Mwanamke msagaji ameniambukiza virusi vya ukimwi.

Mwanamke msagaji ameniambukiza virusi vya ukimwi.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,349
Reaction score
36,303
536369_280862738656675_795011333_n.jpg





Zuwena ( sio jina lake halisi ), ni mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 43. Kwa sasa mwanadada huyu anaishi na virusi vya ukimwi. Mwanadada huyu anabainisha namna, alivyo pata maambukizi ya v.v.u kw kujamiiana na mwanamke mwenzake, ama kwa lugha nyingine, Zuwena anaeleza namna ambavyo mwanamke msagaji alimuambukiza v.v.u wakati wakiwa na uhusiano wa jinsi moja... Fuatilia kisa hiki cha kufundisha na kusikitisha.




425788_277557108987238_1348503100_n.jpg

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007, nilipata tenda ya u MC

katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule Buza.

Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia.

Kama kawaida niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na kufurahi. Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa
naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula.

Ghafla alitokea mama mmoja mtu mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi. Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli yake.

Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba yangu.

Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno " Ahsante baby ". Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu, alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu, nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia chenji ananiambia " utakunywa soda " , siku nyingine anafika ofisini kwangu ananipa hela anaondoka. Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini sikupata jibu.

Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye.

Ilikuwa siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja akanipigia kuniulizia nimekwama wapi? Nikamwambia bado nina wateja , akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo yote. Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo akatoa shilinge 50,000/= .

Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji naishi na nani, nikamwambia naishi na watoto wangu watatu, baba yao baba yao amefariki miaka miwili iliyopita .

Nikamuuliza saluni anataka kufungulia wapi? Akanijibu achana kwanza na mambo na mambo hayo tutaongea baadaye . Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia nawawahi watoto wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue.

Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akavishusha saluni kwangu, akaniambia atanipigia simu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akabishusha saluni kwangu , akaniambia atanipigia simu kesho yake
kuna kitu anataka kunieleza.

Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu wa karibu , ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote mbali ya pale Buza kwa sababu nia yake hatueielewi. Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale .

Alipokuja nilitoa hela ili nimuagizie kinywaji, Yule mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete kinywaji ila alimuomba
Yule rafiki yangu akae meza nyingine. Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa.

Yule rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na akaja kutuaga akaondoka.Nilimtumia meseji kuwa asicheze mbali.

Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu, akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka. Yaani hapo ndio alinifanya niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu wengine wakasema labda ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda
tu au anataka kaka yake akuoe.

Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie nguo za biharusi mtarajiwa.

Tukaondoka wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nakamwambia yapata mwezi mmoja sasa. Nikamuuliza mbona
unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa nakuuliza tu.

Akaniuliza unajishughulisha na nini ,nikamwambia nina saluni na ni mc, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au nimeajiriwa ? Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa ananiambia mimi nichague nguo niliyo ipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa wa Agrrey kuna duka linauzwa nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje kuna kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe tama nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu , meseji ilikuwa
inasema hivi " Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni msagaji mzuri pole Aunty nakuhurumia, " by Angel .

Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia mbona umesoma sms ukaonekana umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms mtoto wake anaumwa sana.

Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama, nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi hospitali. Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli,nilitoka speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari,sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia vocha yash. 5000/= na ujumbe uliosema " I love you baby "

Nilipofika nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine waliniambia namsingizia . Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku hiyo hiyo na pale saluni nisikae.

Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi ya saluni Yombo pale kwangu nikaweka msichana. Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri na simu sina.

Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni kwangu kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote. Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu nikahamia Tandika nyumbani kwetu.

Nilicho hofia ni kwamba kwa sababu nilishakula pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia angeweza kunifanyia chochote.

Je Ni Kitu Gani kiliendelea? Fuatilia kisa hiki cha kusikitisha na kufundisha kupitia :
 
shigongo at work.

Imetosha sasa kaka, tuangalie umuhimu wa uzi huu kwa jamii yetu, habari za Shigongo zinatoka wapi tena mjomba?. Kwa nini usi apreciate jitihada za kutoa elimu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi? Uki apreciate tunacho kifanya hauwezi kupungukiwa na kitu chochote.
 
Huja eleza jinsi huo ukimwi unavyo ambukizwa bado,naona ni hadithi tu,ungeeleza hasa kisayansi ungeelimisha jamii zaidi.
 
Imetosha sasa kaka, tuangalie umuhimu wa uzi huu kwa jamii yetu, habari za Shigongo zinatoka wapi tena mjomba?. Kwa nini usi apreciate jitihada za blogu yangu katika kutoa elimu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi? Uki apreciate tunacho kifanya hauwezi kupungukiwa na kitu chochote.

samahani mkuu kumbe una adivertise blog yako!! i really appreciate ur work bt weka full story.
 
Ni kitu gani
kinakufanya uone hii ni hadithi? ni kwa sababu hauamini usagaji
waweza sababisha maambukizi ya ukimwi au?

ni hadithi nzuri ya kubuni,ila tu ina ujumbe mzuri pia,hongera kwa kipaji chako cha hali ya juu cha utungaji.
 
MADENTI.jpg



USAGAJI NA UKIMWI TANZANIA: Maambukizi Ya V.V.U Miongoni Mwa Wanawake wanao jamiiana na Wanawake Wenzao Nchini Tanzania.
ULIMWENGU USIONEKANA
Na. Waandishi Maalumu.

UTANGULIZI

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye idadi kubwa ya watu wanao ishi na virusi vya
ukimwi . Kwa mujibu wa taarifa ya Tume Ya Taifa Ya Kudhibiti Ukimwi nchini ( TACAIDS ) kwenye
matokeo ya Utafiti wa Kiashirio Cha VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania mwaka 2007-2008 uliojumuisha
kwa kupima zaidi ya wanawake na wanaume 15,000, asilimia 5.7 ya watanzania wenye umri wa
miaka 15-49 wana maambukizo ya VVU/UKIMWI. Matokeo ya utafiti huo yanaendelea kubainisha
kuwa wanawake wanaambukizwa mapema zaidi kuliko wanaume na kwamba kwa wanawake
maambukizo yanaongezeka na umri mpaka inafikia umri wa miaka 30-34 ( 16.4%) wakati
maambukizi ya kiwango cha juu kwa wanaume yanatokea kati ya miaka 35-39 ( 10.6%).
Ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huu ulio fanyika mwanka 2003-2004, matokeo ya
utafiti wa mwaka 2007-2008 yanaonesha kitakwimu kushuka kwa maambukizi ya VVY/UKIMWI
miongoni mwa wanaume lakini si kwa wanawake. Hii ina maana kuwa asilimia kubwa ya watu
wenye VVU/UKIMWI ama ambao wapo katika hatari kuu ya kupata maambukizi ya V.V.U nchini Tanzania ni wanawake.
Pamoja na kwamba wanawake ndio waathrika wakuu wa VVU/UKIMWI nchini Tanzania, yapo
makundi ya wanawake ambayo ndio yapo katika hatari kuu zaidi ya kupatwa na maambukizi ya
v.v.u.
Kwa mujibu wa utafiti wetu, makundi hayo ni pamoja na:

Mosi; wanawake walemavu; walemavu wa akili, walemavu wa ngozi, walemavu wa kuona,
walemavu wa kusikia, walemavu wa viungo, walemavu wenye ulemavu zaidi ya mmoja.

Pili: Wanawake wanao fanya biashara ya kuuza miili yao,

Tatu; wanawake wanao toka katika jamii zinazo shikilia mila na desturi hatarishi kwa maambukizi ya v.v.u, Mila hizo ni pamoja na ;

I.Mila ya kukeketa watoto wa kike
II.Mila ya kurithi wajane
III. Mila ya kutakasa wajane,
IV.Mila ya nyumba nthobhu na
V. Mila ya ndoa za mitaala.
VI.
Nne; Ni wanawake wanao jihusisha na tabia hatarishi za kingono ambazo ni pamoja na wanawake wanao jihusisha na ngono ya kinyume na maumbile na pili wanawake wanao jihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Makala haya yamejikita zaidi katika kuelezea suala la maambukizi ya v.v.u miongoni mwa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao. Hii ni kwa sababu, kuna ombwe la maarifa kuhusu suala hili, na wanawake wengi leo hii, wanajiingiza kwa wingi katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo wanajiweka katika hatari kuu ya kupatwa na maambukizi ya v.v.u na pia kuusambaza ugonjwa huo kwa watu wengine.

Makala haya yanalichambua kwa mapana na marefu suala la maambukizi ya v.v.u miongoni mwa
wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini Tanzania. Kwa mujibu wa utafiti ulio pelekea
kutolewa kwa makala haya, wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini wapo katika
hatari kubwa sana ya kupatwa na maambukizi ya v.v.u . Makala haya yana sehemu zipatazo zipatazo sita ;

Sehemu ya kwanza inaonyesha namna ambavyo suala la mahusiano ya jinsi moja kati ya wanawake kwa
wanawake limeenea na kushamiri katika jamii yetu.

Sehemu Ya Pili : inazionyesha, kuzielezea na kuzichambua kwa kina sababu haswa zinazo wafanya wanawake hawa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao.

