Mwanamke mwenye mtoto!

Mwanamke mwenye mtoto!

jitengenezee role model ya maisha yako binafsi kwakuwa, kila atakayekushauri kuhusu hilo atakushauri kutokana na uzoefu wake binafsi ambao unaweza kuwa na madhara makubwa mno, au usikusaidie kabisa

Asante mkuu.
 
Jilipue tu, matatizo yanakuaga mengi hata kama si leo ni kesho, akishakuwa kama ni mtoto wa kiume anakuwa kama ndio mume wake kila kitu ushauri ni kwake

Ni mtoto wa kike..
 
Kumbuka hao wawili watawasiliana maisha yao yote, hao wameunganishwa na huyo mtoto. Iwe kwa mema au mabaya, mawasiliano baina yao hayakwepeki.

Inawezekana baada ya mda mfupi hisia zikarudi. je, umejiandaa kukabiliana na hali yoyote itakayojitokez? Nina mfano wa sibling, amezaa na mdada, bahati nzuri yule dada kaolewa, jamaa nae kaoa ila hawa jamaa wanakutana na kungonoka. Nilipomuuliza kwa nini anafanya hivyo akajibu, tunakumbushia..

Naamini wapo wanaojitambua ila, kama wewe ni mtu mwenye wivu wa "kijinga" utaumia sana.......!!!!!
 
Sina wasiwasi ila tu.. miluzi mingi humpoteza mbwa. Nampenda ananipendana...tunapendana.., tatizo baadhi ya ndugu na mama wanaona kuna siku ataniacha na kurudi kwa baba wa mtoto. Kitu ambacho kwa kwa tulivyoliongelea hilo swala na bibie ni kitu ambacho hakitatokea..japo OLESAIDIMU kaniasa nisijihakikishie vitu ambavyo havina uthibitisho kisayansi.

Pamoja na hayo tumepanga tuwe na simple function this coming june...na wengine wameanza kutangaza kutokuja.

amjuaye huyo mama mtoto ni wewe. wewe ndiye ujuaye asemacho ni kweli au la...wewe ndiye uonaye jinsi anavyoweza kuishi na huyo mzazi mwenzie na dalili zozote unaona.

kama kweli unampenda umchukue kwani hao wanaokushauri umuache utafute asiye na mtoto:
1. wamewazalisha mabinti wengine na wameolewa na wao wamepigwa kibuti.

2. wanaishi na mke ila watoto si wao (hawajui tu)

3. hawana scientific proof kuwa ukioa ambaye hajazaa hatakutenda kama wanavyodhani kwa huyu.
 
Last edited by a moderator:
Kumbuka hao wawili watawasiliana maisha yao yote, hao wameunganishwa na huyo mtoto. Iwe kwa mema au mabaya, mawasiliano baina yao hayakwepeki.

Inawezekana baada ya mda mfupi hisia zikarudi. je, umejiandaa kukabiliana na hali yoyote itakayojitokez? Nina mfano wa sibling, amezaa na mdada, bahati nzuri yule dada kaolewa, jamaa nae kaoa ila hawa jamaa wanakutana na kungonoka. Nilipomuuliza kwa nini anafanya hivyo akajibu, tunakumbushia..

Naamini wapo wanaojitambua ila, kama wewe ni mtu mwenye wivu wa "kijinga" utaumia sana.......!!!!!

Dah..moyo unapondeka..
 
amjuaye huyo mama mtoto ni wewe. wewe ndiye ujuaye asemacho ni kweli au la...wewe ndiye uonaye jinsi anavyoweza kuishi na huyo mzazi mwenzie na dalili zozote unaona.

kama kweli unampenda umchukue kwani hao wanaokushauri umuache utafute asiye na mtoto:
1. wamewazalisha mabinti wengine na wameolewa na wao wamepigwa kibuti.

2. wanaishi na mke ila watoto si wao (hawajui tu)

3. hawana scientific proof kuwa ukioa ambaye hajazaa hatakutenda kama wanavyodhani kwa huyu.

