Likundumbwii
Member
- Jun 21, 2019
- 7
- 5
Habari zenu hapa wandugu kwa wakubwa na Wadogo. Wandugu nimekuja hapa naomba ushauri kwa huyu binti ambae nimetokea kumpenda na kuwaza Kuishi Nae. Ni binti wa Makamo ambae aliachishwa kuendelea na chuo cha uwalimu wa Prmary kutokana na kupatiwa ujauzito na kijana mmoja ambae nae alikua katika masomo katika Mkoa Husika Anakoishi huyu binti na kisha kumkimbia kwa kurudi makwao. Binti akajifungua na sasa Mtoto yupo na Miez 8 na anasumbuliwa na kifua ivo upelekea kuhitaji matibabu mara kwa mara. Siku Moja Katika Safari za kikazi katika kituo cha Afya kimoja nikakutana na huyu binti katika salamu salamu za hapa na pale nikamgundua binti hawaamini wanaume, Kwakua ilikua Ameenda kupata matibabu namimi si mkaaji pale nikampatia Namba Zangu Katika Karatasi kwani Hana simu.Ni mwezi sasa Amenitafuta jana na Leo nimeonana nae Na meengi kunieleza Kwani hata kwao Kwa sasa n kama Ananyanyaswa kwa kukosa huduma stahiki(Anavosema). Katoto ni kazuri na mwenye furaha niko tayari kumpokea kwa hari alionayo na tulee uyu mtoto Mpaka umri sahihi apatiwe Nduguzo Na Mengineyo atatimiziwa. Naombeni ushauri Wandugu kwa huu Upendo Wangu kwa huyu Dada. Maswali ninajibu.