Sehemu Ya Tatu : inalielezea kwa kina suala la maambukizi ya
v.v.u miongoni mwa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini Tanzania.
Sehemu hii inaonyesha ni kwa jinsi, namna na kiwango gani suala la mahusiano ya jinsi moja kati ya
wanawake kwa wanawake linasababisha kuenea kwa kasi ya maambukizi ya v.v.u kati ya wahusika na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Sehemu Ya Nne : Inaonyesha SHUHUDA KUTOKA KWA WANAWAKE WA KITANZANIA, WALIOPATA MAAMBUKIZI YA V.V.U KWA KUJAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO…Hapa utapata kuzisoma shuhuda za wanawake wa kitanzania wapatoa kumi na watatu ambao wamepata maambukizi ya V.V.U kwa kutokana na kujamiiana na wanawake wenzao, pamoja na shuhuda za wanawake wakitanzania wapato wanne ambao waliingia katika mahusiano ya jinsia moja na zaidi ya mwanamke mmoja huku wakiwa wanajijua fika wana maambukizi ya V.V.U.

Sehemu Ya Tano : Inaonyesha athari nyinginezo wanazo weza kuzipata wanawake wanao wanao
jamiiana na wanawake wenzao nchini. Athari hizo ni pamoja na kupatwa na magonjwa
mengineyo ya zinaa kama vile Gonorhea nakadhalika, athari za kiakili, kimwili na kiroho, pamoja na
athari ziipatayo ama zinazo weza kuipata jamii nzima kutokana na kuwepo kwa wanawake
wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini.

SEHEMU YA SITA : MASWALI NA MAJIBU KUHUSU WASAGAJI NA USAGAJI: Sehemu hii, inajibu maswali mbalimbali yanayo ulizwa na watu kuhusu wasagaji na usagaji kwa ujumla. Maswali kama vile, " mtu akiingia kwenye usagaji hawezi kuacha?", maswali kama vile " Inasemekana wasagaji wana uwezo mkubwa wa kuwaridhisha wanawake kuliko wanaume wanavyo weza kufanya? Majibu ya maswali haya yote na mengineyo yamejibiwa na zaidi ya wanawake wasagaji wapato arobaini wakaazi wa majiji ya Dar Es salaam, Zanzibar na Arusha...Vile vile, kutakuwa na shuhuda kutoka kwa baadhi ya wanawake wasagaji wa hapahapa Tanzania, ambao wanaelezea jinsi walivyoingia katika usagaji, maisha yao katika usagaji yalikuwa vipi, athari walizo zipata, na jinsi walivyo weza kuachana na tabia hii hatarishi kwa afya zao pamoja na ustawi wa taifa letu. Endelea kufuatilia makala haya kupitia hapa hapa JF na kwenye blogu ya : http//www.mungwakabili.blogspot.com

Sehemu Ya Saba : yamfululizo wa makala hayai inatoa mapendekezo ya juu ya kitu gani kifanyike ili kukabiliana na suala la kushamiri kwa vitendo vya mahusiano ya jinsi moja kati ya wanawake kwa wanawake
nchini. Sehemu hii inatoa mapendekezo ya kitaalamu, juu ya mambo gani yafanyike ili kuwafanya
wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini waweze kuachana kabisa na tabia hiyo
hatarishi kwa maambukizi ya v.v.u na wale ambao walikuwa wanafikiria kutaka kuingia katika mahusiano haya waachane kabisa na mawazo hayo.. Sehemu inapendekeza hatua na majukumu yanayo takiwa kufuatwa na kuchukuliwa na watu wa kada na kaliba mbalimbali katika jamii yetu, ili kusaidia
katika mapambano dhidi ya tabia hii hatarishi kwa maambukizi ya v.v.u.

Fuatilia mfululizo wa makala haya mwanzo hadi mwisho, kila siku tutakuwa tuna publish muendelezo wa mfululizo wa makala haya.
Sehemu Ya Kwanza :

WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO NCHINI TANZANIA.



Sehemu Ya Pili :



SABABU ZINAZO WAFANYA WANAWAKE KUINGIA KATIKA MAHUSIANO YA JINSI MOJA. ( A CASE OF TANZANIA )

Sehemu Ya Tatu :



MAAMBUKIZI YA V.V.U MIONGONI MWA WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE
WENZAO NCHINI TANZANIA.


Sehemu Ya Nne :


SHUHUDA KUTOKA KWA WANAWAKE KUMI NA TATU WA KITANZANIA AMBAO WAMEPATA MAAMBUKIZI YA V.V.U KUTOKANA NA KUJAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO.



Sehemu Ya Tano ;

ATHARI NYINGINEZO ZA MAPENZI YA JINSI MOJA KWA WANAWAKE.


SEHEMU YA SITA : MASWALI NA MAJIBU KUHUSU WASAGAJI NA USAGAJI: Sehemu hii, inajibu maswali mbalimbali yanayo ulizwa na watu kuhusu wasagaji na usagaji kwa ujumla. Maswali kama vile, " mtu akiingia kwenye usagaji hawezi kuacha?", maswali kama vile " Inasemekana wasagaji wana uwezo mkubwa wa kuwaridhisha wanawake kuliko wanaume wanavyo weza kufanya? Majibu ya maswali haya yote na mengineyo yamejibiwa na zaidi ya wanawake wasagaji wapato arobaini wakaazi wa majiji ya Dar Es salaam, Zanzibar na Arusha...Vile vile, kutakuwa na shuhuda kutoka kwa baadhi ya wanawake wasagaji wa hapahapa Tanzania, ambao wanaelezea jinsi walivyoingia katika usagaji, maisha yao katika usagaji yalikuwa vipi, athari walizo zipata, na jinsi walivyo weza kuachana na tabia hii hatarishi kwa afya zao pamoja na ustawi wa taifa letu. Endelea kufuatilia makala haya kupitia hapa hapa Ulimwengu Usioonekana Blog.
Sehemu Ya Saba : SULUHISHO LA TATIZO LA USAGAJI KATIKA JAMII YETU : Mapendekezo ya mambo gani yafanyike ili kutokomeza suala la usagaji katika jamii yetu.




KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUIJENGA NCHI YETU. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.


Endelea kufuatilia mfululizo wa makala haya kila siku kupitia hapa hapa : www.mungwakabili.blogspot.com
 
SEHEMU YA KWANZA : WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO NCHINI TANZANIA.

SOURCE : ULIMWENGU USIONEKANA


SEHEMU HII, INAJIBU SWALI, JE ? TANZANIA WAPO WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO? KAMA WAPO WAPO KWA KIASI GANI? NA VITU GANI VINAVYO TUAMBIA KUWA TANZANIA TUNAO WANAWAKE WA AINA HII? AMA NINNI VIASHIRIA VYA UWEPO WA WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO NCHINI TANZANIA?




431252_265172226892393_43046631_n.jpg



Katika miaka ya hivi karibuni, suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja kati ya wanawake kwa wanawake maarufu kama usagaji linatajwa na ama kuripotiwa kushamiri sana katika jamii yetu.


" In 1999, some lesbian activists in Dar es salaam, decided to set up a lesbian association . Its current membership is 205 women, who come from all over the country ….Ruth Morgan & Saskia Wieringa( 2005) kwenye kitabu Tommy Boys, Lesbian Men & Ancestral Wives: Female Same Sex Practices In Africa, ukurasa wa 54. Mwishoni mwa sehemu hii, nitawaletea uchambuzi wa kitabu hiki, ili muone ni kwa namna gani, jamii yetu imekuwa corrupted.

Tafsiri ya sentensi hii ni :
" Mnamo mwaka 1999, wanaharakati wasagaji waliamua kuanzisha chama cha kutetetea haki zao jijini Dar Es salaam. Sasa hivi chama kina wanachama 205 ambao wanatoka katika mikoa yote ya Tanzania ."

UFAHAMU WA WANAWAKE WA TANZANIA JUU YA UWEPO WA WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA JAMII.

Tulifanya mahojiano na wanawake wapatao mia nne ( 400) jijini Dar Es salaam wenye umri wa kati ya miaka 16 hadi 45 ili kubaini ufahamu wao juu ya uwepo wa wanawake na ama wasichana wanao jihusisha na mahusiano ya jinsi moja katika jamii yetu .
Wanawake wanane katika kila wanawake kumi waishio jijini Dar Es salaam, wenye umri wa kati ya miaka 18-45 wamekiri kuwahi kusikia kuhusu uwepo wa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao katika jamii yetu.

Mwanamke mmoja katika kila wanawake 20 wenye umri wa miaka 16- 30, amewahi kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake/ na ama wasichana wenzake ana kwa ana.

Wanawake wanne katika kila wanawake kumi wanao tumia mitandao ya kijamii, wamekiri kuwahi kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao, kupitia katika mitandao hiyo ya kijamii.
Wanawake wawili katika kila wanawake kumi wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 45, wanamfahamu ama kufahamiana na angalau mwanamke mmoja anayedaiwa kujihusisha na mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzake.

Mwanamke mmoja katika kila wanawake thelathini wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 45 amewahi kujamiiana na mwanamke ama wanawake wenzake.