Asante sana mkuu. What a powerful advice. Be blessed.
 
Kwa mwanamke anasema hata kama sitamuoa au hatatokea mtu wa kumuoa basi atakaa hivyo hivyo kuliko kuishi na huyo baba wa mtoto.

Hizo changamoto ni zipi mkuu? Japo nyingine nimeanza kuziona mfano; mama na ndugu hawataki kusikia hiyo habari..kwa sababu tu ya huyo mtoto.

Kwa sasa utasikia mengi tu hata ambayo atashindwa kwa "circumnstancial reasons" ila chuja sana anayosema na wewe unayoona yanawezekana!!!!!

Kukiwa na kikao cha shule utaenda wewe,mama yake ,baba mzazi au wote????!!!!
Mtoto akiumwa (God forbid) huko kwa baba yake mama akakuambia anaenda kushinda na mtoto nawe utshinda huko,utampitisha then umfuate au utaacha aamue mwenyewe???!!!
Baba wa mtoto akiumwa na mpenzio akakuambia anaenda kumjulia hali (request) utasemaje!!!!???
 
Hili jambo wanawake wengi hufanya mpwa hata wale ambao hawana watoto lakini walikuwa tu kwenye mahusiano na watu ambao mwishoni waliwatelekeza.

Mpwa hili jambo lishaumiza wengi sababu dhamira is so disguising!!!!
 
Hapo sasa. Kwa hiyo mkuu nikae kwa wasiwasi tuu..?

Wasi wasi hauna nafasi juu ya hili!!!!!
Jua tu kuna changamoto za hapa na pale na zinaweza kuwa sehemu ya maisha yenu!!!!?????
Ila inawezekana
 
Asante sana mkuu. What a powerful advice. Be blessed.

This is exactly what you want....???

Basi mimi nakushauri kuwa usimsikilize mtu yeyote wa nje...isikilize nafsi yako na wishes zako tu. Kwani mambo yakienda kinyume, hivyo ndivyo utakavyovililia.

Ila kama kweli wewe umejihakikishia kuwa hakuna tatizo lolote na mapenzi yenu ni very strong, kwa nini umeleta huu uzi?

Siyo lazima kujibu hilo swali ila ukijiweka sawa moyoni mwako basi chapa lapa kwa kwenda mbele ili kutekeleza kile unachotamani kukifanya!!
 
^^
Kama umempenda kupita kiasi, love is all about risk taking
^^

lakin akumbuke kitukimoja kuwa mtaliki hatongozwi ila wanakumbushiana tu..... Na mtoto huwa ni kiunganishi cha wazazi.( ni kitu niliwahi kukishuhudia kwa macho yangu) kama huyu mweshimiwa kafungua moyo basi aweke ndani tu
 
Mpwa hili jambo lishaumiza wengi sababu dhamira is so disguising!!!!

Hata mtu akioa au kuolewa na bikra, maisha ya ndoa yana changamoto nyingi. Bora enzi za 1947, ndoa ilikuwa inalindwa na jamii kwa nguvu nyingi sana. Siku hizi, watu ambao tena wengine ndiyo hawajakua kiwamazo wameachwa wapweke wakapuyange wenyewe na mambo yao ya ndoa (sometimes bila msaada wa kutosha). This is very unfair but yet the reality!
 
This is exactly what you want....???

Basi mimi nakushauri kuwa usimsikilize mtu yeyote wa nje...isikilize nafsi yako na wishes zako tu. Kwani mambo yakienda kinyume, hivyo ndivyo utakavyovililia.

Ila kama kweli wewe umejihakikishia kuwa hakuna tatizo lolote na mapenzi yenu ni very strong, kwa nini umeleta huu uzi?

Siyo lazima kujibu hilo swali ila ukijiweka sawa moyoni mwako basi chapa lapa kwa kwenda mbele ili kutekeleza kile unachotamani kukifanya!!

Ukipitia hizo post nyingine utajua kwa nini nimeuleta huu uzi. Kusifia kitu kuwa kizuri haina maana kuwa ndio unakichukua.
 
