Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,443
Hayo yalikuwa ni maneno ya jirani yangu wakati fulani akimuonya mwanawe wa kiume ambaye alikuwa anakwenda kutembelea mbuga za wanyama kama moja ya ziara za mafunzo shuleni. Alikuwa ni mvulana wa miaka kumi hivi na alikuwa anasoma darasa la nne.
Nilishikwa na udadisi, nikamuuliza jirani yangu, kuhusu ile tahadhari kwa mwanae, kwamba alikuwa na maana gani? Akanijibu kwa kuniambia kwamba hapo zamani hofu ilikuwa ni kwa mtoto wa kike, linapokuja swala la mapenzi utotoni, lakini siku hizi hata watoto wa kiume si salama tena…!
"Kuna tabia mbaya sana mashuleni ya watoto wa kiume kulawitiana hususan shule za mabweni au wanapokwenda ziara za mafunzo. Kwa kuwa wanalala wawili wawili kwenye vitanda, kuna uwezekano mwanao kufanyiwa vitendo vya kulawitiwa. Kama usipomuelimisha mwanao nyumbani, mwenzangu utashangaa mwanao anakuwa shoga" alisema mama wa mtoto huyo.
Mazungumzo yangu na mama huyo yalinifanya nijiulize maswali mengi sana, na bado naendelea kujiuliza mpaka leo…. Ina maana watoto wa kiume nao siku hizi sio salama tena…
? Je watoto hawa wanajifunzia wapi mambo haya?
Je wazazi wana wajibu gani katika kukemea jambo hilo?
Je kukemea peke yake kunatosha bila kutoa elimu mashuleni juu ya athari za jambo hilo?
Naomba tutafakari kwa pamoja………….