Mwanangu atasoma shule ya kata kama mimi tu

Mwanangu atasoma shule ya kata kama mimi tu

mimi sina uwezo mkubwa sana...

nimeamua mwanangu asisome shule yoyote ya mtu binafsi.. anasoma shuke ya taasisi yoyote, kanisa au ya serikali tu

atasoma english medium lakini sio ya binafsi...
atasoma olympio au diamond primary yake..

sabab ada ni nafuu.. nawapoza na walimu wachache wamwangalie for a tution.. so nina uhakika atapata elimu bora kuliko nikilipa milioon shule ya mtu binafsi mwenye shule akajenga ghorofa lake au kuonga nyumba ndogo
 
Mtoa Mada anza na "definition" ya Elimu ni nini? Na kwa nini "English " ndiyo ufunguo wa pekee kwa mtoto wa Kitanzania kuweza kuelimika! Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Ukitaka kumsaidia mtu maskini, Mpe mwanae Elimu bora". Utake usitake bila kukimudu Kiingereza angalau kwa wastani, huyo mwanafunzi wa kitanzania elimu bora kwake itakuwa ni ndoto!
Pili kiingereza siyo lazima kifundishwe "English Medium" tu. Wengi wetu hatukusoma hizi shule lakini nakumbuka darasa letu kwenye mtihani wa O level shule ya serikali ufaulu kwenye Kiingereza tulikuwa na wastani wa B. Suluhisho ni kuvizatiti vyuo vya walimu watoe walimu wengi walio bora katika Kiingereza kama zamani.
Kwa taarifa yako China wameanzisha "English Project" nchi nzima kuanzia shule za msingi. Jiulize kwa nini?
 
mkuu huko ni kujinyima wewe na kumnyima mtoto wako.

hakuna familia imemtuma mtu eti ulipe mapesa mengi kwa sababu ya kujifunza lugha ya watu wengine utotoni na ilhali hapo hapo hao hao wanaowasomesha watoto wao lugha hyo ya kigeni wanataka masomo yafundishwe kwa lugha ya nchi yao.

huo ni uchwara ambao mwenye uchwara mwenyewe hajui kama anao.
kuna huduma za msingi sana za kumfanyia mwanao na sio kumharakishia kujua mambo ambayo yapo kinyume na umri wake.
Acha kukariri mkuu we kama hujapanga kupeleka wanao shule hizo acha sisi wengine tulio na mpango huo tupeleke tunajua tunachokifanya hata kama ni kwa kujinyima maana siji kwako kuomba msaada maana kila mtu hupanga afanye nini maishani,hivi umeshajaribu kwenda shule zetu hizi kwenda kuona idadi ya watoto darasani na unadhani mwl atapata wapi muda wa kumsaidia mtoto mmoj mmoja kwa darasa lenye watoto 120? Kwanza walimu wa hizo shule karibu wote wamekata tamaa wanaenda tu kazini alimradi ukiongeza na haya makato yaliyoongezwa ya bodi ya mikopo ndo balaa kabisa........we wapeleke tu wanao lkn wa kwangu mtawapeleka shule ambayo ina walimu walio na ari ya kazi na wako motivated na darasa lina watoto wachache ambao mwl ataweza kumsaidia kila mtoto kwa ukaribu
 
Wewe peleka mwanao shule za kata akakue....

Wenzio wanawapeleka internationl waje kuwatawala

Kupanga ni kuchagua Mkuu
 
Kila mmoja anafnya kitu kinachompa aman, kitu ambcho kwako hakina maana kwa wengne kina maana.
 
Mkuu we fanya vile unapenda tu mm nisome kata mwanangu nae asome kata hapana aisee nitajinyima ili mwanangu asome vizuri
 
Sawa mpeleke, wanao pambana na eng medium kwn wanakuomba msaada, shule tulizosoma ss huwezi fananisha na hizi za kata za sasa,
Pambana na hali yako
 
Acha kukariri mkuu we kama hujapanga kupeleka wanao shule hizo acha sisi wengine tulio na mpango huo tupeleke tunajua tunachokifanya hata kama ni kwa kujinyima maana siji kwako kuomba msaada maana kila mtu hupanga afanye nini maishani,hivi umeshajaribu kwenda shule zetu hizi kwenda kuona idadi ya watoto darasani na unadhani mwl atapata wapi muda wa kumsaidia mtoto mmoj mmoja kwa darasa lenye watoto 120? Kwanza walimu wa hizo shule karibu wote wamekata tamaa wanaenda tu kazini alimradi ukiongeza na haya makato yaliyoongezwa ya bodi ya mikopo ndo balaa kabisa........we wapeleke tu wanao lkn wa kwangu mtawapeleka shule ambayo ina walimu walio na ari ya kazi na wako motivated na darasa lina watoto wachache ambao mwl ataweza kumsaidia kila mtoto kwa ukaribu
Mkuu pokes like x 10 ! Kuna watu Hawaoni uhalisia!
 
Chekechea nilisoma shule ya kanisa,
Primary nikasoma shule za serikali,
Secondary nkasoma shule ya kanisa,
High school nikasoma shule ya serikali,
Chuo kikuu nikasoma chuo cha serikali.

Nachotaka kusema shule zote za serikali nilizosoma zilikuwa na viwango vizuri japo zile za kanisa zlikuwa juu zaidi.
 
Nilipigana ili mwanangu asiishi maisha niliyoishi.
Hatasoma shule za kata
Kiswahili ataongea na wenzake mtaani home ni English
Habari yako Mpendwa,
Unamaoni gani kuhusu matumizi ya lugha ya kufundishia katika ngazi zote za Elimu(Awali-chuokikuu),

Je,kiswahili kitumike au kiingereza kitumike au lugha zote kwa pamoja..?

Shukran!
 
Mtoto wangu atasoma shule niliyo soma Mimi fullstop
 
Kujenga baadae,sababu sijawahi kulala nje
 
Back
Top Bottom