Kwa sasa utasikia mengi tu hata ambayo atashindwa kwa "circumnstancial reasons" ila chuja sana anayosema na wewe unayoona yanawezekana!!!!!

Kukiwa na kikao cha shule utaenda wewe,mama yake ,baba mzazi au wote????!!!!
Mtoto akiumwa (God forbid) huko kwa baba yake mama akakuambia anaenda kushinda na mtoto nawe utshinda huko,utampitisha then umfuate au utaacha aamue mwenyewe???!!!
Baba wa mtoto akiumwa na mpenzio akakuambia anaenda kumjulia hali (request) utasemaje!!!!???

OLESAIDIMU naona umedhamiria kumkatisha tamaa in the name of being real.

kuhusu kikao cha shule cha wazazi sioni tatizo hapo wakienda wawili.

kuumwa kwa mtoto tena wa kike ni vyema kama ataenda kukaa na mama yake hadi atakapopona.

halafu kwanini una assume kuwa huyu mzazi mwenzie yeye hataoa? weka assumption kuwa na yeye ataoa soon so akiumwa atahudumiwa na mkewe and even if hataoa hilo swali wala si la kujadili atafute tu ndugu au rafiki akamhudumie.

nb: kumbuka nadharia zote hizi huweza kutokea hata kwa wale walioolewa na bikra..look vere.
 
Last edited by a moderator:
Kwa sasa utasikia mengi tu hata ambayo atashindwa kwa "circumnstancial reasons" ila chuja sana anayosema na wewe unayoona yanawezekana!!!!!

Kukiwa na kikao cha shule utaenda wewe,mama yake ,baba mzazi au wote????!!!!
Mtoto akiumwa (God forbid) huko kwa baba yake mama akakuambia anaenda kushinda na mtoto nawe utshinda huko,utampitisha then umfuate au utaacha aamue mwenyewe???!!!
Baba wa mtoto akiumwa na mpenzio akakuambia anaenda kumjulia hali (request) utasemaje!!!!???

Maswali magumu kweli. Sina hata jibu la moja kwa moja. Ila je kama case zote zitatokea na asiende wala kujishughulisha nayo tuiteje?
 
Hata mtu akioa au kuolewa na bikra, maisha ya ndoa yana changamoto nyingi. Bora enzi za 1947, ndoa ilikuwa inalindwa na jamii kwa nguvu nyingi sana. Siku hizi, watu ambao tena wengine ndiyo hawajakua kiwamazo wameachwa wapweke wakapuyange wenyewe na mambo yao ya ndoa (sometimes bila msaada wa kutosha). This is very unfair but yet the reality!

Nashukuru babu ,kwanza heshima yako sana!!!!!

Ndio maana namsihi huyu mwanaume mwenzangu alichukue jambo hili kwa tahadhari!!!!
 
Hakuna ubaya wowote uliopo kuoa mwanamke mwenye mtoto maadamu mnapendana.

Lakini mwenye mtoto ataendelea kugegeda mamatoto kama zamani.

Kama hiyo siyo shida kwako, basi unaweza kumuoa huyo mama mtoto.

Ushauri wa kukatisha tamaa huu!
 
Wasi wasi hauna nafasi juu ya hili!!!!!
Jua tu kuna changamoto za hapa na pale na zinaweza kuwa sehemu ya maisha yenu!!!!?????
Ila inawezekana

Mkuu. Kwa changamoto zile za mwanzo..jibu linaweza likawa hivi...na hili alinipa mwenyewe.."nitafanya mchakato wa kumchukua mtoto, ikishindikana basi nitaendelea kuwa mama yake na najua ipo siku atanitafuta". Wasiwasi wangu ukaja kwamba...kwa hicho kipindi mtoto atakachonitafuta..uhusiano wangu na huyo mtoto utakuwaje? Isije ikawa kalishwa sumu kuwa mimi ndio chanzo cha baba yake kuachwa na yeye 'kutelekezwa'.
 
Back
Top Bottom