Mwananchi Communications Limited, mna shida gani siku hizi?

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Nimekua mfuatiliaji mkubwa sana wa Magazeti yenu,hasa Mwananchi na Mwanaspoti! Toka Mkurugenzi wenu akiwa Mzee Tido Mhando Master mind himself.

Siku za hivi karibuni mmekua mnatoa habari za hovyo hovyo kweli,kwanza sio zile habari za kiuchambuzi, mmekua watu wa kusifu sana! Mbili makosa ya uandishi yamekua kama mtoto anajifunza aeiou, mnakera sana.

Katika Gazeti lenu la Jumamosi la Mwanaspoti la tarehe 20.02.202, imenibidi nicheke kwa sauti tu! Hivi kweli Luis Suárez anacheza EPL?? Kylian Mbape anacheza Serie A?? Maana yake mnataka kusema Ligi kuu ya Hispania ni EPL na Ligi kuu ya Ufaransa ni Serie A?

Hamuoni kama munapoteza mashabiki zenu bila nyie kujua?

Leo tena kwenye Gazeti lenu la Mwananchi tarehe 21.02.2021,eti Dr Servasius Likwelile amefariki tarehe 19.01.2021 hivi kumbe alifariki zamani,lakini taarifa ndiyo zimetoka Jana? Mbona mnakua mnakosa weledi wakutulisha sisi walaji?

Hivi mauzo yenu bado yapo juu kama kipindi kile cha Mzee Tido Mhando?? Au na nyie mnataka kufunga ofisi zenu kama Habari Corporation??

Msije tafuta wachawi mbele ya safari, wachawi ni nyinyi wenyewe.

IMG_20210221_121137_064.jpg
IMG_20210221_121017_464.jpg
 
Mwanaspoti tangu aondoke Frank Kipambe Sanga kutimkia Azam pamebaki pa kawaida sana. Machumu ajitafakari.

Na wanapaswa kuajiri Ombudsman ili awasaidie checks and balance maana sio errors hizo na ni kote hata Citizen errors nyingi
 
Siku hizi ukitaka habari za uhakika na za ukweli zisizo ogopa Wala kuabudu jiunge na Kigogo kule Twitter Tena kwa gharama ndoooogo sana.
Kila slowslow analowaza hata kabla hajakwea Viieite sisi tunakua tumelinyaka
 
Back
Top Bottom