Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aikataa Katiba

MoPlan

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
908
660
Hivi punde akipiga kura baada ya kuja bungeni,amepiga kura ya Hapana kwa sura kadhaa na ibara kadhaa.

Baada ya kupiga kura ya Hapana,kuna mjumbe amesimama na kuomba muongozo ambapo amemshambulia kwa dhihaka na kejeli huku akiungwa mkono na wajumbe karibu wote wa CCM bara na wakisema hafai,mnafiki etc huku Sitta akionekana dhahiri kuruhusu vijembe hivyo na hatimae kahairisha bunge hadi Kesho.

Ikumbukwe kuwa Mwanasheria huyu wa Zanzibar alijiuzuru ujumbe wa kamati ya uandishi iliyo chini ya Chenge baada ya wajumbe wenzie kukataa mambo 17 aliyoyaleta ya Zanzibar yasiingie kwenye katiba ila bunge na kina Sitta walifanya siri.



UPDATE,

akundubhyali 13:35 Today

Amekataa Ibara za 2,9,86,70 hadi 75, 128, 129,158,159,160,161,243 hadi 251 pamoja na nyongeza ya kwanza, maudhui yake hayo hapa:
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

9. Ukuu na utii wa Katiba
70. Muundo wa Muungano
71. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi
72. Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
73. Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano
74. Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
75. Wajibu wa viongozi wakuu kulinda Muungano

86. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais

128. Madaraka ya kutunga Sheria
129. Utaratibu wa kubadilisha Katiba

158. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mamlaka yake

159. Rais wa Zanzibar na mamlaka yake

160. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na kazi zake

161. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

243. Misingi ya matumizi ya fedha za umma
244. Akaunti ya Fedha ya Pamoja
245. Tume ya Pamoja ya Fedha
246. Mfuko Mkuu wa Hazina
247. Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina

248. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina
249. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali kuanza kutumika
250. Mfuko wa Matumizi ya Dharura
251. Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina

Nyongeza ya Kwanza: Mambo 14 ya Muungano

UPDATES;
MWANASHERIA MKUU CHINI YA ULINZI!!

Haki sawa 13:04 Today
Leo muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kupiga kura ya wazi ya Hapana kuhusu katiba amekamatwa na watu wa idara ya usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar kama ni kweli anapeleka Zanzibar ama Mambwepande .......

Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana , ila hali inawez kuchafuka wakati Wowote visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .

Updates:
Hali ilikuwa mbaya Sana mara baada ya kupiga kura kwani wabunge wa CCM znz walitaka kumpiga ndio akalazikima kutolewa ukumbini chini ya ulinzi mkali na kufungiwa kwenye ofisi moja akiwa ameandamana na Pandu Ameir Kificho, Balozi Seif Idd, Nahodha , Pinda na baada ya muda aliondolewa hapo Akiwa ameandamana nafPandu Kificho kwenye gari yake kupitia lango la Waziri Mkuu akiwa ameambatana na msafara wa maafisa usalama, na kupelekwa Airport ......

wale wenye Mashaka na habari hii wasilianeni na Dom mtapataukweli ,

Inasemekana amepelekwa airport yadDodoma , ila not yetdconfirmed ,,,,,

Kumbukumbu :::
1. Aboud Jumbe Mwinyi mwaka 1984 , alinyanganywa Urais akiwa Dodoma na mpaka leo yuko Kigamboni
2. Maalim Seif Shariff and wenzake mwaka 1988 , alinyanganywa uwaziri kiongozi akiwa Dodoma
3. Mansour Himid , mwaka 2013 alinyanganywa Ubunge akiwa Dodoma.
4. Othman Masoud , mwanasheria mkuu znz atapona kweli ?




more to come .
 
Hii sio tetesi ni ukweli mods rekebisha heading na mpaka sasa ndio anatukana na wabunge wa znz ukumbini.
 
Hivi punde akipiga kura baada ya kuja bungeni,amepiga kura ya Hapana kwa sura kadhaa na ibara kadhaa!!
Mungu awabariki wote wanaopiga kura za hapana,hao ndiyo mashujaa wetu. Hongereni makamanda muipendao nchi yetu,kura za hapana ndiyo mpango mzima. HAPANA,HAPANA,HAPANA Kuanzia bungeni mpaka mitaani, Warioba naungana naye kwamba tutakutana mtaani na hapo ndiyo watatujua kuwa hatupendi unafki.
 
Hao ndo watetezi wa kweli wa zanzibar, nadhani wale vibaraka wa maccm na watanganyika kule zanzibar watasema sana!
 
sio tetesi amepiga kura ya Hapana kwenye zile ibara za msingi za Muungano na alizo kubali ni kama amekubali Jina tu kwenye hiyo Rasimu kwamba lipo..!
 
Back
Top Bottom