Mwananchi afukuzwa kijijini kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni chuma ulete

mwaminifuhalisi

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
329
416
Wakati tukiwa katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia, bado imani za kishirikina zimeendelea kuchukua nafasi kubwa kwani wananchi wa kijiji cha Ilasilo wilayani Songwe kwenye mkutano uliohudhuriwa na mwenyekiti na polisi wamemfurusha mwanakijiji mwenzao kwa tuhuma za kujihusisha na kazi ya chuma ulete hivyo amefanya kijiji chao kuwa na maendeleo duni tofauti na vijiji vingine vya jirani na kuchukuliwa na polisi kupelekwa kituoni.

Aidha mwananchi aliyetimuliwa alipinga kujihusisha na madai yanatolewa juu yake na kumwaga machozi na kuwa tayari kuondoka kwa sababu wanakijiji wenzake hawamuhitaji.

Inasikitisha sana kuona mpaka miaka hii watu bado kuendelea kuwa na imani za kipuuzi namna hii.
Chanzo: Ebony FM.
 
Watu hawajihangaishi maisha bora yatatoka wapi?
Natamani nijue miaka kadhaa ijayo baada ya jamaa kuondoka watukua wamefikia wapi kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom