Mwanamke ukimfanyia hili anakuwa na furaha sana, hatakuja kugombana na wewe

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".

Wanaume chukueni maarifa hayo.
 
Hata kama unataka kuwa business partner na mtu, mshirikishe make wako wamepewa uwezo Mkubwa wa kujua yupi ni business partner sahihi kwako
 
Lazima ashushe mjengo wa Maana subiri tu kukaribishwa kwake! eti nyumba ya kaka ametupa tuishi kwa muda! mpaka mambo yetu yakiwa mazuri, achana na akina Mosha family.
 
Waungwana natumaini kuwa mu wazima!

Twende kwenye mada, familia nyingi Afrika ziko kwenye mgogoro au kamgogoro, na migogoro hii husababishwa hasa na mambo ya fedha au mapenzi nje ya mahusiano(cheating).

Sasa hapa ninatoa tiba ya mgogoro unaosababishwa na mambo ya kifedha.

Kulingana na kipato chako ewe mwanaume unaweza kuitafuta fedha ambayo kwa level yenu ya maisha itaonekana ni kubwa. Ichukue mpe mkewe atunze, mwambie itunze ninà kazi nayo.

Ukimpa kama milioni 5, 4,3 au hata laki tano akutunzie moyo wake unakuwa mweupe.

Hii style ina faida zake, ikumbukwe wanawake wana forecast nzuri ya kuona jambo zuri ambalo akikushauri ufanye utapata faida kubwa.

Usiwe dictator kwenye masuala ya fedha, kuwa muwazi ingawa usiwe muwazi kupitiliza.
Lakini kuna wanawake wengine unamtunzisha pesa mwisho wa siku tamaa inamjaa anakuibia anasepa, zikiisha anarudi unamsamehe na maisha yanaendelea, je mwanamke kama huyu unamchukuliaje?
 
Hakuna jambo unaloweza kumfanyia binadamu mwenzio ambalo linaweza kumfanya kukupenda, mtu binafsi kama hayupo tayari kukupenda yeye binafsi kwa moyo wake hata umfanyie nini utakuwa unajisumbia tu, moyo wa binadamu ni kichaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binafsi kama nina laki saba nampa laki tano aniwekee mbili nabaki nazo simuambii.

Ikitokea shida na tatizo nyumbani natoa kwenye hizi mbili kimya kimya yeye hajui lolote,kuwasaidia wazazi sio lazima mtu umuambie mkeo wale ni wazazi,sio kils kitu mke ajue aisee.

.yani unamsaidia mzazi pesa ya chai unaenda kumuambia mke "naomba alfu 10 nimtumie maza,kama unawauza wazee hivi na wake zetu walivyo wataona kama wazew watu mzigo hivi aisee.

Mimi lazima nibaki na salio la siri ambalo wife halijui ili kumaliza matatizo ya home kimyakimya,hii inaepusha mke asijekuona kwamba mtu unawasaidia wazee wako tuu.
Wewe huwajui wanawake! Inaonesha hujaoa hata. Mwanamke ukimpa hela atunze, na siku ukawa hujaleta, huo ugomvi Jamaa aliye juu ndiye anajua. Kama unampa zote ukitaka kusaidia ndugu zako, ugomvi sijui nani wa kuuamua. Zikiwa nyingi ataanza 'tumjengee baba yangu kijumba' wakati huo huo wewe ukitaka kutuma hela ya chumvi kwa mama yako kijijini ni msala wa ajabu. Kawaida huwa tunahakikisha wake zetu hawajui ni kiasi gani unapata na kiasi gani kipo MPesa maana Benki hatuna uwezo wa kuwa na account. Hata hela yake ukitaka kuitumia itumie kiakili ila usimuulize anapata kiasi gani na Benki ana kiasi gani. Hapo maisha yanasonga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani umuachie mkeo kazi ya kuforecast mambo ya familia wewe ubaki kukuna kidevu na poumbou ???
Waungwana natumaini kuwa mu wazima!

Twende kwenye mada, familia nyingi Afrika ziko kwenye mgogoro au kamgogoro, na migogoro hii husababishwa hasa na mambo ya fedha au mapenzi nje ya mahusiano(cheating).

Sasa hapa ninatoa tiba ya mgogoro unaosababishwa na mambo ya kifedha.

Kulingana na kipato chako ewe mwanaume unaweza kuitafuta fedha ambayo kwa level yenu ya maisha itaonekana ni kubwa. Ichukue mpe mkewe atunze, mwambie itunze ninà kazi nayo.

Ukimpa kama milioni 5, 4,3 au hata laki tano akutunzie moyo wake unakuwa mweupe.

Hii style ina faida zake, ikumbukwe wanawake wana forecast nzuri ya kuona jambo zuri ambalo akikushauri ufanye utapata faida kubwa.

Usiwe dictator kwenye masuala ya fedha, kuwa muwazi ingawa usiwe muwazi kupitiliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuba msemo unasema "a woman is an incubator"
1. Ukimpa house ana multiply na kuwa home.
2. Ukimpa sperm ana multiply na kukupa mtoto.
3. Ukimpa pesa ana multiply na kukuza kipato

RESPECT TO MOMAN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom