[h=1]Mtoto wa Aliyekuwa Haini Ateuliwa kuwa AG[/h] Written by
abdisalum
Inashangaza sana kuona uteuzi kama huu umepitishwa na SMZ, serikali ambayo imeshikilia mrengo mkali sana wa kimuhafidhina wa kutokukubali mabadiliko.
Said Hassan Said, ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa SMZ.
Huyu ni mtoto wa Bwana Hassan Said Mzee (ex-comrade) na aliwahi kushtakiwa au kuhusishwa na kesi ya uhaini ya kumuuwa Mzee Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar.
Nakumbuka kati ya watu walioteswa vibaya sana pale kwa Ba-mkwe chumba cha mateso Zanzibar alikuwa huyu Bwana Hassan Said Mzee, Hashil Seif (comrade, former Navy officer) na Shafi Adam Shafi (watu wengi tulidhani wakati huo kuwa hawa wameshakufa kw amateso waliyoyapata). Uhai uko kwa Allah sio kwa Mandera (mtesaji).
Katika mifumo ya ajira v.s security (vetting) ya kidunia na hapa Zanzibar hususan, mtu kama huyu huwezi kumpa nafasi kama hii kubwa na nyeti.
Tuseme leo AG wetu mpya akiamua kupekua mafaili ya huko nyuma na akaona mambo juu ya mambo na vijambo itakuaje?
Kuna kesi mbili ttau ninazijuua Tanzania/na Zanzibar kuwa ajira fulani fulani zilifutwa just kwa sababu ya uhusiano wa baba/na mwana katika kesi hii ya uhaini ua kumuuwa Mzee Karume (mmoja amekosa Urais
.! na mmoja amekosa Urubani wa ndege ya Rais
n.k n.k) na nyingine nyingi.
Vipi wengine wakoseshwe na wengine wapatiwe???
Najua kuwa Bwana Hassan Said, Mzee wake huyu AG mpya alikuwa comrade, na mpinzani wa dhahir then chini kwa chini; lakini baadaye alibadilika na kuwa pro-system na kufikia kuwa kamishna wa tume ya uchaguzi ya mwanzo ya Zanzibar chini ya Dr.Salmin Amour.
Huenda ikawa hii ni bahshish yake ya matokeo ya uchaguzi ya mwaka 1995.
.you scratch my back
.Ashak malizia hapa
.mie sijui kizungu mwanangu weeee
wenzetu wengine wanasema nipe-nikupe, wengine wanasema ihsani inalipwa kwa ihsani
..wengine ni quid pro quo
.wengine /fadhila
..min fadhilikya
tuipokeee katiba mpya kwa mbwemwbe zote
Ehhh na vipi ile ibara inayosema kuwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa TZ ndiye atayeteuwa Wakuu wa Mikoa Zbar, ina maana mpaka masheha, maana technically, RC ndiye anayeteuwa masheha hapa kwetu. Je akama aRais wa TZ atateuwa Bwana Rweikiza kutoka Ngara, Kagera, kama anavyoona yeye inafaa na masheha pia wataoka huko huko kwa sababu na yeye RC ataona hao wa kwao ndio wanaofaa wale akina Vuai, Ame, Simai, jecha na askari wastaafu basi tena
.au vipi jamani??
Ashak hebu nisaidie translation ya ibara hii.
Na ile kuwa Rasimu hii inatambua JWTZ na Polisi na JKT tu, vikosi vyetu vya SMZ hamna mle, itakuaje????? Je, tuvivunje vikosi vyetu vya SMZ? Almuradi utamu juu ya utamu mwaka huu??