Scott junior
JF-Expert Member
- Mar 24, 2022
- 2,391
- 3,155
habari zenu wakuu...aisee Mimi napitia wakati mgumu sana nilikuwa Nina mpenzi wangu tumezaa naye mtoto mmoja na kwao tayari nilishajitambulisha japo Bado sijatimiza sharti la mahari.
Ni hivi huyo ndiye mwanamke wangu wa kwanza kuwa naye serious kwenye mahusiano katika maisha yangu na Mimi ndiye mwanaume wake WA kwanza kwenye suala la mapenzi.
Tatizo ni kwamba nimeanza kuishi naye wakati nimetoka chuo na hivyo sikuwa nimejipata kimaisha japo yeye alikuwa ana vibiashara vyake vidogo vidogo vinamuingizia kipato.
Kwahiyo ikawa rahisi sisi kuishi pamoja baada ya kumpa mimba, mtoto wetu hivi Sasa ana miaka miwili na nusu na hivi karibuni maisha yameniendea kombo sana kiasi kwamba huduma zote za nyumbani nikawa kama namtegemea yeye.
Hali iliyopelekea yeye kunambia kuwa amechoka anaomba nimpishe na mtoto kwa muda, japo sikuondoka lakini kauli hiyo ilinichanganya sana akili na kunipa mawazo kiasi kwamba nikajikuta natumbukia kwenye ulevi.
Siku Moja nilimkuta amesimama na mwanaume aisee na nilikuwa nimelewa hivyo sikujipa muda wa kutafakari ikapelekea nimpige kibao mpaka wazazi wake yaani baba ake akaja kumchukua namimi ikabidi nirudi kwetu kwa muda kupumzisha akili.
Sasa ni hivi kesho yake baada ya kurudi kwangu nikakuta ameniwekea mizigo yangu yote nje akimaanisha haitaji tena kuishi na mimi, aisee nliondoka lakini baadae nimeanza kumtafuta kumuomba msamaha kanikataa kata kata na kunitishia nikiendelea kumsumbua ataniblock na nisisikie kabisa kuhusu mwanangu tena.
Naombeni ushauri kwakweli roho inaniuma sana sikuwa tayari kuipoteza familia yangu kwa wakati huu nampenda sana mwanamke wangu pamoka na mwanangu siku ya tatu Leo nakosa usingizi mawazo yamenijaa Sina Raha ya kuishi kabisa.
MEMBER MWENZETU ANAOMBA USHAURI
KUTOKA WANAUME UNION.
naamini atapata ushauri sahihi wakuu.