HahaaaPenye penzi hapakosi tenzi, wakale walisema na huwezi kula muwa bila kukuta fundo. Huu wimbo unaniacha hoi saana. Wewe utakua mpenzi wa msondo mwenzangu. Najua utakua unakunywa safari na Ni mshabiki wa timu kongwe. Dar es Salaam Young Africans.
Sio kweli mkuu jamaa umri ulienda sana pia feg na konyagi alipiga sana nilimuona last timu pale dar safari pak buza
Hao ndo walikuwa wanamuziki, hawa wengine ni wasanii.Mzizi Mkuu wa Bendi nzima ndiyo umeshaondoka hivyo na sina tu uhakika tena kama waliobakia wataisimamisha Msondo kama hawa Walioondoka.
KISUMA ya mbagala kuna wauza firigisi wengi sana pale usiku nazani wamehama toka kona barKumbe wewe ni Mdau mwenzangu wa Kisuma siku ya Alhamis?
AiseeeTimu imekamilika, ingekuwa inawezekana wangeenda anzisha bendi huko walipo, R.I.P
Wapi hapo?Apumzke anakostahili
Dah. Aisee wewe bado dogo sana.Nilivyokuwa mdogo nlikua naskia wimbo unaimbwa "Mabeee mabee mabela" daah RIP
Da....nimesikitika sana kuondoka kwa gwiji la muziki ujanani mwangu.Gwiji wa muziki wa dansi na Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 29, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni nyumbani kwake Goba.
Msiba upo Nyumbani kwake Tegeta A maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam.
===
SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA
GWIJI wa ukung'utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia jana saa 6 za usiku.
Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.
Mtoto wa marehemu, Mabera Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.
RIP maberaMpiga solo mkongwe wa bendi ya msondo ngoma mzee Saidi Mabele ameaga dunia usiku wa kuamkia leo kwa kinacho daiwa kuwa ni mshtuko wa moyo.Habari nyingine zaidi zitafwatia baadae.R.I.P.
Firigisi za kuku na hata za bata huku pia zinauzwa kuanzia muda ya jioni..KISUMA ya mbagala kuna wauza firigisi wengi sana pale usiku nazani wamehama toka kona bar
Ni Kisuma ya Mwembe Yanga,kila Alhamis.KISUMA ya mbagala kuna wauza firigisi wengi sana pale usiku nazani wamehama toka kona bar