Katika sehemu ( sura ) ya pili ya makala haya, nitaelezea athari za wanawake/wasichana kuwa na ufahamu kuhusu uwepo wa wanawake/wasichana wanao jamiiana na wanawake wenzao. Endelea kufuatilia makala haya kupitia hapa JF ama htpp://www.mungwakabili.blogspot.com
 
SEHEMU YA KWANZA INAENDELEA : Vyanzo Vikuu Vya Taarifa Zinazo husu Uwepo wa Wanawake Wanao Jamiiana na Wanawake Wenzao Nchini Tanzania

source : ULIMWENGU USIONEKANA



417397_265172203559062_2123771777_n.jpg






Tulitaka kujua kuhusu vyanzo vya taarifa zao kuhusu uwepo wa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao katika jamii, ama kwa maana nyingine tulitaka kujua ni wapi huko wanapo zipata taarifa za kuwepo kwa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao katika jamii yetu?.
Wanawake saba kati ya kumi walio fanyiwa mahojiano walisema, taarifa nyingi kuhusu uwepo wa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao katika jamii wamezipata katika vyombo vya habari hususani magazeti , blogu na mitandao ya kijamii, wanawake wawili kati ya kumi walio hojiwa walisema walisikia juu ya uwepo wa suala la usagaji katika jamii kutoka kwa watu ambao wameshududia ama kusimuliwa kuhusu uwepo wa wanawake wa aina hiyo. Wanawake watatu kati ya kumi walisema walisikia ama kushuhudia juu ya uwepo wa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao walipo kuwa mashuleni na vyuoni.


WANAWAKE AMBAO WANAWAFAHAMU " PERSONALLY "WANAWAKE WANAO DAIWA KUJAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO .


Tukataka kupata takwimu za idadi ya wanawake ambao wanamfahamu mwanamke au wanawake ambao wanadaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja . Katika kila wanawake 20 walio fanyiwa mahojiano wawili kati yao wamekiri kumfahamu mwanamke ama wanawake ambao wanadaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.


" Ninafahamu wasichana zaidi ya kumi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.Baadhi yao ni wasichana wa mitaani na wengi nimewafahamu katika mazingira ya chuo. " anasema Tina.


i. Nimewahi kusikia visa vinne vyenye ushahidi vinavyohusiana na wanawake wanaojamiiana na wanawake wenzao hapa jijini Dar Es Salaam. Nitavielezea kama ifuatavyo:-

Kisa cha kwanza ni kile kilichowahi kurushwa hewani na redio Clouds Fm, kupitia kipindi cha leo tena cha Dina Marios kwenye kipengele cha hekaheka. Hiki ni kile kisa kilichomuhusu mama aliyekuwa akimfanyia vitendo vya usagaji mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka saba, na kupelekea mtoto huyu kuharibika kabisa maumbile yake ya uke na pia sehemu ya haja kubwa.

Kisa cha pili kiliwahi kuandikwa kwenye gazeti la uwazi sikumbuki toleo lipi, hiki kilimuhusisha dada mmoja ambaye alikuwa akiishi maeneo ya (Kigogo Cha Wote) karibu na shule ya Msingi. Yeye alikuwa na mahusiano ya jinsia moja na mtoto wa darasa la sita kutoka katika hiyo shule ya jirani. Inasemekana mtoto huyo alikuwa pia akiishi jirani na alipopanga huyo dada, na alikuwa na mazoea ya kutumwa dukani na huyo dada. Kilichotokea ni kwamba baada ya kujenga mazoea na ukaribu na mtoto huyu, huyu dada alimshawishi mwanafunzi huyu kufanya nae vitendo vya usagaji kwa kusema kwamba ni salama kwani hatopata maambukizi wala ujauzito na pia si rahisi wazazi kugundua kwani dada huyu alikuwa akimwita huyu mwanafunzi mdogo wake wa hiari. Kadri siku zilivyoenda mwanafunzi alibadilika darasani alishuka kitaaluma na wakati mwingine alikuwa akitoroka shule na kwenda kwa huyu mpenzi wake, na siku zingine kutofika kabisa shule. Hali hii ilipelekea walimu wake kufanya mawasiliano na wazazi ili kujua tatizo nini. Cha ajabu wazazi hawakujua chochote sababu binti alikuwa akitoka nyumbani asubuhi na kurudi muda ule ule wa kutoka shule. Ndipo ilpobidi walimu na wazazi wambane na kumuhoji vizuri Yule binti na hatimaye alielezea yote yaliyokuwa yakifanyika katika mahusiano yake na Yule dada.



Walimu na wazazi wakishirikiana na polisi waliamua kuweka mtego ili kumtia hatiani Yule dada, hivyo wakamtuma Yule binti atoke kwenda kwa Yule dada na akifika asiseme chochote ila aendelee na ratiba zao za kila siku na wao watakuwa karibu kabisa na eneo la tukio ili kupata ushahidi wa kutosha. Hivyo binti alifanya kama alivyoelekezwa na hatimaye walifanikiwa kumkamata Yule dada akimfanyia vitendo hivyo Yule binti na kumtia hatiani.

Kisa cha tatu hiki nilisimuliwa na jirani yangu ambaye alikuwa akifanya kazi katika duka moja la wahindi huko kariakoo. Huyu dada alifanya kazi katika duka hilo kwa muda wa mwaka mmoja na alikuwa akiishi hapohapo kwa mabosi wake. Tulikuwa katika maongezi ya kawaida nikamuuliza kwa nini aliacha kazi ya kuuza duka? Ndipo aliponosimulia yaliyojiri, akasema yeye hakuacha kazi ila lile duka lilifungwa na mume wa bosi wake. Nikamuuliza kwa nini lifungwe? Akaniambia kwamba bosi wake yeye alikuwa ni mwanamke aliyeolewa na ana watoto wanne wa kwanza akiwa form six. Huyu bosi alikuwa na rafiki yake mwingine ambaye ni mwanamke pia na ni muhindi mwenzie. Kwa muda wote ambao yeye amekuwa akifanya kazi pale aligundua hawa watu wana ukaribu sana zaidi ya urafiki wa kwaida. Ndipo akawaulizia wenzake ambao walitangulia kuajiriwa pale nao wakamwambia kuwa wale wanawake wawili ni mtu na mpenzi wake ila wote wameolewa na waume zao hawajui kinachoendelea. Kutokana na maelezo ya huyu jirani yangu anasema muda mwingi Yule rafiki wa bosi wake alikuwa akija kushinda pale dukani na mara nyingi akija huwa ana tabia ya kumpakata bosi wake na kuna wakati aliwahi kushuhudia akimpapasa, ina maana huyu bosi wake ndie aliyekuwa akishika nafasi ya kike na Yule rafiki yake ndie aliyeshika nafasi ya kiume katika mahusiano yao. Na mara zote mume wa bosi wake anaposafiri basi Yule rafiki wa bosi wake huwa anakuja nyumbani na huingia chumbani kabisa kwa bosi wake anasema huko wanaweza kujifungia hata kutwa nzima, wakihitaji chochote kama vinywaji, vyakula n.k basi bosi wake hutoka kuvichukua na kuingia navyo huko huko ndani. Kisa cha duka kufungwa ni taarifa alizopata mumewe toka kwa mtu wake wa karibu, ambaye siku moja alimuona mwanamke huyo na rafiki yake wakiingia katika chumba kimoja cha hoteli bila wao kumuona. Mume alipopata hizo taarifa kwanza alimuhoji dereva wake ambae humuendesha mkewe na huyo rafiki yake muda mwingi, nae alimueleza kweli amekuwa akiwapeleka hoteli hiyo na zingine nyingi ila wao husema wanaenda kupata lunch au dinner nay eye huwa ni mtu wa kukaa kwenye gari na kusubiri hivyo hajui kinachojiri huko ndani.




Yule mume akaamua kumtumia Yule mtu wake wa karibu kwa kuwa alikuwa ni mmoja kati ya wahusika katika ile hoteli, nae akamwambia amesikia story za chinichini kutoka kwa wafanyakazi wa hoteli ile kuwa mkewe na rafiki yake ni wapenzi. Ndipo siku moja Mume akaongopa anasafiri na baadae kurudi ghfla kesho yake mchana ndipo akamkuta mkewe na rafiki yake huyo chumbani kwake wakiwa faragha. Ndipo alipoamua kumrudisha kwao mwanamke na kulifunga lile duka alilomfungulia na ndio kisa cha jirani yangu kukosa kazi.

Kisa cha nne hiki nimekisikia huku huku maeneo ya Tabata ninapoishi, kuna mama mtu mzima, ni daktari katika zahanati Fulani ya serikali na pia ni mjariamali.Nasikia ana mahusiano na binti wa miaka ishirini na sita na mahusiano yao inasemekana yana muda kama wa miaka mitatu sasa. Huyu binti hata mimi namfahamu kiukweli sijawahi kumuona akiwa na kampani ya wanaume yani boyfriends hapana. Mwanzoni nilikuwa nasikia watu na majirani wakizungumzia hayo mahusiano yao lakini kwa sasa nasikia wako wazi zaidi, sababu wamekuwa wakionekana pamoja hata katika maeneo ya starehe kama vile Bar na mara zote meza yao huwa wapo wawili tu nasikia ikitokea mwanaume akamsalimia Yule binti huyu mama huwa anakasirika na wakati mwingine humfokea Yule binti. Siku za karibuni nimesikia huyu binti kapewa gari ya kutembelea na huyu mama na kweli nimemuona huyu binti anaendesha gari ndogo mpya aina ya premio. Ila walio karibu na huyu binti nasikia mwenyewe anasema ni kweli ile gari amepewa zawadi na huyo mama ila kwa sababu amekuwa akisimamia vizuri miradi yake na si vinginevyo. Inasemekana huyu binti hapendi watu wajue mahusiano yake na huyo mama ila kwa kuwa huyo mama anafahamika tabia zake ndo maana watu wamebaini uhusiano wao............Haya ni maelezo ya mwanadada Samira wa jijini Dar Es salaam.





