Mwanamume ang'atwa na kichwa cha nyoka Texas, Marekani

Mwanamume ang'atwa na kichwa cha nyoka Texas, Marekani

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Mwanamume mmoja katika jimbo ya Texas, Marekani nusura afe baada ya kuumwa na kichwa cha nyoka ambaye alikuwa amemkata na kumuua.

Jennifer Sutcliffe ameambia kituo cha runinga cha KIII-TV kwamba mumewe alikuwa akifanya kazi shambani pale alipomuona nyoka huyo wa urefu wa futi nne (1.25m) na kumkata kichwa kwa upanga.

Nyoka huyo alikuwa aina ya nyoka atoae sauti ya kuchacharika kwa mkia wake, maarufu kwa Kiingereza kama rattlesnake.

Alipouchukua mzoga wa nyoka huyo akautupe, kichwa cha nyoka huyo kilimuuma.

Ililazimu madaktari kumdunga sindano ya vipimo 26 vya dawa ya kuua sumu kumuokoa.

Nyoka akiguswa anaweza kumuuma mtu saa kadha kabla ya nyoka huyo kufa.

Bi Sutcliffe ameambia KIII-TV kwamba mumewe alianza kupapatika ghafla.

Alisafirishwa kwa ndege hadi kwenye hospitali iliyo karibu na Corpus Christi ambapo alitibiwa kwa dawa ya kuua sumu aina ya CroFab.

Wiki moja baada ya kisa hicho, mwanamume huyo anadaiwa kuwa katika hali nzuri hospitalini, ingawa figo zake bado ni dhaifu.

Leslie Boyer, ambaye ni daktari wa kukabiliana na sumu ya nyoka katika taasisi ya VIPER ya chuo kikuu cha Arizona amewatahadharisha watu dhidi ya kujaribu kuwaua nyoka, hasa kwa kuwakata kata.

"Ni ukatili dhidi ya wanyama hao na hukuacha na vipande vingi vyenye sumu ambavyo unahitaji kuviokota," aliambia tovuti ya Gizmodo.
BBC
 
Angekufaje wakati bongo tunafata maandiko ya kibiblia nyoka lazima apondwe kichwa yeye kampiga tumboni tena kindezi shusha bonge ya jiwe mpka kichwa chake kizame ardhini
Ni kweli mkuu maana Kama kichwa hakita pondwa hudhuru pia ,kinaweza kuota tena Kama mkia wa mjusi unapo katika huota
 
Back
Top Bottom