MWANANCHI LAUZWA NA DAMU ZA WATU i | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MWANANCHI LAUZWA NA DAMU ZA WATU i

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngurdoto, Oct 26, 2012.

 1. n

  ngurdoto Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugu wanajamvi; Leo nimepata taarifa za gari la kusambaza magazeti kwenda Kanda ya Kaskazini mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuwa limepata ajari wilayani Same likielekea Arusha. Nyuma ya gari hilo kulikuwa na abiria ambao kwa taarifa nilizipata wamefariki watu wawili na dereva wa gari hilo.

  Kutokana na aina ya ajari abiria walikuwa nyuma walivuja damu nyingi na kusababisha mzigo zote wa magazeti kutapakaa damu. Cha ajabu mzigo huo wa magazeti umesafirishwa hivi hivi na damu za maiti mpaka Arusha kisha kusambazwa mitaani kwa ajili ya kuuzwa.

  Jamani hii mbona ni hatari kuuza Gazeti zikiwa na damu za watu? Naomba kuwasilisha huku nikitanguliza pole na maombi yangi kwa Mungu kwa ndugu wa marehemu wote waliokuwa kwenye ajari hiyo.
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  we umenunua na kushuhudia??
   
 3. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Nawapa pole wote waliofikwa na misiba !
  Mungu atawasaidia na kuwafariji.
   
 4. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Kweli bana! Aisee ila jamaa wanakuwaga speed sana

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 5. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani haya magari ya magazeti mwendo yanayotembea sio kabisa...halafu imekuwa ni kawaida kwao kujaza abiria RIP waliokufa na Majeruhi poleni. Wewe ulonunua gazeti "chafu" shauri yako kwani huna macho?
   
 6. J

  John W. Mlacha Verified User

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  tamaa ya pesa mbaya
   
 7. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Kama Mbeya vile, unapigwa nondo ya kichwa ili damu ivujie kwenye nondo wakaitumie kutundikia nyama buchani. Kwa siku unauza nyama za ng'ombe kumi+.

  Hiyo ni biashara na miiko yake.
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Aweke picha hapa!
   
 9. j

  jail JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  je kuna anayeweza thibitisha hili?nani kanunua gazeti na kukuta limelowa damu?
   
 10. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hiii ni ajali kama ajali nyingine. Kuuza magazeti hayo ni sawa kabisa ila kunachumvi hapa kwamba eti yameuzwa yakiwa na damu huu ni uongo. Tupigie gazeti lenye damu likiwa pamoja na magazeti mengine kama ni kweli. Haya magari tunaomba wenyewe abiria kutokana na haraka zetu. Mimi nilishawahi panda gari la posta mnapangwa kule nyuma kama magunia. Ila kutokana na mazingira niliyokuwa nayo ilinibidi nipande tu.
   
 11. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Unfortunately Business has no humanity.
   
 12. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  asituletee umbea wa kimasai! jina lake lenyewe la kifisadi
   
 13. M

  Mtoto wa tembo Senior Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haina maana yoyote,usiingize imani za ajabu humu.wewe kama unaogopa damu na unadamu utakua *****,acheni ulimbukeni kwahiyo ajali zote ni ushirikina.peleka upuuzi wako mbali ya jf.
   
 14. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Naomba nieleweshwe hapo, wanajaza abiria na majeruhi? Hao majeruhi huwa wanatolewa wapi?
   
 15. baba junior

  baba junior Senior Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  amesema kapata taarifa.sasa picha ya nini tena?
   
 16. s

  solokela Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toa ushahidi wa picha ya gazet lililo loa damu
   
 17. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  N.B: PICHA HII HAIHUSIANI NA HABARI HII

  Nataka kuuliza wana JF:

  ... hivi haya magari kwa nini huwa wanayakimbiza hivyo?!

  Je? huwa yana ruhusa ya kuvunja amri za Barabani? ... kama high Speed na kadhalika? ...

  Je? ... huwa wanasimamishwa na Trafiki kuhusiana na Over-speeding?

  Vipi kuhusu Takwimu za ajali? ... je huwa yanapata ajali mara kwa mara au vipi? ... maana ukikutana nalo njiani ni hatari!!

  Mwenye uzoefu na hili naomba watujuze zaidi

  adakiss23 . Mkirua . Mpitagwa .
  [​IMG]

  N.B: PICHA HII HAIHUSIANI NA HABARI HII​
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135


  Hahahahaaaa...Mkuu Jabulani...it was a slip of the tongue...Kina Mulugo tupo wengi...LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mandown

  Mandown JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 1,577
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  mimi naona ni sahihhi, msiba umetoke na riziki lazima itafutwe sasa. Ndio maana ni gazeti bora kuliko mengine, wafanye nini na wa shakula hela za matangozo na kumuhaikishia mteja wamba wanafika huko. Kama ni kweli BIG UP MWANANCH
   
 20. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu Dotworld, Ni kwanini wanakimbia ni vigumu kujua. Nadhani kwakuwa huchelewa sana kuondoka ...kutegemea gazeti limetoka saa ngapi may be saa tano usiku au baada ya hapo then wafanye packing wapambane na foleni ya kimara sasa kuliwahisha Arusha asubuhi na mapema nadhani ndipo changamoto zinapoanzia hapo..

  Kwamba yana ruhusa kuvunja sheria ni waji jibu ni hapana kwani hakuna aliye juu ya sheria.
  Kuhusu kusimamishwa na traffick ni vigumu kwani huwa yanasafiri usiku....

  Takwimu za ajali sina ila nadhani zingekuwa kubwa tungezisikia ila nadhani hiki kisiwe kigezo kwani ukweli utabaki kuwa Mwendokasi ni Hatari na unaua hata kama unafanya hivyo miaka yote na hujafanikiwa kufa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...