Mwanariadha Jackline Sakilu Ashinda Tuzo za TASWA kwa Mwezi Februari, 2024

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
310
288
IMG_8486.jpeg

Mwanariadha wa Kimataifa, Staff Sergeant (SSgt) Jackline Juma Sakilu wa JWTZ, amechaguliwa kuwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwezi Februari , 2024 katika tuzo zinazotolewa na chama Cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA).
IMG_8105.jpeg

Kushoto : Jackline Sakilu na Alphonce Simbu

TUKUMBUKE;

Jackline Juma Sakilu ALIVUNJA Rekodi ya Taifa kwa sekunde 33, kwenye Mbio Ndefu za Kilomita 21, Kwa kushika nafasi ya Tatu Kwa Muda wa 1:06:04 (Half Marathon) Tarehe 24/02/2024 , Rekodi ya Taifa ambayo iliyokuwa inashikiliwa na Magdalena Shauri kwa muda (1:06:37) toka tarehe 21 February 2020 kwenye Mbio za Ras Al Khaimah Half Marathon (U.A.E) kwenye njia hiyo hiyo, na wote ni Wanariadha kutoka (JWTZ).
 
Back
Top Bottom