Mwanamke ni nani?( Sio msichana tafadhali)

Mwanamke ni nani?( Sio msichana tafadhali)

Prince Naahjum_

Senior Member
Joined
Jun 13, 2016
Posts
139
Reaction score
125
Mwanamke ni binadamu wa pili kuundwa na Mungu kutokana na ubavu wa Adamu.

Mwanamke ni yule ambae huijua thamani yake angali bado mdogo aidha kwa kufundishwa na wazazi wake au kwa utashi wake binafsi.

Mwanamke ameumbiwa mwanaume mmoja tu, mwanamke hatakiwi kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, hutulia na mwanaume mmoja hata pale mahusiano yake yasipoenda sawia, husubiri muda muafaka wa kupata mwanaume atakaempenda na sio kuwapanga foleni.

-: Hujua thamani ya mume wake na nafasi yake ya usaidizi kwa mwanaume wake.

-: Tumbo lake la uzazi li tayari kubeba mimba, nyonga zake zi tayari kupokea kashikashi za uchungu na kujifungua, Mikono yake na moyo wake u tayari

-: Humnyonyesha mwanae na si kumpa maziwa ya kopo akihofia kuharibu maziwa yake.

-: Hufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo na kumhudumia mumewe.

-: Kwake tendo la ndoa ni hisia zaidi na hulifurahia afanyapo na yule anae mpenda na sio zawadi kwa vile amefanyiwa jambo fulani na mwanaume yeyote.

WASICHANA HUWA HIVI....

-: Wamewapanga foleni wanaume, wanaume za watu pamoja na wavulana mithili ya enzi za kupokea mishahara dirishani au kidraw pesa ATM mara baada ya kutoka.

-: Hawana muda wa kuwaza future, wao ni kuponda raha kufa kwaja.

-: Kucha zao zina thamani, kuliko hata nguo zao za ndani.

-: Kwao mwanaume ni kitega uchumi swadakta kabisa, ambacho kinahitaji ili kupata wakitakacho huwekeza miili wao.

-: Hufanya ngono kwa kutegemea mrejesho wa pesa, kitu au ahadi walizopewa na watu wao..!

-: Hutumia muda wa dakika mbili kuoga lakini hutumia lisaa lizima katika kujiremba na kujipiga picha nzuri ya kuweka Instagramu, facebook, Snapchat huku wakilembua macho na kutoa ndimi zao nje mithili ya nyoka aonae kitu au mwenye kiu...!

-: Miaka ikikatika na akifiki sha umri wa miaka 30+ na bado bila bila, husema anahitaji mtoto tu na hana haja ya mume, lakini akiwa mwenyewe chumbani kwake, anajijua na nafsi yake jinsi anavyotamani maisha mema ya ndoa.

-: Utetezi wao mkubwa wao husema ndoa kitu gani, watu wanaoana leo na wanaachana kesho, pasina kujua kwamba Ndoa inahitaji msingi imara ikiwemo na uvumilivu na Mungu juu ya vyote.


NDUGU YANGU TAMBUA KUWA:-

Ni vigumu sana kushindana na asili, kuna wakati utafika na kusema bora ningefanya hivi. Amua njia ile iliyo sahihi ambayo kwayo unajiona hutakua na majuto nayo hapo baadae.

Siku zote kuna manufaa katika kusubiri, ila kuna majuto mengi katika kukurupuka.

Mungu awabariki 'wanawake' wote katika magumu yote mnayopitia akawafanyie wepesi, na pia awabariki 'wasichana' watambue ni nini wanapaswa kufanya, kwa wakati walionao na wajitambue na waweze kuwaza huko waendako....!

KWA JINSIA YA KIKE...!

VIPI WEW NI MSICHINA AU MWANAMKE.......!?





PRINCE NAAHJUM ALSINA
THE GREAT PIONEER



#THIS THING CALLED LIFE
 
Back
Top Bottom