Mwanamke wa mjini na kijijini yupi anafaa kuoa?

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Habari za j2 wana jamvi ktk tafakari yangu ya leo nimejiuliza ili mwanaume kufika aumuzi wa kuoa ni bora angeenda kijijini kuoa au ni bora aoe mjini nikidhani either upande mmoja kati ya mjini au vijijini wanawake sio tegemezi na wana true love na kujituma ktk kutafuta. Swali wapi bora?

Nawakilisha
 
Anaefaa ni mwanamke........hakuna cha wa kijijini wala mjini, kwani huyo wa kijijini ukishamleta mjini atabakia kuwa wa kijijini tu?

Usiombe jogoo lililochelewa kuwika likajua ghafla kuwaika, litawika kuzidi majogoo yote tena bila kujali wakati, lenyewe litawika tuuuuuuuu
 
song:nikusaidiaje
bY.Prof jay.

Umesahau ulipotoka, hujui unapokwenda
Ukapata kiburi kuona mi nakupenda
Nilikuthamini na letu penzi kulienzi
Na leo siamini kama umenisaliti mpenzi
Kumbuka nilikukuta kijijini sitimbi
Umebeba mahindi na furushi la maimbi Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji
Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitaji
Kigoli mwenye umbo kama la mdori
Wala sikutaraji ungepiga nami stori
Nilifurahi kuweza kukufahamu
Na nikakuahidi subiri zangu salamu Kwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi
Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi
Wote walishangaa kusikia namtaka mchumba
Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumba
Wakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa
Niliapa kujua iwapo ningekukosa Walinikabidhi nirudi nawe mjini
Na nikakusisitiza mjini kuwa makini....
 
Da siku hizi wote wamejanjaruka,wote wanaangaria pakeeeeee yeyote anafaaa kuoa ili mradi umeridhika nae period
 
Tabia ya mtu haitegemei ni wa mjini au kijijini. Kote kote unaweza kuoa ili mradi tabia yake imekuridhisha. Ila ukipata mwenye tabia njema mjini ni bora zaidi maana yule wa kijijini tabia yake inaweza change pindi atakapoingia mjini.
 
Nimedhani wa mjini ni mtu wa starehe na matumizi mengi zaidi ya kijiji sijui kama fikra yangu imekuwa sahihi au la?
 
Habari za j2 wana jamvi ktk tafakari yangu ya leo nimejiuliza ili mwanaume kufika aumuzi wa kuoa ni bora angeenda kijijini kuoa au ni bora aoe mjini nikidhani either upande mmoja kati ya mjini au vijijini wanawake sio tegemezi na wana true love na kujituma ktk kutafuta. Swali wapi bora?

Nawakilisha
Sidhani kama 'ukijijini' au 'umjini' ni kati ya sifa za mwanamke
 
Nimedhani wa mjini ni mtu wa starehe na matumizi mengi zaidi ya kijiji sijui kama fikra yangu imekuwa sahihi au la?

Unafikiri wanawake wote walioko mijini walizaliwa na kukulia mijini? Unaweza ukamleta mwanamke kijijini na baada ya muda mfupi nae akaendekeza starehe na matumizi mengi. BTW kuna mwanamke gani (whether mjini au kijijini) asiyependa starehe na matumizi? All women want to have fun.

Omba Mods Mods wahamishie uzi wako jukwaa la MMU.
 
Habari za j2 wana jamvi ktk tafakari yangu ya leo nimejiuliza ili mwanaume kufika aumuzi wa kuoa ni bora angeenda kijijini kuoa au ni bora aoe mjini nikidhani either upande mmoja kati ya mjini au vijijini wanawake sio tegemezi na wana true love na kujituma ktk kutafuta. Swali wapi bora?

Nawakilisha

Hizi hadithi za kwenye 70s kumbe bado zipo! Umenikumbusha ule wimbo ni mwokoe nani kati ya mke, mwana na mama? mkuu inakubidi ubadilike ili uendane na hii karne ya 21. Kwenye hii karne mtu mke na mtu mme wote sawa sawa. Unachotakiwa ni wewe kujiuliza una ubora gani na unahitaji mke mwenye ubora gani ili kupata familia unayoitaka.
 
song:nikusaidiaje
bY.Prof jay.

Umesahau ulipotoka, hujui unapokwenda
Ukapata kiburi kuona mi nakupenda
Nilikuthamini na letu penzi kulienzi
Na leo siamini kama umenisaliti mpenzi
Kumbuka nilikukuta kijijini sitimbi
Umebeba mahindi na furushi la maimbi Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji
Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitaji
Kigoli mwenye umbo kama la mdori
Wala sikutaraji ungepiga nami stori
Nilifurahi kuweza kukufahamu
Na nikakuahidi subiri zangu salamu Kwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi
Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi
Wote walishangaa kusikia namtaka mchumba
Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumba
Wakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa
Niliapa kujua iwapo ningekukosa Walinikabidhi nirudi nawe mjini
Na nikakusisitiza mjini kuwa makini....

malizia mbona umeukata? Nadhan huo wimbo utakuwa ni msaada kwa muomba ushauri. Afadhari ukaoa changu au bamedi.
 
kaka muombe mungu sana usije ukakakosea kuoa,mshirikishe mungu akuchagulie wala si macho yako na tena mlilie sana akuelekeze mke wa koua naamini utapata mke mwema,njia ya kutokea kijijini au mjini si njia ya wewe kumpata mke mwema
 
Back
Top Bottom