kwanza kuliko yote swala la mahali sio la wazazi tu wanalipanga.
Inategemea na madhehebu aliotokea.
Kuna makabila mengine mtoto mwenyewe ndio anapanga mahali.
Kuna makabila mengine baba anapanga mahali.
Na kuna makabila mengine mama ndio anapanga mahali.
Na mengine yule aliekupa jina siku unazaliwa, na wengine yule alie kulea.
Na kuna makabila mengine ukoo mzima unapanga mahali.
So kwanza inabidi ufuatilie madhehebu ya kwao huyo mchumba wako.
Labda kwao anaetaka kuolewa ndio mwenye haki kupanga mahali je?
Watu wanaweza kukuambia mengi, so kuwa makini kabla hauja amua kufanya lolote juu ya mchumba wako.
Kuna watu wanaolewa bila mahali,
Na wengine ujipangia mahali wenyewe,
Na wengine uolewa na mahali kubwa
Na wengine uolewa na mahali ndogo
Na wengine uolewa na mahali nusu.
So usipende kujifananisha na wengine, hayo ni maelewano yako na mchumba wako na wazazi wenu.
Fuatilia madhebu ya kwao, na fuata masharti.
Kama uwezo wako mdogo na yeye anataka mengi muambie hauna uwezo uwo, basi bora musioane, hakika kama anakupenda uwo ushangingi wa vinywaji utamtoka kichwani.
Mwanamke akikupenda kweli unaweza kumuoa bila mahali au mahali ndogo sana.
JUU YA WANAWAKE WA SASA
Wanawake wa sasa wengi wanataka sifa, waoneshe kwa marafiki zao kuwa wameolewa na mahali kubwa, na sherehe kubwa.
Na hata mama zao ndio hivo hivo, uswahili.
Kuna kaka mmoja alisema yeye hataki kuoa, sababu gauni ya harusi laki 2, madhahabu, viatu, saloni na vipambo, anakadilia laki 5 kwa pamoja. matarumbeta, baikoko, taarabu, nk. vyakula na vinywaji.
Anakadilia ni milion 10.
Baada ya miezi sita anadai talaka, kisa uwezo wa kununua gari kama mume wa rafiki yake hauna.
Nawapa pole wanaume.
Mungu akusaidie uoe kwa gharama sahihi na udumu nae ktk ndoa.