Mwananchi wa kawaida ni nani?

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Neno hili linatumika sana hasa kwenye medani za siasa nchini ,je ni nani hasa ambaye ndio mlengwa wa jina hili ndani ya nchi hii.?
"MWANANCHI WA KAWAIDA"??

Naomba kuwakilisha!
 
Sasa iweje waheshimiwa wetu mjengoni wao wanasimama na kusema "mh spika mwanananchi wa kawaida anaumia" je wao si wananchi wa kawaida?
Mkuu polisi ama.mwanajeshi anaposema "siku hizi hatuishi kambini tunaishi na raia" huwa wao wamepoteza uraia au? Nadhani ni neno tu kama lile la kiingereza yaani layman ambalo layman kwa kitu fulani ni professional kwa kitu kingine.
 
Poisi ni askari na humaanisha "asiyekuwa askari"(raia)
Je madaktari wanapodai malipo zaidi,ndio wanataka kuliacha daraja la mwananchi wa kawaida?
Na kuhamia la waheshimiwa(kipato kikubwa)?
 
Poisi ni askari na humaanisha "asiyekuwa askari"(raia)
Je madaktari wanapodai malipo zaidi,ndio wanataka kuliacha daraja la mwananchi wa kawaida?
Na kuhamia la waheshimiwa(kipato kikubwa)?
Mkuu raia ni nani? Mwananchi wa kawaida ni Commonmwananchi (wewe) kwa Kenya wanaitu Wanjiku na Wamboi. Kwa kifupi ni walalahoi
 
Mkuu raia ni nani? Mwananchi wa kawaida ni Commonmwananchi (wewe) kwa Kenya wanaitu Wanjiku na Wamboi. Kwa kifupi ni walalahoi

Ahsante kwa kulielewa hilo.je waheshimiwa wabunge wetu na familia zao wako kundi hili?au je wanatuwakilisha kama wanavyodai au la.......
 
Ahsante kwa kulielewa hilo.je waheshimiwa wabunge wetu na familia zao wako kundi hili?au je wanatuwakilisha kama wanavyodai au la.......
Wabunge si commonmwananchi. Wao wana uhakika wa kula wao na familia zao. Wanajiwakilisha wao zaidi kuliko wanavyowawakilisha wananchi.
 
Mwananchi wa kawaida ni yule ambae kipato chake hakimtoshi kwa mwezi bila kuiba au kuomba.
 
Wabunge si commonmwananchi. Wao wana uhakika wa kula wao na familia zao. Wanajiwakilisha wao zaidi kuliko wanavyowawakilisha wananchi.

Kwani wabunge kazi yao nini? zaidi ya kutafuta maslahi yao kwanza, halafu ya vyama vyao, halafu mwisho ndio maslahi ya misukule wanaotegemea kuwa wanasiasa wako pale kwa ajili yao na si kwa ajili ya nafsi zao.
 
Neno hili linatumika sana hasa kwenye medani za siasa nchini ,je ni nani hasa ambaye ndio mlengwa wa jina hili ndani ya nchi hii.?
"MWANANCHI WA KAWAIDA"??

Naomba kuwakilisha!
Ili kupata jibu la swali hili inabidi ujiulize kwanza, ni nani asiye mwananchi wa kawaida?
 
Mwananchi wa kawaida ni yule ambae kipato chake hakimtoshi kwa mwezi bila kuiba au kuomba.
hahahah halafu hao wananchi wakawaida wakipata madaraka ndo wanakuwa majambazi kama lowasa, toka kwenye ngoma mpka gufisadi.
 
IMO.... Mwananchi wa kawaida ni lazima itakoa tofauti na jamii husika hasa ki taifa. Hivo nikiangalia jamii ya Tanzania naona kama mwanannchi wa kawaida ni yule ambae huendesha maisha yake ya kila siku kwa nafasi ambayo inatakiwa ichezwe na yeye iwe ni mwajiriwa wa serkali ama binafsi (mwenye kiwango cha kipato ambacho kinatimiza tu mahitaji yake na familia bila akiba ama akiba kiasi)/mkulima na wafanya biashara wadogo wadogo. Take note wale ambao wanaishi maisha ambayo ni ya kubahatisha kama machokoraa hawapo inclusive. Hayo ndio maoni yangu... naomba mtoa mada unipe perspective yako.
 
ni yule anayeshindia mihogo ya kuchoma, ngisi na pweza wa stendi ya daladala, miguu na utumbo wa kuku wa kukaanga, halafu kesho yake hajui ataamka vipi
 
Back
Top Bottom