Mwanaume ampe mkewe asilimia ngapi ya mshahara

Ushauri hapa jf ni bure bila gharama. Ila gharama ni kuutekeleza.
Kwanza; Je, umemuoa? Mna muda gani tangu mkae pamoja? Umemsoma vizuri kitabia?? Je ana mipango mizuri ya maendeleo?
Hayo ndiyo yatakupelekea umpe mshahara wako wote au umpe tu hela ya chakula kila siku. Unaweza amua kwenda weka pesa yako kwenye duka la Mangi uwe ukichukua hapo kidogo kidogo kila siku jioni. Umuachie mkeo kwani hata ukimpa ruksa kwenda kuchukua mwenyewe kwa Mangi, atakuibia.
Wapo wanawake yaani ni ngekewa tupu. Ukimwachia elfu 5 kwa siku, mnakula hadi mnashiba. Unga kidogo tu, unaumuka ka kaweka amira. Wapo wengine hata ukileta unga kg 5 hautoshi ugali. Sio kwamba kaumwaga. Hapana. Ni mkono wake tu mbaya.
Hivyo kwamba umwachie kiasi gani, itatokana na hayo hapo juu
 
Mwanamke anashirikishwa kwenye mipango ya maendeleo pekee,ukiwa unampa hela ata peleka kwenye vikoba mara vikundi alafu atarudi kukuomba tena ela ya matusi mwezi huo huo.
 
Mwanaume akishapokea mshahara anatakiwa ampe mkewe asilimia ngapi ya mshahara na asidai pesa nyingine hadi mwezi ujao, pesa hizo ni pamoja na pesa za chakula, matumizi yake na matumizi ya watoto
Itadepend na lifestyle yao .
 
Maana yake hiyo ni paka sio mke
 
Mwanaume akishapokea mshahara anatakiwa ampe mkewe asilimia ngapi ya mshahara na asidai pesa nyingine hadi mwezi ujao, pesa hizo ni pamoja na pesa za chakula, matumizi yake na matumizi ya watoto
Hata ukimpa 100% ya kipato chako haisaidii kitu, budget ya mwanamke inapangwa kutokana na hela iliyopo na mahitaji ya mwanamke hayana kikomo Hata ukimpa Mali za dunia yote. Mahitaji ya mwanamke yanabadilika kutokana na hisia zake, zikibadilika na mahitaji yanabadilika.
 
Let say mshahara wangu ni 1m ,ntampa laki 3.5 za matumiz ya nyumban,laki 2 kwa matumiz yangu binafis,laki 4.5 kwa maendeleo,
 
Mwanaume akishapokea mshahara anatakiwa ampe mkewe asilimia ngapi ya mshahara na asidai pesa nyingine hadi mwezi ujao, pesa hizo ni pamoja na pesa za chakula, matumizi yake na matumizi ya watoto
Hela ya kumpa inategemea na haya
1. Ukubwa wa mshahara
2. Matumizi kwenye chakula Kwa siku halafu zidisha mara 30
3. Matumizi yake yenye tija Kwa mwezi

Etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…