Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Dah pole sana jamani kaka,
Pole sana jamani.
Kuna clip niliona,watoto wenye tatizo la kchelewa kuongea wanawekea nyimbo,na mazoezi flani flan
Ila sikuizingatia ngoja niigogle kama nnitaiona
Again pole sana
 
Mkuu hongera umezaa bonge la genius maybe atakuja kubadilisha hii nchi kwa namna fulan Ila ana nyota Kali sanaa jitahidi kimtafutia Kinga za aina mbalimbali

EPUKA MATAPELI..
 
Pole sana
Hiyo millioni tano itenge kwa kumnunulia vifuatavyo
Sensory toys - Hizi ni aina ya toys ambazo zinaamsha akili ya mtoto katika kuchezea, inaweza kuwa kwa kushikashika hii ina inaleta msisimko kwenye touch sensing, kumbuka sisi wadogo tumefinyanga sana magari ya na midoli ya udongo, au kuzipanga kama vipande vya maumbo yanayoleta picha kamili, hii ina mfanya aanze kutumia akili,
Aina nyingine ya hizi toys inaweza kuwa zenye kutoa sauti, kama ngoma firimbi, hii itamsaidia kuielewa aina za sauti abapo atakapo kuja kuzisikia haitamshtua, kumbuka watoto wa wenye autism huwa hawapendi makelele,
Ocuupational therapy toys - Hiizi ni aina ya toys zitakazomjenga mtoto kushika nakutumia vitu yaani itamtengenezea coordination mfano ni toys za kuhesabu, za maumbo tofauti na pia za kupanga vitu kimpangilio mfano kutunga vitu vyenye tundu kutumia kamba au uzi.

Haya ninayaandika kwa kuwa nimeyapitia

Na kama unaweza mnunumie kishikwambi chenye kufundisha au michezo ya watoto, mara nyingi na kwa niliyoyapitia mimi, atajifunza kutamka maneno kwa kufuata na kuimba mwenyewe kwa pia kwa kumsaidia lakini ni vigumu kuwa naye muda wote kwa hiyo kishikwambi kitasaidia kwake mwenyewe kujifunza
watoto wenye autism wanapenda kujifunza sana wenyewe ukiwawezesha,
Leo hii mtoto wangu ana miaka 10 anacode game zake mwenyewe za platformer.
alikuwa ukimletea toys anakufuata umuonyeshe inavyotumika ukiwa katikati ya kumuonyesha anakupokonya na kuendelea mwenyewe .

Kumbuka unatakiwa kama mzazi utenge muda wa kukaa na kufanya haya na mtoto wako.
 
Acheni ujinga aisee. Yan eti anapenda hicho kitu cha kuning’iniza nguo ya mama ake ya ndani anakuja nayo sebuleni? 😂😂😂

Mkuu uko serious? Kwamba huyo mke hajui kutunza vitu? Kyupi mnawekaje sehemu zinapoonekana na mtoto?
Acha upumbavu wako wa Facebook. Yaani katika maelezo yote umezingatia Chupi tu.!?
 
Acheni ujinga aisee. Yan eti anapenda hicho kitu cha kuning’iniza nguo ya mama ake ya ndani anakuja nayo sebuleni? 😂😂😂

Mkuu uko serious? Kwamba huyo mke hajui kutunza vitu? Kyupi mnawekaje sehemu zinapoonekana na mtoto?
Kyupi 😂😁
 
Mimi ni mama wa mtoto mwenye autism! Naomba nikazie hapa .
 
Pole , je tatizo haliishi?
Tatizo ukiliwahi kwa kufanya therapy na vyakula matunda na dawa japo izi dawa aziponeshi ila zinatuliza vile vile moods!

Mimi huwa naagiza nje na zinagharama mpaka kufika Tz !Kuna vitaminiD3, ADHD fish oil omega 3, magnesium glycinate. Hii husaidia kupata usingiz , magnesium citrate hii inasaidia kupata choo coz autism people wanasumbuliwa na consipation, magnesium L,threonate hii inasaidia cognitive, function memory, depression, anxiety and sleep! Zinc

Hizi ni supplemental anatumia mtoto hadi mtu mzima mwenye usonji Kwaiyo ukiwafwatilia vyakula unavyompa na therapy shulen nyumban.

Mzazi jitahidi sana kumsemesha mtoto wako usikate tamaa siku adi siku anayaelewa yale maneno! Pia msemeshe maneno mepesi! Mfano acha au hapa na usimsemeshe neno lenye msamiati mgumu!

Mpongeze akiweza kutamka neno au kukuiga kitendo! Mzazi ndio mtu pekee anakaa na mtoto masaa Mengi kuliko shule
 
Pole sana! Mpeleke shule za watu wenye usonji watamtrain atadevelop taratibu! Usonji autaki haraka!Muombe Mungu maisha Malefu umtunze mwanao!

Mfundishe kama kaweza kula ataweza kufanya na kitu kingine! Mwenyezi Mungu anawapa wazazi strong anajua utaweza ilo jaribu ndio maana kakupa mtoto wa ivyo! Some times Unaweza kuwa na pesa na pesa isikusaidie !

Mungu aliekupa uyo mtoto mtegemee kwa kila kitu! Usisahau therapy kwa mtoto kumsemesha ivyoivyo msemeshe mpeleke afanyiwe na mazoez ya mikono yake iwenanguvu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…