Mwanamke wangu kaninunia baada ya kumwambia anakosea

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Ndugu zangu wanaJF, naombeni ushauri wenu.

Nina mwanamke wangu nampenda sana na ninamuelewa kwa tabia zake za uvumilivu,heshima kwa ndugu zangu, nikikosea hata nikikosea huwa mwepesi kunikosoa wapi nakosea huwa anaelekeza kwa kifupi ni mwanamke anajitambua kwa kweli nampenda mnoo,

Ila shida inayokuja saivi ameamua kuninunia nikimtumia meseji saa nyingine anajibu short cut na saa nyingine hanijibu kabisa hata kuonana na Mimi hataki tuzungumze yaishe na chanzo cha yeye na mimi kutoelewana ni simu alinipigia sikupokei ilikuwa chaji nilivyokuja kumpigia alinifokea sana na kuanzia kulalamika akajua simu sikupokea makusudi siku ya pili nilimpigia simu kumuelezea sikupendezwa na ile hali ya juzi alichofanya sio sahihi kunifanyia vilee

Basi amenikasirikia hataki kuongea na Mimi kwa kifupi kaninunia kila nikijaribu kujirudi basi arudishe moyo wake kama zamani lakini wapiii

Naombeni ushauri mimi kwa kweli sijisikii vizuli anavyonifanyiaaaa
 
Tafuta mwanamke wa pili.

Mwanaume ukiwa na mwanamke mmoja ndio huja na mambo ya kitoto kama haya.

Swali lako ni kama mwanaume ambaye Mke wake kajifungua na yupo kipindi cha uzazi. Alafu unaomba ushauri kwa wanaume kuwa unahamu ya kusex alafu mkeo ni yupo kwenye uzazi.

Unaigopwa kununiwa, mbona bado hujakomaa. Wanawake kwa kununa ndio tabia zao.
Akinuna achana naye, Fanya mambo mengine.
 
As you're a man..... .though itakua ngumu kwako kwa jinsi ulivyo muelewa Ila JARIBU TU...mchunie kwa mtindo wa kum blacklist kwa muda usio julikana..atakutafuta tu nakukuuliza ndo na we umeamua kumkatili kabisa?...keep that in yo mind ukimtumia text na calls nyingi yy ndo anafurahi kwa kujua kweli unampenda...fanya kama ume give up to apologize..with assuarance akiona 5+days zinapita bila kum tafuta atasumbuka yeye kukutafuta. Endelea na mitikasi2 she'll regret
 
Huwa tuna mood swings ukilielewa hilo walaa hupati taabu na sisi. Fanya kama nawe unamuignore hivi, kama ni mood swing kweli atajirudi ila kama anakutafutia sababu ujue ndio imetoka hivyo.
Asipokuelewa hapa basi haji kuelewa kitu maishani mwake
 
Ndugu zangu wanaJF, naombeni ushauri wenu.

Nina mwanamke wangu nampenda sana na ninamuelewa kwa tabia zake za uvumilivu,heshima kwa ndugu zangu, nikikosea hata nikikosea huwa mwepesi kunikosoa wapi nakosea huwa anaelekeza kwa kifupi ni mwanamke anajitambua kwa kweli nampenda mnoo,

Ila shida inayokuja saivi ameamua kuninunia nikimtumia meseji saa nyingine anajibu short cut na saa nyingine hanijibu kabisa hata kuonana na Mimi hataki tuzungumze yaishe na chanzo cha yeye na mimi kutoelewana ni simu alinipigia sikupokei ilikuwa chaji nilivyokuja kumpigia alinifokea sana na kuanzia kulalamika akajua simu sikupokea makusudi siku ya pili nilimpigia simu kumuelezea sikupendezwa na ile hali ya juzi alichofanya sio sahihi kunifanyia vilee

Basi amenikasirikia hataki kuongea na Mimi kwa kifupi kaninunia kila nikijaribu kujirudi basi arudishe moyo wake kama zamani lakini wapiii

Naombeni ushauri mimi kwa kweli sijisikii vizuli anavyonifanyiaaaa
Ishi bila yeye, upendo kwake umeisha usimlazimishe. hata kama unampenda lakin yeye hakupend tena.....kuwa mwamba asikuyumbishe bhn
 
Back
Top Bottom