Mwananchi lasimamisha kesi ya tuhuma za ufisadi N

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Mwananchi lasimamisha kesi ya tuhuma za ufisadi NBC Send to a friend Tuesday, 15 February 2011 20:46

mwananch.jpg
James Magai
HABARI iliyoandikwa na gazeti hili juzi kuhusu tuhuma za ufisadi wa Sh31 bilioni ndani ya Benki ya NBC 97 Ltd, imemtikisa wakili anayeiwakilisha kesi hiyo ,Dk Wilbert Kapinga ambaye ameamua kumkataa mshauri wa Mahakama ambaye ni mwandishi wa Mwananchi, Sadick Mtulya.

Wakili huyo alimkataa Mtulya kushiriki mwenendo wa kesi hiyo jana wakati ilipoitwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Katika kesi hiyo ya madai namba 236 ya mwaka 2003, Mwenyekiti wa NCCR–Mageuzi ,James Mbatia anaidai NBC fidia ya Sh5 bilioni kwa madai ya kudhalilishwa na benki hiyo kwa kumuita mbumbumbu asiyejua mambo ya kibenki.

Mbatia anadai benki hiyo ilimtukana hivyo, baada ya kuanika kile alichodai ufisadi katika uuzwaji wake kwa Kampuni ya ABSA kutoka Afrika Kusini mwaka 2000.

Mtulya alikuwa ni mmoja wa washauri wa Mahakama walioteuliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi hiyo ambayo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana ambapo mlalamikaji (Mbatia), alitarajiwa kutoa ushahidi wa tuhuma zake kwa benki hiyo.

Lakini, kabla ya kuanza kusikilizwa, pande zote zilikubaliana mambo ya msingi katika kesi hiyo na ndipo wakili wa Mbatia, Dk Sengondo Mvungi alipoitaarifu Mahakama kuwa wako tayari kuanza kutoa ushahidi na kwamba tayari kuna washauri wa mahakama walioteuliwa na mahakama hiyo.

Hofu ya wakili Kapinga wa NBC iliibuka ghafla mara baada ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Imani Aboud kuwataka washauri hao wajitambulishe.

Baada ya Mtulya kujitambulisha kwa jina na chombo cha habari anachofanyia kazi, Dk Kapinga alishtuka na kumwekea pingamizi.

Uamuzi wa wakili huyo kumwekea pingamizi Mtulya ulitokana na habari iliyochapishwa na Mwananchi juzi ikielezea kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ikiwa na kichwa cha habari, “Tuhuma ufisadi Sh 31bilioni za NBC kulipuliwa”.

“Kama kuna mtu wa Mwananchi nina Serious Objection (pingamizi zito),” alidai Dk Kapinga baada ya Jaji Aboud kuuliza kama kuna upande wowote wenye pingamizi dhidi ya washauri hao.

“Kuna habari ambayo gazeti hili limei-publish (limeichapisha) tena linainadi kwa bango kubwa tu kuhusu kesi hii kwani imeandika mambo ambayo bado hayajazungumzwa hapa,” alisema Dk Kapinga huku akimwonesha Jaji Aboud gazeti hilo.

“Kwani haya yaliyoandikwa hapa yanahusiana na kesi hii? Huyu si ameandika tu ili kuuza story?” alihoji Jaji Aboud huku akiiangalia habari hiyo.

“Mheshimiwa Jaji ukiendelea huko mbele naona kama inahusiana kwani imemtaja hata Plaintiff (mlalamikaji) humo ndani. Kwa hiyo naona huyu asihusike kwani si vema kuwa mshauri wakati tayari limeshaanza kuandika kwa angle hiyo,” alisisitiza Dk Kapinga.

Jaji Aboud baada ya kuipitia habari hiyo kwa ufupi alimuuliza Dk Mvungi kama alikuwa na lolote la kusema kuhusiana na pingamizi hilo la Dk Kapinga, naye akasema hana.

“Kama mwenzangu anaona si vema kuwa na mshauri huyo sawa, Mahakama inaweza kumtafuta mwingine wa kuziba nafasi hii maana ninaamini inayo orodha kubwa tu ya washauri wanaoweza kusimamia kesi hii,” alijibu Dk Mvungi.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Aboud alikubaliana na pingamizi hilo na kuridhia Mtulya aondolewe katika orodha ya washauri hao ili atafutwe mwingine.

Kutokana na kuondolewa kwa Mtulya katika orodha ya washauri wa Mahakama katika kesi hiyo, kesi hiyo ilishindikana kuendelea kusikilizwa jana na hivyo kuahirishwa hadi Machi 16 na baadaye Machi 21 mwaka huu, ili kutoa nafasi kwa Mahakama kumteua mshauri mwingine badala ya Mtulya.

Kabla ya kesi hiyo kuahirishwa, Dk Mvungi aliieleza Mahakama kuwa anatarajia kuwa na mashahidi wanne katika kesi hiyo na kwamba shahidi wa kwanza ni Mbatia ambaye pia ni mlalamikaji alikuwa tayari kuanza kutoa ushahidi wake.

Juzi Mbatia alilieleza Mwananchi kuwa anazo nyaraka za kutosha kuthibitisha tuhuma zake za ufisadi katika ubinafsishaji wa benki hiyo ambazo atazitoa mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake.

Jana baada ya kesi hiyo kuahirishwa Mbatia aliliambia Mwananchi nje ya Mahakama kwamba amejiandaa vema kufyatua vielelezo kimoja baada ya kingine kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya benki hiyo na kwamba ataonesha jinsi fedha hizo zilivyopotea Septemba 2 mwaka 2003.

Katika kesi ya msingi, NBC ilimshtaki Mbatia ikimdai fidia ya Dola za Kimarekani 1milioni kwa madai ya kuitukana na kuidhalilisha.

Mashtaka hayo yalitokana na tuhuma za Mbatia dhidi ya benki hiyo alizozitoa katika mkutano wake na waandishi wa habari Septemba 16 mwaka 2003.

Katika mkutano huo, Mbatia alidai kuwa kuna wizi na ufisadi katika mchakato wa uuzwaji wa benki hiyo kwa Kampuni hiyo ya ABSA na kwamba benki hiyo haiendeshwi kwa maslahi ya umma kutokana na utawala mbovu wa kampuni hiyo.

Mbatia alihoji uhalali wa kuuzwa kwa Sh 15 bilioni huku muda mfupi baadaye duru huru za kiuchunguzi zikionyesha katika tawi moja pekee la Samora, ilikuwa na deni la sh 31 bilioni.

Mbali na kutoa madai hayo kwa vyombo vya habari, Mbatia pia alimpelekea tuhuma hizo Rais Benjamin Mkapa ili azifanyie kazi.

Lakini siku moja baada ya Mbatia kurusha tuhuma hizo, NBC nayo ilimjibu Mbatia kuwa ni mbumbumbu akisiyejua mambo ya kibenki.

Kama vile haitoshi, ilimpelekea taarifa ya kumtaka ailipe fidia ya Dola hizo za Kimarekani 1milioni, kwa madai ya kuitukana, lakini Mbatia akakataa ndipo wakamfungulia kesi mahakamani.

Baada ya kumfuingulia kesi hiyo, Mbatia naye akaifungulia kesi kinzani dhidi ya benki hiyo akiidai fidia ya Sh5 bilioni kwa madai ya kumdhalilisha kwa kumtukana kuwa ni mbumbumbu.

Hata hivyo, kesi ya NBC ilitupiliwa mbali na Jaji Aboud mwaka 2007 na kuendelea na kesi kinzani.

Awali NBC waliwahi kumuomba Mbatia wapatane nje ya Mahakama, ingawa Mbatia alikubaliana na ombi hilo, lakini hawakufikia mwafaka baada ya NBC kukataa kumlipa fidia hiyo na ndipo kesi hiyo iliporudi tena mahakamani hapo.
 
PHP:

Veri interesting kuona kesi mama inatupwa lakini kesi kinzani inaamuliwa iendelee.................i very much doubt that justice will very served there.....................
 
Back
Top Bottom