WANAWAKE AMBAO WAMEWAHI KUWASHUHUDIA WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO WAKIFANYA VITENDO VYA KUJAMIIANA V YA JINSIA MOJA AMA VITENDO VINAVYO ASHIRIA KUWEPO KWA UHUSIANO WA JINSIA MOJA KATI YAO.


Tulitaka kupata takwimu za wanawake ambao wamewahi kuwashuhudia wanawake wenzao wakifanya vitendo vya kujamiaana vya jinsia moja ama vitendo vinavyo ashiria kuwepo kwa uhusiano wa kujamiiana kati ya wanawake hao. Wanawake wawili katika kila wanawake ishirini ambao walifanyiwa mahojiano walikiri kuwahi kuwashuhudia wanawake wenzao wakifanya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ama vitendo vinavyo ashiria uwepo wa mahusiano ya jinsia moja kati ya wanawake husika.


Tina * ni mwanadada wa kitanzania mwenye umri wa miaka 25 anaye ishi jijini Dar Es salaam, anasimulia jinsi alivyo wafuma rafiki zake wakifanya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja wakati wanasoma chuoni.


Nilishawahi kuwa na marafiki waliokuwa wakifanya kitendo hiki,kutokana na watu hao nimeweza kujua mengi kuhusiana na watu hawa.Mtaani nilikuwa na marafiki ambao wao walianza kufanya kitendo hiki kwa muda mrefu lakini walikuwa wakificha. Hawa ni marafiki ambao nilikuwa na cheza nao tangu utotoni. Wao mara nyingi walikuwa wakipendelea kuwa pamoja katika kila mchezo tuliokuwa tukiucheza. Kama tukicheza mchezo wa kujificha basi lazima watajificha sehemu moja na kama tukicheza mchezo wa kifamilia wao walipenda sana kuchukua nafasi ya baba na mama. Kwa wakati huo walikuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya kitendo hicho bila hata kujua kama ni tabia ya Usagaji.
Waliendelea na tabia hiyo mpaka walivyokuwa wa kubwa, ikawa ni tabia yao na walikuwa wakifanya nyumbani kwao.Mimi nilifahamu kuhusu tabia yao nilipokuwa kidato cha pili.Baada ya kuwagundua waliniahidi kuacha kwa sharti moja ambalo lilikuwa nisitoe siri yao, nami nilikubaliana nao.Baada yakuona kama nimetunza siri yao ndipo walipoweza kuniambia siri zao nyingi.


Pia katika mazingira ya chuo nimeishi na watu ambao wao pia walikuwa na tabia hiyo.Lakini wao walitoka na tabia hiyo walipo kuwa wakisoma ambapo ni katika shule ya bweni ya wanawake watupu, huko ndipo walipoanzisha tabia hiyo.
Wao walikuwa katika uhusiano mkali ambapo kila mtu alikuwa akihisi kuna kitu kati yao. Kwanza walikuwa hawapendi kabisa kuwa karibu na wavulana, pili walikuwa hawahitaji marafiki wa kike hasa wakaribu kwa sababu wote walikuwa na wivu, tatu walipenda kuwa pamoja muda wote hata wakati wa kulala na kuoga.
Wao pia walikuwa wakifanya siri juu ya jambo hili ingawa watu wengi waliwashuku. Ila mara nyingi walikuwa wakifanya tendo hilo usiku wakati watu wamelala. Siku moja nililala chumbani kwao nikaamka usiku bila wao kujua nikawasha taa nikawaona walichokuwa wakikifanya. Walishtuka baada ya kuniona mimi na kujua kama nimeona walichokuwa wakikifanya, waliacha na kulala.
Siku iliyofuata walinifuata nakuniomba pia nisitoe siri yao,Ila niliwaambia kuwa wanachokifanya sikizuri katika dini na jamii kwa ujumla.Ila waliniahidi kuacha ingawa wao walisema itakuwa ngumu kuacha kwa ghafla hivyo niwape muda wataacha.
Wao walianza kufanya kitendo hicho kwa kuwa shuleni kwao kulikuwa hakuna wavulana kwa hiyo walianza kidogo kidogo kujaribu kile walichokuwa wakikiona kwenye filamu za ngono ilikukidhi haja zao.Wanaume wa chuo walikuwa wakiwataka kimapenzi sana lakini hakuna aliyefanikiwa kwa sababu tayari wao walikuwa wanakidhiana haja zao.
Hivyo basi mara nyingi watu hawa huwa hawajihusishi na mapenzi ya jinsia nyingine ingawa wapo wachache ambao huwa na uhusiano na wanaume huku wakiwa wasagaji.




Priscila, mwanadada mwenye umri wa mika 23 ambaye ni muhitimu wa Chuo Kikuu, anasimulia kisa chake :


" Nakumbuka mwaka jana wakati bado nasoma chuo , nilikwenda maeneo ya Coco Beach kwa ajili ya kujipumzisha, nikiwa maeneo hayo , pembeni yangu kulikuwa na mabinti wawili wadogo wa kike ambao kwa kuwakadiria umri wao ni kati ya miaka 15 na 17 hivi, walikuwa wamelaliana, wanashikana huku wananyonyana ndimi zao kwa mahaba mazito sana, na kwa jinsi walivyo kuwa wamezama kwenye mapenzi wala hata hawakujali uwepo wangu katika eneo hilo " Anasema Prissila, mwanadada anaye ishi jijini Dar Es salaam.




Eliza * ( 32 ) anasema " Nilikuwa nasoma chuo kimoja hapa Dar. Kwa kuwa kwetu ni mkoani, nilipokuja Dar nilifikia kwa dada yangu ambaye alikuwa amepanga nyumba nzima maeneo ya Tabata. So nilipo kuwa nikija Dar, nilikuwa nafikia kwa dada yangu huyo, nakaa siku kadhaa then nakwenda kuishi hostel. Mara kwa mara nilikuwa naenda kumtembelea dada yangu siku za weekend hususani katika vipindi ambavyo shule ilikuwa haijachanganya sana . Wakati huo nilikuwa nina miaka 23 na dada yangu alikuwa ana miaka 30. Dada yangu alikuwa na rafiki yake wa kike amabaye alikuwa almost agemate wake. Siku moja nilienda kumtembelea nyumbani kwake. Nilipofika nilikuta geti na milango yote imeegeshwa huku muziki wa taratibu unasikika kwa mbali, nikaenda chumbani kwa dada yangu kumsalimia. Nilicho kikuta kilinishangaza sana, nilimkuta dada yangu na Yule rafiki yake msichana wapo kama walivyo zaliwa wamezama kwenye tendo la kusagana. Nilivyo wakuta dada yangu alikuwa akimnyonya Yule rafiki yake wa kike kwenye sehemu zake za siri na Yule rafiki yake alikuwa anapiga kelele za mahaba. Walipo shtukia uwepo wangu katika eneo hilo, waliacha mara moja walicho kuwa wanakifanya , mimi nikatoka nje, dada yangu akanifuata huku akinifokea sana na kuniambia kwa nini ninaingia nyumbani bila hodi, wakati wote huo mimi nilikuwa nimenyamaza kimya na Yule ‘mpenzi ' wa dada yangu alikuwa amebaki kule chumbani. Jioni ya siku hiyo walinikalisha chini na kunieleza mambo mengi sana ambayo naweza kusema kwa kiasi kikubwa sana, yalibadili msimamo na mtazamo wangu kuhusu masuala ya mahusiano ya kimapenzi.
 
[h=3]SEHEMU YA KWANZA INAENDELEA : Wanawake Walio wahi kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao.[/h] Source : ULIMWENGU USIONEKANA





314623_196742477068702_1153203693_n.jpg



1. Walio shawishiwa ana kwa ana iwe kwa kutongozwa moja kwa moja ama kwa vitendo .



Kwa mujibu wa utafiti wetu , katika kila wanawake ishirini tulio wafanyia mahojiano kuwauliza kama wamewahi kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsia moja na wanawake wenzao, wanawake wawili kati yao wamewahi kutongozwa ama kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja na wanawake waenzao .


Zuwena ni mwanamke wa kitanzania mwenye makazi yake jijini Dar Es salaam. Kwa sasa ana umri wa miaka 42 na ana watoto wane alio zaa na marehemu mume wake. Miaka kadhaa iliyopita aliwahi kukumbwa na kadhia ya kushawishiwa kuingia katika uhusiano wa jinsia moja na mwanamke mtu mzima ambaye alikuwa anajihusisha na mahusiano ya jinsia moja . Hebu fuatilia kisa chake hapa chini :


Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007, nilipata tenda ya u MC katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule Buza.


Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia. Kama kawaida niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na kufurahi. Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula. Ghafla alitokea mama mmoja mtu mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi. Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli yake. Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba yangu.
Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno " Ahsante baby ". Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu, alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu, nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia chenji ananiambia " utakunywa soda " , siku nyingine anafika ofisini kwangu ananipa hela anaondoka. Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini sikupata jibu.
Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye. Ilikuwa siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja akanipigia kuniulizia nimekwama wapi? Nikamwambia bado nina wateja , akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo yote. Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo akatoa shilinge 50,000/= . Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji naishi na nani, nikamwambia naishi na watoto wangu watatu, baba yao baba yao amefariki miaka miwili iliyopita . Nikamuuliza saluni anataka kufungulia wapi? Akanijibu achana kwanza na mambo na mambo hayo tutaongea baadaye . Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia nawawahi watoto wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue. Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akavishusha saluni kwangu, akaniambia atanipigia simu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akabishusha saluni kwangu , akaniambia atanipigia simu kesho yake kuna kitu anataka kunieleza.


Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu wa karibu , ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote mbali ya pale Buza kwa sababu nia yake hatueielewi. Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale . Alipokuja nilitoa hela ili nimuagizie kinywaji, Yule mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete kinywaji ila alimuomba Yule rafiki yangu akae meza nyingine. Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa. Yule rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na akaja kutuaga akaondoka. Nilimtumia meseji kuwa asicheze mbali.


Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu, akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka. Yaani hapo ndio alinifanya niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu wengine wakasema labda ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda tu au anataka kaka yake akuoe.
Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie nguo za biharusi mtarajiwa. Tukaondoka wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nakamwambia yapata mwezi mmoja sasa. Nikamuuliza mbona unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa nakuuliza tu. Akaniuliza unajishughulisha na nini , nikamwambia nina saluni na ni mc, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au nimeajiriwa ? Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa ananiambia mimi nichague nguo niliyo ipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa wa Agrrey kuna duka linauzwa nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje kuna kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe tama nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu , meseji ilikuwa inasema hivi " Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni msagaji mzuri pole Aunty nakuhurumia, " by Angel .


Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia mbona umesoma sms ukaonekana umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms mtoto wake anaumwa sana. Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama, nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi hospitali. Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli, nilitoka speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari, sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia vocha ya sh. 5000/= na ujumbe uliosema " I love you baby "
Nilipofika nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine waliniambia namsingizia . Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku hiyo hiyo na pale saluni nisikae. Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi ya saluni Yombo pale kwangu nikaweka msichana. Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri na simu sina. Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni kwangu kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote. Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu nikahamia Tandika nyumbani kwetu. Nilicho hofia ni kwamba kwa sababu nilishakula pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia angweza kunifanyia chochote.




Mei ni mwanadada mwenye umri wa miaka 32, ni mkaazi wa jijini Dar es salaam na anaishi na mume wake wa ndoa kwa miaka mitatu sasa. Yeye pia amewahi kushawishiwa na mwanamke mwenzake kuingia katika uhusiano wa jinsia moja. Anaelezea ;
" Nilikuwa nafanya kazi kwenye ofisi moja hapa jijini. Mkurugenzi wa jingo ambalo ofisi yetu ipo ni mwanamama mtu mzima tu ambaye kwa kumkadiria umri wake ni kama miaka 50 hadi 55 hivi. Kwa kweli ana pesa na mali nyingi tu ila tatizo ndio hilo, ni msagaji. Alikuwa na uhusiano mzuri na wa karibu na bosi wangu ofisini pale so mara kwa mara alikuwa anakuja ofisini kwetu pale na mara kadhaa tulikuwa tunapata naye lunch pamoja ( sisi kama wafanyakazi wa ofisi ile ) Sijui kitu gani kilitokea lakini nahisi yule mmama alivutiwa na mimi labda. Akaanza ukaribu na mimi, mara ikawa mazoea, akawa anainiletea letea zawadi. Mwanzoni sikuhisi kitu chochote kibaya kwa sababu alikwa anaonekana ni mwanamke anaye jiheshmu tu. Basi hali hiyo ikaendelea kwa kama miezi miwili hivi, wakati mwingine akawa ananitoa lunch na dinner. Mpaka hapo sikuwa a uhakika sana ila nilikuwa nahisi tu kwamba anaweza kuwa mtu wa dizaini hiyo but nikajipa moyo wa subira hadi niuone mwisho wake. Mwisho wa siku akaamua kunitamkia live kwamba eti ananipenda anataka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi. Niliogopa sana na kuanzia siku hiyo nikawa namkwepa , sikutaka kabisa urafiki naye wowote. Alivyoona nimekwazika na alichoniambia akaniambia eti alikuwa ananitania tu na nini, but sikumuamini tena na nilimpa karipio kali sana kwamba sitaki kabisa aniambie tena mambo yake ya kijinga jinga hayo. Baadaye akatoweka sikuwa namuona tena, ratiba za kuja ofisini kwetu zikapungua, na hata alivyo kuwa anakuja akapunguza mazoea na mimi, akahamishia ushoga kwa mwanamke mwingine aliyekuwepo pale ofisini. Sijui walifikiaga wapi coz sikukaaga muda mrefu sana pale nikahama, ila nasikia bado yupo hapa mjini na anaendeleza tabia yake hiyo kwa wanawake wenzake.


Naye Grace , msichana mwenye miaka 24 ni mkaazi wa jijini Dar Es salaam. Grace anao marafiki watano ambao wote wapo katika mahusiano ya jinsia moja na wanawake wenzao. Hii ina maana kuwa Grace anafahamiana na wanawake kumi ambao wapo katika mahusiano ya jinsi moja. Anasimulia kisa cha yeye kushawishiwa na mmoja kati ya mpenzi wa jinsia moja wa rafiki zake hao kuingia katika mahusiano ya jinsia moja ;
" Ninao rafiki zangu wasichana watano ambao wote wapo katika mahusiano ya kimapenzi na wanawake wenzao. Mimi mwenyewe nimeshatongozwa na wadada wawili ambao ni marafiki wa hao rafiki zangu walio katika mahusiano ya kimapenzi na wanawake wenzao.




Mdada mmoja kati ya hao alionitongoza anafanya kazi nzuri tu tena kwenye kampuni kubwa. Ni mwanamke tu wa kawaida lakini anajiweka kidume dume sana, anavaa hadi suti, kwa walio tembea naye wanasema huwa anavaaga hadi boxer.
Hataki kabisa kusikia kuhusu habari za wanaume, anasema alishawahi kuwa na mwanaume wakati wa utotoni mwanaume akamuumiza sana so akaamua kutokujihusisha kabisa na wanaume .
Nadhani familia yake wameshakubaliana na hali yake kwa sababu hakuna yoyote katika familia anayemuhoji kuhusu tabia yake ingawa hajionyeshi sana kwa wazazi wake ila nadhani kila mtu katika familia yake analifahamu hilo kwa sababu umri wake kwa sasa ni karibu miaka 38,hana mtoto wala rafiki wa kiume.
Nadhani sababu inayo wafanya ndugu zake hasa wazazi wake wasimsumbue kuhusu mwenendo wake ni uwezo wake wa kipesa, katika ukoo wao yeye ndio ametoka na amewatoa ndugu zake na wadogo zake wengi tu, mara nyingi ndugu zake huwa wanawapeleka watoto wao nyumbani kwa mdada huyo ambaye huwasomesha na kuwatunza hadi wanapomaliza masomo yao.


Huwa wanaogopa sana kujulikana kwa sababu wanaogopa kutengwa, kwa mfano huyu mdada aliwahi kuwa na uhusiano na binti mmoja ambaye anaishi na wazazi wake, mara kwa mara mdada huyo alikuwa anaenda hadi kwao na huyo binti kama ' family friend ' nyumbani kwao na huyo binti walikuwa wanamuheshimu sana huyo mdada bila kujua siri iliyo fichika nyuma yake, walikuwa wanamuona kama mdada fulani hivi mstaarabu mwenye mapenzi mema na binti yao kumbe alikuwa anawasaidia kumuharibu binti yao.
Niliwahi kumuuliza, kama umeamua kuishi aina hiyo ya maisha kwa nini sasa usiwe huru tu kujitangaza ili watu wote wafahamu, akaniambia " Hapana mdogo wangu unajua nikisha julikana, sitaaminika tena katika jamii, kumbuka jamii yetu ipo kinyume kabisa na haya mambo so watakapo jua kuwa ninajihusisha na mambo hayo watanitenga, wazazi hawatawaruhusu binti zao kuwa na ukaribu na mimi.
Kama isingekuwa ujasiri wangu wa kuwakemea kwa nguvu zangu zote sasa hivi na mimi ningekuwa katika mahusiano na wanawake hao, kwa sababu walinikomalia sana, yani huwa hawachoki, kila saa inaingia meseji ya kimapenzi mpaka unashangaa hivi hawa watu ni nani aliye waroga, mimi niliwakemea sana wale wadada na hadi sasa hivi wametokea kunichukia sana na nimekata kabisa mawasiliano nao. "
 
[h=3]SEHEMU YA KWANZA INAENDELEA: Wanawake walio shawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao kupitia mitandaoni.[/h]
SOURCE : ULIMWENGU USIONEKANA


womancomputer.jpg

Wanawake wanne kati ya kumi wanao tumia mitandao
mbalimbali ya kijamii kama vile Facebook, hushawishiwa
na wanawake wenzao kujiunga katika mahusiano ya jinsi
moja kila uchwao.




