Mama hamtaki Mpenzi wangu

princess ariana

JF-Expert Member
Aug 19, 2016
7,553
14,383
Habari za saa hii wana Jf

Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • Mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-Wote tumeishia 0- level kielimu
-Anataka kunioa pale nikiridhia

Sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-Ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- Aliwahi kuishi na mwanamke
-Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- Hana mvuto mbele za watu
-Hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- Anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-Kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-Hana hadhi ya kuwa na mimi

Sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa

- Mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? Maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! Kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...

Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...

Nimepata feeling mama yangu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..

Maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? Nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.
 
Pole sana Mkuu

Isingekuwa heshima zetu kwa Wazazi ungeweza kumuuliza Bi Mkubwa kama nayeye alichaguliwa kuwa na Mzee wako au walipendana wenyewe 🤔

Anyways, Wanasema Wazazi wamewahi kuona jua kabla yetu, jaribu kumsikiliza pengine kuna jambo ameona kwa huyo Boyfriend wako
 
Habari za saa hii wana Jf
Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-wote tumeishia 0- level kielimu
-anataka kunioa pale nikiridhia

sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- aliwahi kuishi na mwanamke
-anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- hana mvuto mbele za watu
-hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-hana hadhi ya kuwa na mimi
sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa
- mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...
Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...
nmepata feeling mama angu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..
maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.
Duh humu ni bora kuliko mama mzazi aliyekuzaa mzazi hawezi kumdanganya mwanae. Kaa chini na mama yako muyajenge sio mtandaoni
 
Hata mimi nisingekuozesha yaani mwanaume an a kunywa pombe, bangi ,sigara mie hapana wanakuaga malaya mno

Afu pia wewe umeishia olevel na yeye olevel watoto wenu nani atawafundisha? Tafta hata mkaka mwenye diploma mtoto enu awe inspired kusoma kwa bidii

Usitangulize hisia mbelembele
 
Maisha ni vile unataka wewe na sio mama wala baba yako! Ingawa pia ni muhimu kupima kila ushauri unaopewa na wazazi!
Je kwa sasa kijana anafanya kazi gani? Pia kiwango chake cha ulevi ni kiasi gani ( mind you ulevi una addiction)
Kuhusu mama yako, je yeye ana kijana wa kiume? Na kama ndiyo je kaka yako na huyo mchumba wako nani ana mafanikio zaidi?
Au yeye mama yako alichaguliwa wa kumuoa I mean baba yako?
Wapo Vijana wengi hawakuwa na kitu mwanzoni lakini kwa kutumia akili, maarifa na kujituma leo wapo mbali sana kimaisha.
 
D8264023-08B5-43E4-8710-E51F859EB127.jpeg

Pole sana mkuu
 
usimpuuze mama ana hoja,hasa kwenye kuvuta bangi na pombe kama ni kweli
Na hivyo vitu sio kivile, pombe ameacha tangu nimwambie mi pia staki hivyo vitu akishindwa kuacha tutakua tu casual amenielewa anayafanyia kazi hayo
Pole sana Mkuu

Isingekuwa heshima zetu kwa Wazazi ungeweza kumuuliza Bi Mkubwa kama nayeye alichaguliwa kuwa na Mzee wako au walipendana wenyewe 🤔

Anyways, Wanasema Wazazi wamewahi kuona jua kabla yetu, jaribu kumsikiliza pengine kuna jambo ameona kwa huyo Boyfriend wako
ukimuuliza anasema umemtukana
 
Maisha ni vile unataka wewe na sio mama wala baba yako! Ingawa pia ni muhimu kupima kila ushauri unaopewa na wazazi!
Je kwa sasa kijana anafanya kazi gani? Pia kiwango chake cha ulevi ni kiasi gani ( mind you ulevi una addiction)
Kuhusu mama yako, je yeye ana kijana wa kiume? Na kama ndiyo je kaka yako na huyo mchumba wako nani ana mafanikio zaidi?
Au yeye mama yako alichaguliwa wa kumuoa I mean baba yako?
Wapo Vijana wengi hawakuwa na kitu mwanzoni lakini kwa kutumia akili, maarifa na kujituma leo wapo mbali sana kimaisha.
kwasasa ni kama ameacha tangu nimkataze hajanywa na wala hakua mlevi ivyo ni mnywaji tu
- mama hakuchaguliwa baba
-ninae kaka angu ila hamfikii wa lolote kwenye kujituma mpaka maendeleo huyu jamaa yuko mbele sana
jamaa yeye amesema tumpe muda ajithibitishe kuwa ni sahihi na anajitahidi ila mama hamtaki
mpaka biashara anataka kunifungulia ila mama hataki
 
Back
Top Bottom