Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Mwanaume huyu toka jamii kutoka Ndola aliamua kumuacha mke wake waliyeoana miaka saba iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Mwanamke huyu alienda mahakamani ilikutafuta suluhu ya ndoa yake na maridhiano na mume wake, akiomba mahakama imsaidie kunusuru ndoa yake na kuongeza kuwa hajui kwanini mume wake aliamua kuchukua uamuzi wa kumuacha na kuoa mfanya kazi wao wa ndani.
- Mwanamke huyu aliiambia mahakama kuwa anampenda mume wake na haamini kama kweli ameamua kufanya kitu kama kile na kutaka kujua sababu zilizopelekea mume wake afanye hivyo.
- Mahakama ilipomuuliza mwanaume juu ya suala hilo alisema hawezi kubadili msimamo wake na hawezi kumuacha mke wake mpya wala hawezi kumrudia mke wake wa zamani maana maamzi yake ndio yalikuwa yameshafika mwisho na kushukuru kumpata mtu sahihi kwake na kusema mwanzo alifanya makosa kwenye kuchgua mke bila yeye kumjua mwanamke huyo vizuri.
Akaendelea kuaiambia mahakama kuwa mke wake huyo wa zamani alikuwa mzembe kupita kiasi, hakuweza hata kufanya kazi za ndani zinazomhusu kama mama wa familia na badala yake hata yale majukumu yake kwa mumewe aliyaacha mikononi mwa mfanyakazi wao wa ndani ambaye alijikuta kuwa ndio msaada mkubwa kwa mwanaume huyu , mfanyakazi wao wa ndani ndio aliyefua nguo zote za mwanaume huyo huku mke wake akiwa hana habari nae, hakutaka hata kukaa na kuongea na mume wake isipokuwa mfanyakazi wa ndani alikuwa akimuona amerudi toka kazini anampokea na kumuandalia maji ya kuoga, kisha anampa chakula na kukaa na kuongea nae sebuleni huku akimpa pole kwa uchovu na kumtia nguvu pindi anapoonekana kuchoka sana au kuwa na mawazo.
-Kuhusiana na suala hilo wazee walishawakalisha chini na ili kuwapatanisha bila mafanikio yeyote kwa wanandoa hao.
Alichokuwa akikifanya mwanamke huyu nyumbani ni kuwa bize kutoa maelekezo kwa mfanyakazi huyo wa ndani na kumfokea muda wote na kuwa bize na simu huku mfanya kazi wa ndani akiwa bize na mwanaume baba wa familia, hivyo niliona kila mtu abaki na kitu anachopenda kuwa bize nacho muda wote, mfanyakazi wa ndani anapenda kuwa bize na baba wa familia basi ni vyema awe nae aliatimize majukumu yake kwa baba wa familia vizuri, na mke wake kwa sababu yuko bize na simu basi nimuachie nafasi akae na kuchati kwa uhuru ili kila jambo liende sawa pia kwa upande wake.
Mume aliendelea kusema hata siku za mwisho wa juma (weekends) akiwa hayuko kazini mwanamke hakuona umuhimu wa kupika chakula kwa ajili ya mume wake kama alivyokuwa akifanya siku za mwanzo wa ndoa yao,badala yake alikuwa akifanya maandalizi ya kwenda kwenye sherehe za harusi na kamati za Kitchen Party, anarudi amelewa kitu ambacho mwanzo alikuwa hafanyi, na kama angekuwa anafanya nisingemuoa kabisa.
-Mume akaenda mbele zaidi na kuiomba mahakama iangalie kwa makini kucha ndefu za mwanamke huyo kama kweli zinaonesha mwanamke anayeweza kujishughulisha na shughuli za nyumbani kama mke wa mtu, muulizeni ana miaka mingapi hajawahi kupika chakula, kufanya kazi za nyumbani zaidi ya kuagiza, nani amekuwa akitandika kitanda changu kwa muda wa miezi nane sasa ?, Ni lini amejishughulisha hata kutunza na kuangalia watoto kama kweli ni mwanamke anayefaa kuwa mke, hayo yote mfanyakazi wa ndani ambaye ni mke wangu sasa ndio amekuwa akiyafanya siku zote.
Baada ya mahakama kujiridhisha na maneno ya mume ikatengua ndoa hiyo ili sasa mwanamke aendelee kuchat bila kikomo, ahudhurie sherehe za fungate, harusi na kufuga kucha huku mfanyakazi wa ndani akiwa boss ndani ya nyumba mwenye kujua na kujali majukumu yake kwa undani.
Wanaweke wengi huyajua makosa yao na ukimya wa mwanaume humfanya ayaendeleze bila kujua mwanaume muda mwingine yuko kimya akiwaza hatima ya jambo hilo na mwisho anaweza kuja na uamzi mwingine
Kuna la kujifunza.