Linapokuja suala la wanawake kutongozwa ama kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi ya jinsi moja na wanawake wenzao, wanawake wanao tumia mitandao ya kijamii ndio wahanga wakubwa wa kadhia hii. Tulifanya mahojiano na wanawake wapato 120 ambao ni watumiaji wa mitandao ya kijamii. Swali waliloulizwa ni je, umewahi kutongozwa ama kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi ya jinsi moja na mwanamke ama wanawake wenzako kupitia hapa mtandaoni?. Katika kila wanawake ama wasichana kumi walio fanyiwa mahojiano, wanawake wanne kati yao wamekiri kuwahi kushawishiwa na wanawake wenzao kuingia katika mahusiano ya jinsi moja kupitia katika mitandao hiyo ya kijamii.
Wengi wa hao wanawake wanao shawishi wanawake wenzao kuingia katika mahusiano ya jinsi moja huwa wanatumia akaunti zenye majina feki lakini wengine hutumia akaunti zao halisi. Endapo mtongozwaji ataonyesha muelekeo wa kukubaliana nao ndipo hu reveal their real identity.
" Lakini wengine huwa ni wasichana tunao wafahamu kabisa , kwa mfano mimi kuna msichana ambaye ni rafiki wa rafiki yangu aliwahi kunitongoza kupitia mtandao wa kijamii. Nilipo wadadisi watu wanao mfahamu vema msichana huyo wakasema ni kweli huo ndio mchezo wake na amekwisha watongoza wasichana wengi tu " ….Anasema Natalia wa Dar Es salaam.
Kwa mujibu wa takwimu zetu, wanawake wanane kati ya kumi walio wahi kutongozwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao kupitia katika mitandao ya kijamii, wametongozwa na wanawake wanao tumia majina na picha za bandia. Ni wanawake wawili tu kati ya wanawake kumi walio fanyiwa mahojiano ndio wamekiri kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wanao wafahamu kabisa au ambao wanatumia majina na picha zao halisi.
 
SEHEMU YA KWANZA INAENDELEA : Taarifa za Mitandaoni Kuhusu wanawake kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao.

SOURCE : http://www.mungwakabili.blogspot.com




529188_280862385323377_519614873_n.jpg




Katika mitandao na blogu mbalimbali za kitanzania zinazo milikiwa na kuendeshwa na watanzania waliopo ndani na nje ya Tanzania, zipo taarifa za wanawake na ama wasichana mbalimbali katika jamii yetu ambao wanadai kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao. Zifuatazo ni baadhi ya taarifa za mitandao ya kitanzania, zinazo ripoti kuhusu uwepo wa wanawake wa kitanzania wanao dai ama kulalamika kushawishiwa ama kutongozwa na wanawake wenzao kuingia katika mahusiano ya jinsi moja :
1. PINDI MWANAMKE MWENZAKO ANAPOKUTAKA KIMAPENZI NA KUKUNYIMA RAHA....Inatoka hapa chini

DINA MARIOS (DM): PINDI MWANAMKE MWENZAKO ANAPOKUTAKA KIMAPENZI NA KUKUNYIMA RAHA.......... Story ninayokupa ni yaukweli kabisa ambayo amenisimulia huyu dada ambae nilitambulishwa kwake weekend hii

Huyu dada anafanya kazi kampuni fulani hapa Dar es salaam anamiaka 26,sasa hapo kazini kwao kuna dada mwingine ana miaka ya thelathini na ushee hivi anamtaka kimapenzi tena kwa udi na uvumba kiasi kwamba amekuwa kero kwake anamnyima raha ukizingatia wanafanya wote kazi na wapo ofisi moja kabisa viti vinatazamana.


Ofisini ikitokea ameongea na mwanaume anamgombeza kwa nini anaongea na wanaume wangine hajui anamuumiza roho,akizoeana na mwanaume kosa kabisa,anamletea zawadi za hapa na pale lakini yeye huzikataa akitoka lunch lazima amletee kifurushi cha chakula,anampigia simu kila saa kumchombweza kwa maneno ya mahaba,lakini dada anasema ameshamwambia hamtaki.


Dada anasema kuwa kwa jinsi anavyomtongoza mpaka akimuona anamuonea aibu utafikiri anatongozwa na mwanaume.Sasa juzi jumamosi wakati nakutanishwa nae ndio anasema ijumaa alimwambia huku ana huzuni kubwa kuwa kama kweli hamtaki awe mpenzi wake basi anaomba wakutane faragha angalau ampe kiss(denda),na akamuahidi kuwa baada ya denda hilo kama kweli hatahisi chochote tofauti kama kumpenda au msisimko wa mwili basi atamuacha aende na atakubali kumkosa japo roho itamuuma.Sasa bidada anasema amechoka kiukweli hana raha ya ofisi kuwaambia mabosi wake hataki kumkosesha kazi mwenzake kwa jambo kama hilo na pia si kila bosi anaweza litilia maanani jambo hilo ila hamuelewi akimwambia hamtaki amemganda kama ruba..


........tuliongea sana kiukweli lakini mimi na wewe hembu tuvae viatu vya huyu dada, tungefanyaje??



Mada hii ilichangiwa na watu wengi , miongoni mwa walio toa maoni yao katika mada hii ni wanawake ambao walidai nao pia kuwahi kukutana na kadhia ya kushawishiwa kuingia katika mahusiano ya jinsi moja na wanawake wenzao :


Mmoja kati ya wachangiaje hao alisema :
" Asikuambie mtu inakera mie ilishanitokea nilitetemeka mwili mzima,ila nahisi huyo dada pia anapomkatalia haonyeshi kuwa yuko makini na anamaanisha hicho anachosema,itafika mahali atmfata chooni si anajulikana mmke na mnaingia wote chooni,mh dunia imeisha "

Mchangiaji mwingine aliongeza


" Eheee! Hapo hapo dada, yalinikuta hata mimi Jirani yangu alikuwa ana miaka 25 na mimi nilikuwa na miaka 27, basi kila siku ananisimulia mambo ya kimapenzi yahusuyo mwanamke kwa mwanamke nikijaribu kuanzisha story nyingine wapi anadakia, alikuwa anasisimka vibaya mno hadi nikamgundua huyu ndugu si wa kawaida, basi siku moja akanambia ana DVD za kimapenzi za wanawake kwa wanawake niende nikaangalie, hapo ndo nikampa ukweli kuwa mie sio wa kihivyo kaa mbali na mimi na nikaondoka zangu.

Kuanzia siku hiyo balaa tupu kwani nyumba zetu zilikuwa zinatizamana, mara anizushie hili mala lile, hakunisalimia hadi akahamia mkoa mwingine. Na mimi nikapumua kwani alinikera.

Sasa huyo dada anaetongozwa kumwambia hamtaki haiatoshi kwani kwakusema hivyo inamaanisha yeye anachukuliwa na mwanamke mwingine.

Nadhani angemwambia samahani sina uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke! Ni mwanaume tu ndo anaruhusiwa kunitongoza mimi na sina vionjo vyovyote vyakuvutiwa na mwanamke kimapenzi. Mfano hata unikonyeze hata mshipa wa nanilii haunigongi, nenda katafute ulikozoea kwa watu wa aina yako.

Nahisi atamuelewa kama kweli mtongozwa yupo serious.

By mchangiaji. "



2. Urafiki Imekuwa Balaa ! MWANAMKE MWENZANGU ANANITONGOZA
Inatoka hapa : HarusiYangu.com...Tanzania's Wedding Portal


[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100%"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD="colspan: 4"] Habari zenu, jamani mimi ni mara ya kwanza kuleta tatizo hapa, ni matumaini yangu nitafaidika na ushauri wenu. Mimi ni mwanamke nina miaka 36 nimeolewa na nina watoto wawili, nafanya kazi kwenye kampuni moja hapa bongo, hivi karibuni hapa kazini kuna mama nae kaolewa ana miaka 40 amekuwa akinitaka kimapenzi.Siwezi kusema ni bosi wangu maana tuko ofisi moja ila ana madaraka zaidi yangu, huyo dada tumezoeana kikazi lakini, hivi karibuni amekuwa karibu sana na mimi, mara huniletea lunch ofisini, mara anisubiri tuondoke wote, mara aje tu ofisini kuniongelesha. Mwanzoni nilifikiri anataka tu kunizoea kama rafiki lakini hivi karibuni naona kazidisha. Juzi kaja nilipokuwa nimekaa akaniwekea mkono begani halafu akaniangalia usoni kwa sekunde kadhaa karibu nijikojolee kwa uoga, hajanitamkia ila nahisi ananitaka kimapenzi maana ni wazi kabisa. Jana jioni kanisubiri mpaka nimemaliza kazi kanipa lifti mpaka nyumbani kwangu. Jana kaniachia kimeseji ofisini eti tukutane lunch kufika kaniodea na chakula nikabaki nimeduwaa, nikamuambia sitaweza kukaa kula maana nina kazi kibao ofisini nitabeba basi na yeye kabeba chake kaja kula ofisini kwangu alivyomaliza akakaa nikawa najaribu kupoteza lengo namuuliza mambo ya kazi lakini mara anishike mkono, mara aniangalie tu kwa muda usoni ili mradi tu ni kama mwanaume anavyomtongoza mwanamke vile, sasa najiuliza nimuelezeje huyu dada kuwa mimi sio msagaji? na sipendi anavyofanya, hajanitamkia wazi ila wiki iliyopita kaniletea zawadi alivyotoka kwenye mkutano Arusha, sasa nimechanganyikiwa nihame ofisi au nimwambie bosi maana na yeye ana ubosi fulani pia, au nifanyeje? maana nae kaolewa sasa sijui kwanini ananitongoza wakati ana mume, kilichonifanya nishtuke ni kadi aliyoninunulia siku chache zilizopita yaani ilikuwa ni ya kimapenzi kabisa, nikamuuliza ni ya nini akasema eti kwasababu hakunipa kadi ya iddi, nikabanwa na uharo kabisa, wenzangu ofisini wanadhania nimechanganyikiwa tu hawaamini, ila jamani natongozwa mie na mwanamke mwenzangu nifanyeje? [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[TD]

[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD="width: 4"][/TD]
[TD="width: 292"][/TD]
[TD="width: 221"][/TD]
[TD="width: 116"][/TD]
[TD="width: 116"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]




· 3. Kweli Ushoga kazi!!!!

Habari dada,naomba unisaidie hili swala,nina rafiki yangu wa kike,urafiki wetu wa miaka kama 8 sasa,ila tangu mwaka jana dec,simuelewi shoga yangu kabisa ananiletea tabia za usagaji,tunaweza kwenda diiner wote ,akishalewa tu yaani anataka kunubusu,kunishikashika maziwa,sasa nikamuuliza kwanini unapenda kufanya hv ,akanijibu anapata hisia nami,mie nikamjibu siwezi kufanya kitendo hicho naye,kwanzia hapo shoga ananichunia,nikimtafuta ananiwekea pozi.jamani mnajua maana ya urafiki nimeshamzoea shoga yangu ila vitendo vyake vyanishinda,je nitamsaidiaje aache hivyo vitendo?

CHANZO : Kweli Ushoga kazi!!!! - Ladies Chat
 
SEHEMU YA KWANZA BADO INAENDELEA : TAARIFA ZA KWENYE MAGAZETI KUHUSU UWEPO WA WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA JAMII YETU.

SOURCE: ULIMWENGU USIONEKANA






Kwa muda mrefu sasa, vyombo vya habari nchini Tanzania hususani magazeti , haswa haswa yale yajulikanayo zaidi kama magazeti pendwa ama magazeti ya udaku vimekuwa vikiripoti mara kwa mara kuhusu uwepo wa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini.
Kwa mujibu wa utafiti wetu , kati ya mwezi January mwaka 2000 hadi mwezi Januari mwaka 2013, zimeripotiwa habari zaidi ya 140 kuhusu wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini .
Hii ni sawa na wa habari 14 kila mwaka ambayo ni sawa na wastani wa habari moja kila mwezi.
Hii ni sawa sawa na kusema kwamba, katika kila mwezi, angalau habari moja inayo husu wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao, huripotiwa kwenye mojawapo kati ya magazeti ya Tanzania, hali inaonyesha ni kiwango gani, suala la usagaji limeshamiri katika jamii yetu.

Zifuatazo ni baadhi ya habari za magazeti ya Tanzania ambazo zinaripoti kuhusu uwepo wa wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao katika jamii yetu:

UCHAFU ! Warembo Wawili Wafumwa Chooni Wakifanya Vitendo Vya Kisagaji! Wananchi Wahoji Nchi Inakwenda Wapi ? ….Gazeti la Ijumaa Wikenda, Toleo Na. 13 , Monday, August 6, 2007
Na Mwandishi Maalumu.
Pamoja na Serikali kuongeza mkazo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, inaonekana baadhi ya Watanzania bado hawajali, kwani hivi karibuni kamera yetu iliwabamba warembo wawili wakifanya vitendo vya usagaji chooni.

Warembo hao waliofahamika kwa majina moja moja, Khanifa na Mwaija (pichani kushoto), walibambwa Agosti 2, mwaka huu ndani ya choo kilichopo kwenye Ukumbi wa Baa ya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakifanya uchafu.

Kamera yetu iliyokuwepo ukumbini humo kushuhudia burudani kutoka kwa Kundi la Jahazi Modern Taarab, ilitonywa na chanzo chetu kimoja kuhusu uwepo wa ‘kamchazo kachafu ka' warembo hao chooni.

Chanzo hicho, jinsia ya kike ambacho kilionesha kukerwa na uchafu wa warembo hao, kilitupasha kuwa, Khanifa na Mwaija walikuwa kero kwa watu wengine kwa sababu waligeuza choo kuwa chumba cha kufanyia mapenzi.

Kiliendelea kutanabahisha kwamba, warembo hao walikuwa wameingia chooni muda mrefu, lakini cha ajabu badala ya kutimiza kilichowapeleka, waliamua kufanya vitendo vya kusagana.
“Wanatia kinyaa, tunaomba mtusaidie, yaani wamevuana nguo, mmoja matiti yako nje, sisi wengine tukienda chooni ni kero tupu,” kilisema chanzo hicho.

Baadaye, katika kupata ukweli wa mambo, ‘paparazi’ wetu wa kike aliingia kwenye choo hicho ambapo aliwakuta warembo hao na kufanikiwa kuwapiga picha wakiwa katika pozi la kimahaba huku wakitomasana.

Hata hivyo, kutokana na kile kilichotafsiriwa kama ni kutokujali, warembo hao waliendelea na mchezo wao bila wasiwasi licha ya kushuhudia wakipigwa picha huku baadhi wateja wakiwataka waondoke chooni.

Aidha, baada ya paparazi wetu kufanikiwa kuwapiga picha wasagaji hao, chanzo chetu kingine kilichodai kinawafahamu warembo hao, kiliwataja majina yao kuwa ni Mwaija na Khanifa ingawa hakikuwatofautisha.

Kilisema, warembo hao wameshakubuhu kwa vitendo vya usagaji na mara wanapozidiwa na kilevi, hushindwa kujizuia na kufanya mapenzi sehemu yoyote.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kwa sasa wasagaji hao wanaishi kama mke na mume nyumbani kwao, ingawa hakikusema ni sehemu gani ya Jiji la Dar es Salaam.

Gazeti linalaani vikali vitendo vya aina hiyo, kwani siyo tu kwamba vinakwenda kinyume na maadili ya Mtanzania bali pia vinachochea kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Tunaiomba serikali idhamirie kukomesha hali hiyo. MHARIRI.







· AIBU ! Mke wa mtu afumwa akisagwa laivu! Mumewe ajiua!
Gazeti la Leo Tena c, Toleo No. 090 DESEMBA 24-30, 2009.

Katika kile kinacho onekana kama dunia kwa sasa imefika mwisho, wanawake wawili walibambwa laivu wakisagana, bila hata kuona haya na mwisho mume wa mmoja kati ya wanawake hao kuamua kujiua.
Sakata hilo ambalo lilishuhudiwa ‘ laivu ‘ bila chenga na mdaku wetu linadaiwa kuwa lilikuwa kama vile ilipangwa fumanizi kutokana na wanawake hao kuwa na ukaribu wa kutia shaka.
Wanawake hao wanaoishi eneo la Makao Mapya , Arusha walikuwa wakifuatiliwa kwa ukaribu na wadaku ambao walishahisi uhusiamo wa kusagana kati yao.
“ Unajua dada mmoja aitwaye Mama Ashura, ndiye aliye mshawishi mwenzake kuingia katika mchezo huo mchafu kwani yeye alisha achika siku nyingi na kurejea hapa akitokea Nairobi.
Alipo fika hapa Arusha na yeye alipanga katika nyumba hiyo na akiwa hapo ndipo alipo anzisha nahusiano na dada mwingine aitwayea Mariam.

Kila siku alikuwa akionekana akiwa naye huku akimtoa ‘ out ‘ kutokana na tukashangaa kuona Mariam akikataa wanaume huku Mama Ashura wakati mwingine akimfokea akiona amesimama na mwanaume yoyote Yule.

