amuua mpenzi wake gesti

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
MKAZI wa jijini Mwanza, Thomas Jilala (22), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kumuua anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Levina Kiwili (26), mkazi wa Mfaranyaki katika Manispaa ya Songea, ambaye alikutwa akiwa amekufa kwa kunyongwa shingo katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi, mjini Songea.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Paulo Mashimbi, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa 2 asubuhi, huko kwenye nyumba ya kulala wageni chumba namba kumi.
Mashimbi alisema kuwa ililetwa taarifa katika kituo kikuu cha polisi mjini Songea, kuwa katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi chumba namba kumi kilichokuwa kikitumika na watu wawili, alikutwa mwanamke akiwa amefariki huku mwanaume aliyekuwa naye akiwa amekimbia.
Alisema kuwa Oktoba 23 mwaka huu, saa sita usiku mtuhumiwa anayedaiwa kufanya mauaji hayo, ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa marehemu, alikamatwa akiwa anatoroka kuelekea barabara ya Songea-Tunduru maeneo ya Namtumbo.
Alieleza kuwa mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikutwa na baadhi ya vitu vya marehemu ikiwemo saa aliyokuwa ameivaa kabla ya kuuawa pamoja na simu mbili za mkononi.
Alifafanua kuwa mtuhumiwa pia alikutwa na vifaa vingine vilivyoibiwa kwenye ofisi aliyokuwa akifanyia kazi marehemu usiku wa kuamkia siku ya tukio.
Hata hivyo vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Jilala kabla hajafanya kitendo hicho, alikuwa akionekana mara kwa mara katika ofisi ya marehemu ijulikanayo kwa jina la Mpenda Production kwa madai kuwa amekuja kutengeneza kadi za harusi ya kaka yake.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limesema linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na kwamba baada ya uchunguzi huo kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji linalomkabili.

Source: Mwanaume amuua mpenzi wake gesti
 
Sijui jamaa alikuwa hana pesa ya kumlipa?
Au jamaa alilazimisha tiGo? dah
Alafu jamaa umri dogo kuliko demu
R.I.P Levina Kiwili
 
Mbona haya mambo yako mengi sikuhizi kuna tangazo liliwahi kuwekwa kina dada msikukuruke na wanaume msiowajua nimeskia issue nyingi hasa bongo kuna jamaa(majamaa)wanatafuta sana wake za watu wakienda nao wanaua(kwa kitu cha ncha kali au kunyonga) fasta tu
 
Sijui jamaa alikuwa hana pesa ya kumlipa?
Au jamaa alilazimisha tiGo? dah
Alafu jamaa umri dogo kuliko demu
R.I.P Levina Kiwili
Lol....... Umri mdogo lakini ana manguvu ya kunyonga umri mkubwa...
Anyway R.I.P Levina!
 
Hata hizi style nyingine inabidi watu kuwa makini nazo, unaweza kukuta mtu amepindwa mpaka unashangaa!
 
Dah...........wadada kweli mko hatarini! jamaa katumia gia ya kumwangukia; akaiba ofisini na kisha kuondoa ushahidi kaamua kummaliza..............masikini dada wa watu!
 
22yrs??? Jamani mkumbuke muumba wako enzi za ujana wako, uache ya dunia, madawa ya kulevywa, uache uasherati na ulevi!! Epuka hukumu!
 
Hakunaga zaidi yangu mi na wewe...jamaniiiii haya mambo yataisha lini? kama kakupa mzigo na ukachapa ya nini uue? Idiot
R.I.P Revina huna hatia japo umetimiza wajibu wako lakini jamaa hakuona umuhimu wako.
 
Hata hizi style nyingine inabidi watu kuwa makini nazo, unaweza kukuta mtu amepindwa mpaka unashangaa!

Hahahaha mzazi kweli kuna style zingine noma mdada anabiduka za masoti balaa kama wheel barrow style hii noma mzazi
 
Lol...so mshikaji yaezekana alikuwa katika kutafuta utamu ulikojificha akajikuta ameua au?

Jamaa alikunja kama nyani akasahau kuwa dada analia maumivu ya shingo imenasa kwenye chaga yeye akajua analia kwa ajili ya utamu akaongeza speed
 
Jamaa alikunja kama nyani akasahau kuwa dada analia maumivu ya shingo imenasa kwenye chaga yeye akajua analia kwa ajili ya utamu akaongeza speed
Hahahaha! Fidel utanilipa hizi mbavu zangu zilizoteguka?...lol
 
Hahahaha! Fidel utanilipa hizi mbavu zangu zilizoteguka?...lol

Cheka nusu
Hapo jamaa kuja kushtuka mtu kasizi kasikilizia kama nusu saa haamki lol akaamua kukusanya nyaraka muhimu za dada na kuchapa mwendo. Hii ilimtokea hata bro. yeye bahati nzuri yule binti alikuwa anazimia tu alicho haribu alizimia kwenye geto la bro akaamua kumbeba usiku kwa usiku na kwenda kumuegesha karibu na kwao yeye bro alijua nae kaua lol mchana anamkuta anadunda mtaani.
 
Hahahahaha! Nna hakika bro nae kidogo azimie baada ya kukutana na marehemu anadunda lol...kumbe wakati mwingine watu wanaua bila kukusudia eeh? Nimecheka sana!... Sasa ya bro iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom