“Mwanangu, mwenzio akikushika makalio usikubali…”

“Mwanangu, mwenzio akikushika makalio usikubali…”

Mtambuzi ni kweli kabisa USHOGA upo na Huanza kama mchezo mchezo tu...Watoto wanaiga kwa kusikia au UDADISI unaotokana aidha na uzembe wa WAZAZI au MAJIRANI...Kumwambia kama alivofanya Huyo jamaa yako ni NJIA mojawapo kwa sababu inasaidia kuufanya moyo wa MTOTO kushtuka kama akikutana na JAMBO kama hilo..BUT all in all utandawazi umekuja na KUACHANAWAZI!!
 
Last edited by a moderator:
05.jpg


hayo yalikuwa ni maneno ya jirani yangu wakati fulani akimuonya mwanawe wa kiume ambaye alikuwa anakwenda kutembelea mbuga za wanyama kama moja ya ziara za mafunzo shuleni. Alikuwa ni mvulana wa miaka kumi hivi na alikuwa anasoma darasa la nne.

nilishikwa na udadisi, nikamuuliza jirani yangu, kuhusu ile tahadhari kwa mwanae, kwamba alikuwa na maana gani? Akanijibu kwa kuniambia kwamba hapo zamani hofu ilikuwa ni kwa mtoto wa kike, linapokuja swala la mapenzi utotoni, lakini siku hizi hata watoto wa kiume si salama tena…!

“kuna tabia mbaya sana mashuleni ya watoto wa kiume kulawitiana hususan shule za mabweni au wanapokwenda ziara za mafunzo. Kwa kuwa wanalala wawili wawili kwenye vitanda, kuna uwezekano mwanao kufanyiwa vitendo vya kulawitiwa. Kama usipomuelimisha mwanao nyumbani, mwenzangu utashangaa mwanao anakuwa shoga” alisema mama wa mtoto huyo.

mazungumzo yangu na mama huyo yalinifanya nijiulize maswali mengi sana, na bado naendelea kujiuliza mpaka leo…. Ina maana watoto wa kiume nao siku hizi sio salama tena…

? Je watoto hawa wanajifunzia wapi mambo haya?

Je wazazi wana wajibu gani katika kukemea jambo hilo?

Je kukemea peke yake kunatosha bila kutoa elimu mashuleni juu ya athari za jambo hilo?


naomba tutafakari kwa pamoja………….


ndio,ni kweli kabisa
angalizo zuri hilo
 
Mtambuzi,,Dunia imetoboka mahali!
::
Nani kasema wazazi wanasitahili lawama? Hatuoni jinsi usasa unavyotawala akili za kila mmoja wetu? Hatuoni mitaala ya elimu inavyopuuzia tamaduni zetu?
::
Hatuoni jinsi Elimu yetu ya shuleni na nyumbani inavyopuuzia somo la mawasiliano? Je watoto wanafundishwa athari za makundi? Je wajua thamani ya miili yao.
::
Maisha yanabadilika upesi sana.Wengi wanashangilia mabadiliko ya malezi,wachache wenye upeo na mabadiliko haya wapo kimya,na wamejificha katikati ya makundi wasionekane.Maana kujulikana kuna gharama zake.
::
Naam,tusiseme la kuvunda hali ubani,serikali,jamii,mimi na wewe tusiwe kimya haya mabaya yanapotokea.HISTORIA itatuhukumu sote tunaosema na tuliokimya wakati tukiona taifa la watoto linasombwa na utandawazi nasi tumeshona midomo.
=
 
alishangaa house girl anatemeana ama anaumana midomo na mkaka wa jirani.
Au alikuwa anamng'oa jino?

He he he, nataka wajukuu jamani lol

jambo lipi hilo? leta udaku mama.

:madgrin: :madgrin: :madgrin:
 
Ndugu yangu Mtambuzi huwa nikifikiria malezi ya watoto wa sasa, kichwa kinaniuma mno. Binafsi nafikiri kama wazazi tunapaswa kutoa malezi sahihi kwa watoto wetu. Kama ni baba mfunze mtoto na kumshirikisha kwenye mambo ya ubaba kulingana na umri wake ili akue akijua kuwa yeye ni baba. Kama ni mtoto wa kike afundishwe na kulelewa kama mtoto wa kike, na kwa pamoja wote tukiwashauri na kuwaeleza watoto mambo mabaya ambayo wanaweza kukutana nayo huko wanakokuwa mbali na sisi wazazi. Ni vyema pia kuwaeleza madhara na ubaya wa hizo tabia chafu.

Nikirudi kwenye maswali yako ...
1. Je watoto hawa wanajifunzia wapi mambo haya?
Hujifunzia shuleni huko kwenye mbweni, nyumbani, vichochorini (kwenye michezo yao), utandawazi (mikanda ya wakubwa, porn sites nk) ma-houseboys (wanaotusaidia kazi nyumbani), kwa baadhi ya walimu, ndugu (wanaolala na watoto wetu), majirani (tunaowakabidhi watoto na kuwaamini) nk

2. Je wazazi wana wajibu gani katika kukemea jambo hilo?
Kukaa karibu na watoto na kujenga nao urafiki, kuwachunguza na kufuatilia tabia na mienendo yao, kuwalinda dhidi ya watu wasioaminika, kuwafundisha juu ya mabaya na uovu wa baadhi ya watu, kuwatahadharisha, kuongea nao na kuwauliza maswali kwa hekima (utapata ukweli watoto hawajui kudanganya) nk

3. Je kukemea peke yake kunatosha bila kutoa elimu mashuleni juu ya athari za jambo hilo?
Kukemea pekee hakutoshi, elimu na ukaribu kwa watoto ni vitu muhimu sana ...

Pamoja na upagani wangu, namuomba Mungu sana kwa ajili ya maisha na tabia za watoto wetu tuliowazaa!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom