Mwanamke mwenye nuksi

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Nadhani utakua umewahi kusikia hiyo kauli.

Inadaiwa kuwa kuna wanawake ambao mwanaume ukimuoa tu mambo yako yanaparaganyika.Yaani kama ulikua na mafanikio kidogo au sana unaanza kuandamwa na mikosi mpaka unafilisika kabisa.

Jambo la kushangaza sijawahi kusikia mwanaume mwenye nuksi,hapo ndipo napata wasiwasi wa dhana hii kuwa ya ukweli.

Kwanza sijui kama dhana hii ina ukweli na kama ina ukweli ni kwanini ni wanawake tu? Je, tutawezaje kumjua mwanaume aliyeshindwa kuwajibika na mwanaume alioa mwanamke wa aina hii kisha tukamhusisha na dhana hii?

Nahisi hii ni excuse ya wanaume wazembe ili wahalalise uzembe huo.

Kama ni kweli kuna wanawake wana nuksi naombeni uthibitisho halafu mniambie ni kwanini hakuna wanaume wenye nuksi (au wapo? Kwa mujibu wa dhana?)

Vinginevyo mtu atakaeniletea maneno haya nitamuona kama aliyeshindwa kuwajibika tu!
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,989
2,000
Hiyo dhana na uchawi wa akina @gfsnowin na mwenzie Zinduna wala hazina tofauti:smile:
 
Last edited by a moderator:

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
2,000
Mie huhusisha na ile kurelax kidogo baada ya ndoa na matumizi makubwa wakati wa harusi. Inachangia kuyumba kiasi, no savings etc. Lakini habari ya nuksi, akhhhu! Na uvivu wa kufikiria na kutenda unachangia.
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
king'ast ,tatizo la dhana hii ni kuwa mtu anaweza kuwa na hela lakini baada ya kuoa tu matatizo yanaanza
"
Hapa na mambo ya kwenda kwa mganga yanaanzia hapo,ndipo unaenda kwa mganga unaambiwa mkeo ana nuksi.
"
Nyani Ngabu ,binafsi naamini uchawi upo,ila dhana hii sidhani kama iko ki hivyo!
 
Last edited by a moderator:

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
king'ast ,tatizo la dhana hii ni kuwa mtu anaweza kuwa na hela lakini baada ya kuoa tu matatizo yanaanza
"
Hapa na mambo ya kwenda kwa mganga yanaanzia hapo,ndipo unaenda kwa mganga unaambiwa mkeo ana nuksi.
"
Nyani Ngabu ,binafsi naamini uchawi upo,ila dhana hii sidhani kama iko ki hivyo!
 
Last edited by a moderator:

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,613
2,000
Hiyo dhana hata mimi nimewahi kusikia zaidi ya mara moja ingawa nimekuwa mgumu sana wa kuamini kuwa dhana inayofanya kazi. Nimeshuhudia rafiki zangu wawili ambao baada ya kuoa mambo yao ya kiuchumi yalidorora sana.

Kwa haraka haraka, inawezekana si nuksi kama nuksi ila ni mfumo wa mwanaume wa kusaka pesa unaobadilika baada ya kuoa - unaweza kuchangia kushuka kwa kipato chake. Inawezekana labda kabla ya kuoa/kuwa na mpenzi alikuwa anajishughulisha sana na kazi na kufanya mpaka 'part-time' na 'overtime' lakini baada ya kuingia kwenye mahusiano anaumega muda wake kukaa na kufurahi na mpenzi wake na eventually anakuta kipato kikishuka wakati matumizi yanapanda (maana wako wawili na si pekee yake kama zamani) ...

Ni mtazamo tu ....
 

makolola

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
767
170
[h=1]mfahamu jini mahaba kisrani nuksi mikosi na kifungo mwilini mwako!!!!![/h]4/07/2015
imeletwa kwenu na dr. Tamba
huyu na jini mahaba wa aina yake katika majini mahaba wote jini huyu huwa na athari nyingi na za kisasi na vituko visa kwa alie kuwa nae mwilini mwake jini huyu usababisha madhara mbalimbali kwa wakati mmoja mtu akapatwa na matatizo mfululizo jini huyu uharibu uvuruga ufunga na kuteketeza vitu mbali mbali kuteketeza mali maisha ya mtu kutia maradhi mwilini kutesa mtu kumpa wakati mgumu maishani kushusha hadhi kushusha thamani kumfungia kila kitu na kumfukuzisha


kazi kibarua na kumuharibia ndoa kumuharibia mshusiano

kumfukuzisha kwa mume au kumkimbiza mtu asionekane bila ya ugomvi wala sababu jini huyu umtilia mtu kisirani katika kazi zake katika biashra katika maisha yakawa mikosi nuksi za mara kwa mara kupotteza pesa kutofanikisha kila ufanyalo umri unakwenda huna chochote cha maana ulichofanikisha maishani jini huyu ufunga mtu asipate mtomto wala asizae asishike mimba akishika inatoka jini huyu hata wakati mwingine usababisha kutopatikana kwa vipimo sahihi vya mgonjwa kwa visa vyake mtu anaweza kuumwa maradhi yasionekane mpaka madaktari wkashangaa jini huyu umsumbua mwanadamu na kumkosesha amani maishani ikaonekana kila kitu kipo sawa katika vipimo lakini yeye bado mgonjwa anaumwa kila siku na tiba hapati jini huyu umfunga mwanaume asimpe mimba mwanamke uharibu mbegu za uzazi za kiume zikawa viza au wadudu kukosa nguvu ya kumpa mtu mimba jini huyu uvuruga kazi biashara uitia kisrani ikakosa mafanikio ikakosa wateja ikakosa faida unauza upati kitu unapata khasara na hata udalali ukifanya ufanikishi unaweza kumtafutia mtu kitu akafanikisha wewe usipate chochote akatokea mwingine akapata kiulaini jini huyu ufunga rizki kipato na utaftaji kuwa mgimu pesa haikai ikiingia tu mara imetoweka bila cha maana ulichofanyia na ukipata kidogo haipatikani nyingine mpaka iliyopo iishe jini huyu uitia pesa mikosi na nuksi ukapatwa na majanga matatizo mfululizo mpaka pesa imalizike ukauguza ukauugua ukapatwa na misiba ukaharibikiwa na vitu vyako muhimu au mtoto akafukuzwa shule na kila tatizo huwa kisrani cha jini huyu umtia kisrani mtu asiolewe asiooe asikae na mtu mara kaachwa mara kakimbiwa jini huyu umfunga mtu akakosa misaada kwa watu mbalimbali anao wajua wakmdanganya au kumdharau na ahadi hewa zisizotekelezeka jini huyu mahaba kisirani na nuksi na mikosi uharibu vitu muhimu vya mtu mahali popote pale umsababishia mtu kutokubalika umuharibia kila kitu chake jini huyu mahaba wa kisrani umtia mtu katika kuchukiwa na watu hata ndugu jamaa na marafiki jini huyu ni hatari sana ukiwa nae mwilini mwako huna la maana utakalo fanikisha unaweza kufuatilia kitu ukifika mwisho kina kwama jini huyu umtia mtu nuksi kila mahali aendapo na kumsababishia migongano mbali mbali jini kisrani mahaba ukiwa nae ujue upo katika matatizo makubwa sana maishani jini huyu ufunga nyota zako na kuzitia giza zisiwake jini mahaba wa kisrani huwa jini anae kaa mbele mahali popote uwendapo atangulia yeye jini huyu hatari sana katika mwili wa mwanadamu na ukiwa nae huwezi kupata utakacho mpaka atoke mwilini au atolewe


 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Kweli mkuu kuna wanawake wenye nuksi nakumbuka chuo kuna mwanamke ulikuwa ukidate naye tu lazima ule sup za kufa mtu kama sio kudisco kabisa,
 

feitty

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
2,088
2,000
Me naisikia sana lakini huwa hainiingii akilini kabisa.Na ntaamini pale ntakaposikia na wanaume nao wana nuksi so ukiolewa nao mambo yako yanaharibika.Nadhani hizi ni imani tu tulizonazo na kama mwanamke anaweza akawa na nuksi lazima pia na wanaume watakuwa nazo.Na kwanini iwe wanawake tu.
 

akajasembamba

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
514
1,000
Me naisikia sana lakini huwa hainiingii akilini kabisa.Na ntaamini pale ntakaposikia na wanaume nao wana nuksi so ukiolewa nao mambo yako yanaharibika.Nadhani hizi ni imani tu tulizonazo na kama mwanamke anaweza akawa na nuksi lazima pia na wanaume watakuwa nazo.Na kwanini iwe wanawake tu.
Sasa mwanaume akiwa na nuksi huyo mke atampataje!! Wkt hana hela hana bahati kumbuka kigezo kikubwa cha mwanaume kuoa ni uwezo wa kipesa hata kidogo wkt mwanamke ni umbile lake sura au shepu yake ya kuzaliwa. Mwanaume mwenye nuksi hapati mke na nuksi ya mwanamke huonekana kwa kuwa wengi hutegemea wanaume, mporomoko wa mwanaume ndiyo huonyesha nuksi ya mke. Mwanamke haporomoki kwa kuwa huolewa na mtu aliyemzidi uwezo
 

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,758
2,000
Ila haya mambo yapo, na kuna wanawake wana kismati ukiwa naye mambo yanaenda vizuri hadi unajiuliza hili nimeweza wezaje kirahisi hivi?. Hapa na ushahidi kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom