Mwanamke:-Ukijifungua, tulia kwanza, usije jiuwa bure..............

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Kama uchovu na ukosefu wa usingizi ndivyo vinavyowafanya wanawake ambao wamejifungua karibuni kutoshiriki kwenye tendo, hapa kuna sababu nyingine ambayo pengine ni muhimu zaidi.

Ni ipi hiyo?

Sikiliza kwa makini.

Mji wa uzazi wa mwanmke ambaye amejifungua karibuni unakuwa na mishipa ya damu iliyotepeta na mipana. Kwa hiyo anaposhiriki tendo, misukosuko ya jambo hilo huifanya mishipa yake kujaa hewa, hivyo damu kuwa na aina ya povu.

Povu hili linaweza kusababisha damu ya mwanmke kuganda. Kuna ushahidi wa vifo ambavyo vimetokana na tatizo hili kwa wenzetu ambao huweka kumbukumbu za sababu ya vifo. Kwa mfano huko Uingereza wanawake 18 walipoteza maisha kati ya mwaka 1967 hadi 1994.

Kwa hiyo baada ya kujifungua inabidi mwanamke asahau kidogo jambo hili kwa sababu kama ni upendo utaendelea kuwepo tu na mume hawezi kutoka nje kwa sababu yeye (mwanamke) analea. Labda tu kama upendo haupo.
 
Asahau kwa muda gani...
 
seriously!!!???? one whole year???? one whole year with no sex????? unafanya utani eti eh? how is that even possible?
 
Na wewe MTAMBUZI ushaidi wa Uiengereza tupe na wa Tanzania
Tanzania hatuwekagi kumbukumbu za vifo.........Mara nyingi mtu akifa kumbukumbu inayowekwa ni kwamba ALIROGWA....................

Niliwahi kutembelea Hospitali moja ya wilaya fulani na kumuuliza Daktari mkuu kama anayo kumbukumbu za vifo vya watoto usingizini kitaalamu huitwa Sudden infant death syndrome (SIDS) Wamarekani huita Crib Death, lakini yule Daktari hakuwa na kumbukumbu zozote za vifo hivyo wakati katika eneo hilo kulikuwa na vifo vingi vya aina hiyo na watu walikuwa wakikamatana uchawi kweli kweli.................. Ilikuwa karibu watu wauwane, jambo ambalo lingeweza kuepushwa na wataalamu wetu hawa kwa kuwaelewesha wananchi hao juu ya vifo hivyo kitaalamu.
Nikipata muda nitaweka mada juu ya jambo hilo.
 
mimi ninavyojua ni kwamba post partum period imegawanyishwa katika vipindi tofauti tofauti.

  • kuna 1week post delivery: hapa dkt anampa mama appointment ili amwangalie anaendeleaje in terms of discharge na kama anatoa maziwa ,nk
  • 42 days post delivery ambapo organs za mwilini zinakuwa vimerudia khali yake ya zamani. however, it will take up to 6months post delivery for the joints to become fixed like before because during pregnancy, ile progesterone inasababisha relaxation ya joint ligaments.

ila swala lako hilo linaloitwa air embolism sidhani kama mishipa ya damu inabaki vulnerable (permeable) for that long! am sure within the 42days post delivery, those mishipa will be back to pre pregnancy states.

i stand to be corrected
 
Maelezo yako ni sahihi kabisa................................
 
Kama MWAKA MMOJA hivi...........................! LOL

mmh huo mwaka mzima ni mashindano ya olimpyc afu mwanaume atavumilia mwaka mzima kuona unapitapita mbele yake bila kukumbushia mchezo,huyo atakuwa na nyumbandogo i dought
 
mmh huo mwaka mzima ni mashindano ya olimpyc afu mwanaume atavumilia mwaka mzima kuona unapitapita mbele yake bila kukumbushia mchezo,huyo atakuwa na nyumbandogo i dought
Nimeshazua mjadala hapa.............Jamani nilikuwa natania tuuu..........................He!
 
Tanzania hatuwekagi kumbukumbu za vifo.........Mara nyingi mtu akifa kumbukumbu inayowekwa ni kwamba ALIROGWA.................... Niliwahi kutembelea Hospitali moja ya wilaya fulani na kumuuliza Daktari mkuu kama anayo kumbukumbu za vifo vya watoto usingizini kitaalamu huitwa Sudden infant death syndrome (SIDS) Wamarekani huita Crib Death, lakini yule Daktari hakuwa na kumbukumbu zozote za vifo hivyo wakati katika eneo hilo kulikuwa na vifo vingi vya aina hiyo na watu walikuwa wakikamatana uchawi kweli kweli.................. Ilikuwa karibu watu wauwane, jambo ambalo lingeweza kuepushwa na wataalamu wetu hawa kwa kuwaelewesha wananchi hao juu ya vifo hivyo kitaalamu. Nikipata muda nitaweka mada juu ya jambo hilo.
Sina uhakika kama jibu la hiv tunalitaka hapa jamvini,huwezi kuwa JF halafu ukaongea vitu kwenye mabano kama "wilaya fulani" !Yaani watu wanzembea halafu bado unatuficha wilaya inayofanya kazi kwa uzembe namna hiyo?Hebu kama unafunguka basi funguka laa sivyo usituwekee mafumbo kaa kimya!mie hiyo hjuu imenikera na km kweli ni stori halisia hebu fafanua Hii ni JF where people speak openly!
 
Back
Top Bottom