“ Mume wa Mariam alikuwa amesafiri , aliporudi naye akashangaa kuona mabadiliko makubwa kwa mkewe na ndipo akaanza kumfuatilia kwa karibu zaidi baada ya wapambe kumtonya’ kilisema chanzo chetu.
Mpashaji wetu alidai kuwa wiki mbili zilizo pita , mume wa Mariam alimuaga mumewe kwamba anasafiri kwenda Uganda kikazi, lakini kumbe alikuwa ‘ yupo yupo ‘ Arusha.
Chanzo chetu kinatupasha kuwa ,wakati alipoaga anaondoka aliacha mpambe ambaye alimpa jukumu kla kumfuatilia Mariam kwa karibu zaidi ili kujua mwisho wa yote utakuwaje kati yao watu hao siku hiyo.
Inadaiwa ilipofika saa 8 mchana, Mariam alijitoma katika chumba cha Mama Anna, huku mpambe akishirikiana na mpangaji mwingine katika kupata picha halisi za tukio ili aonyeshwe mume wa Mariam.
Mume wa mwanamke huyo alipigiwa simu na kuitwa baada ya wanawake wale kupigwa picha kwa siri bila kujijua kwani walikuwa wamezama katika ‘ malavidavi ‘ makubwa kiasi cha kushindwa kutambua kama kuna watu wameingia chumbani kwao na wanawapiga picha.
Inadaiwa kuwa mume wa Maria alipo fika na kushuhudia kile mkewe alichotenda , hakuaga mtu na alikuja kupatikana baada ya siku tatu akiwa amekufa.
“ Hatujui kama alijiua au la lakini kwa vyovyote vile Mariam ndiye aliye changia yote, kwani huenda mumewe alipatwa na mshituko mkubwa baada ya kumshuhudia mkewe akiwa anafanyiwa ubaradhuli na mwanamke mwenzake ‘. Mnyetishaji wetu alihabarisha zaidi ya kwamba, kwa sasa Monica na Mama Anna wamekimbia pamoja na inadaiwa wapo Nairobi ambapko wanaishi kama mke na mume .
 
SEHEMU YA KWANZA INAENDELEA: TAARIFA ZA KWENYE TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU UWEPO WA WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA JAMII YETU .


SOURCE : ULIMWENGU USIONEKANA





Katika tovuti na blogu mbalimbali zinazo milikiwa na watanzania waishio ndani na nje ya nchi, suala la wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao, limekuwa likijadiliwa mara kwa mara na mara zote linapojadiliwa hupata maoni mengi kutoka kwa mafuatiliaji wa mitandao hiyo . Zifuatazo ni baadhi ya mada zinazo zungumzia suala la mahusiano ya jinsia moja ya wanawake kwa wanawake katika tovuti na ama blogu mbalimbali zinazo milikiwa na watanzania


1. INASEMEKANA IDADI YA WANAWAKE KUJIHUSISHA KIMAPENZI NA WANAWAKE WENZAO INAONGEZEKA KILA SIKU...KISA???




Inasemekana idadi ya wanawake kujihusisha kimapenzi mwanamke kwa mwanamke inaongezeka,na wengi hulalamika wamechoka presha za wananaume...mioyo yao imeumizwa wamechoka...sasa sijui kiukweli naomba mniambie hapa nielewe ni kweli wanaume ni sababu katika hili?au kuna lingine?kwa nini tabia hii inakua?na wanawake mnasemaje?
CHANZO : ...... http://dinamarios.blogspot.com/2009/07/inasemekana-idadi-ya-wanawake.html












[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 81%"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
2. TABIA CHAFU ILIYOANZISHWA NA WASICHANA WA DAR ES SALAAM


CHANZO : Sintah.Com: TABIA CHAFU ILIYOANZISHWA NA WASICHANA WA DAR ES SALAAM
Hi wadauzz

Mamboz
kuna tabia chafu ambayo wasichana wengi wa Dar es salaam hata wasanii wa kike wamekuwa nayo,hii tabia ni ya kujiusisha na ngono ya jinsia moja(usagaji)
sielewi hili balaa limeanzia wapi eti ni fashion,yaani wasichana wengi wa Dar wakiwemo wasichana maaruf they do practise,kwangu mimi sijaifurahia kwani kama wasichana maarufu ambao ni kioo cha jamii wanatia aibu hakuna fashion ya usagaji jamani fanyeni vyote ila sio hii
hii ninawapa the ist awaken call,wakiendelea nitawataja humu humu maana watu kama sisi tumeletwa kwa ajiil ya kusaidia jamii ukizingatia kizazi kipya kinakuwa
ukinichukia alrit,ukinipenda alrit mimi ndio mim,

Kumbuka hii ni kuwaambia wajirekebishe, tuu ila ikiindelea tutawaanika humu.






3. Shangazi Yangu Ananisaga Kila Mara, Nifanyeje??


Mimi naitwa NASRA na nina mika 24, hilo nalileta kwenu jambo lango wana-Udakuz naomba mnisaidie ushauri ili niwe kutatua tazizo hili linalonikabili hapa chini:

Baada ya mama yangu kufariki 2001 kuna shangazi yangu (ambaye ni mke wa mjomba wangu) alinichukua kwa minajil ya kunilea na kunisomesha ila amekuwa AKINISAGA tokea niko mdogo mpaka sasa! ambapo nikiwa mdogo wakati nimelala nilikuwa nashtuka yupo juu yangu na mimi nipo UCHI huku ananinyonya MATITI na sehemu nyingine za mwili na baadae alikuwa anapanda juu yangu na kunilalia huku akifanya vitu fulani mpaka ananimwagia vitu fulani katika sehemu zangu za siri na kuniambia ninyamaze nisimwambie mjomba "eti atanipa pesa ya kutumia shule na kunipeleka na gari, alipokuwa akimaliza baadae alikuwa akiniogesha na kuninunulia vitu VITAMUTAMU. Nilinyamaza maana sikujua jambo lile ila aliendelea kila mara mchezo wake huo.

Mpaka sasa Nimekuwa Lakini anaendelea mchezo huo na mimi nimeshajua na sometimes nasikia raha ila roho yangu haitaki kabisa mchezo huo , huwa naumia sana ...nataka niwe msichana wa kawaida ni date na wavulana na nisikie raha napokuwa na mvulana.....naombeni ushauri...

Chanzo :Shangazi Yangu Ananisaga Kila Mara, Nifanyeje??
Re: MCHUMBA WANGU HAJISIKII RAHA KUFANYA MAPENZI NA MWANAUME ILA KUSAGANA NA MSICHANA MWENZAKE.

CHANZO : https://www.jamiiforums.com/mahusia...anaume-ila-kusagana-na-msichana-mwenzake.html

Habari za majukumu wanajamii frm wote. Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa. Nimekuja hapa kwenye jamvi hili kutafuta ushauri ili nimsaidie mchumba wangu

Mimi ni kijana wa umri wa mika 27, nina mchumba wangu ambaye nampenda na tunatarajia kuoana kabisa kama Mungu akipenda.


Lakini tatizo la huyu mpenzi wangu hafurahii wala hana hamu kabisa ya kusex na mwanaume ila anasema anafurahi kusagana na msichana mwenzake mchezo ambao waliuanza tangu walipokuwa shule na mpaka leo hii wanaendelea nao japokuwa huyu mpenzi wangu ananiambia wazi kuwa haupendi mchezo huo, amechoka na yeye papoja na huyo msichana mwenzake wanatamani kuacha ila wanashindwa na sasa wanafanya sio kwa kupenda ila mazowea tu kwani wamekuwa kama waathirika wa mchezo huo.


Na kwa maelezo yake hali hiyo ya kutojisikia kusex na wanaume, sio kwamba ilianza baada ya kuanza kusagana na huyo msichana. Anadai ilianza tangu alipokuwa na mpenzi wake wa kwanza ambaye ni mvulana kabla hajaanza kusagana, kwa hiyo alianza kusagana wakati akiwa na mpenzi wa kiume.


Kwa kweli hivi sasa wanauchukia na wanatafuta njia ya kuachana na mchezo huo na kurudi kwenye hali ya usichana yaani kutamani kusex na mwanaume. Hii ndio maana nimekuja hapa jf kwa great thinkers kuomba ushauri wafanyeje kuacha kusagana na kurudisha hamu ya kusex na mwanaume. Natanguliza shukrani kwa watakaochangia ushauri na mawazo yao kunisaidia katika hili.





KATIKA MITANDAO YA KIJAMII:

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, kuna idadi kubwa sana ya watumiaji wa mitandao hiyo ambao wanajitambulisha kama wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao ama wanawake wanao tafuta wanawake wenzao kwa ajili ya kuanzisha nao uhusiano wa jinsi moja. Kwa mujibu wa utafiti wetu, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2013, kuna makundi zaidi ya thelathini kwenye mtandao wa kijamii wa facebook yanayo wahusisha wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 45 ambao wanajitambulisha kama wanawake wa kitanzania wanao jamiiana na wanawake wenzao ama wanao tafuta wanawake wenzao kwa ajili ya kuanzisha nao uhusiano wa jinsia moja. Wastani wa idadi ya wanachama katika kila kundi ni wanachama 40. Wengi wa wanachama katika makundi haya pia ni wanachama katika makundi mengine ya wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao waliopo katika nchi za Kenya, South Afrika, Ghana,
Nigeria nakadhalika.


SEHEMU YA PILI BADO INAENDELEA; COMING UP NEXT..



553505_280861908656758_999164511_n.jpg

529188_280862375323378_2050598982_n.jpg



1..WANAWAKE WANAO TAFUTA WANAWAKE WENZAO KATIKA MITANDAO YA URAFIKI NA UCHUMBA KWA AJILI YA KUANZISHA MAHUSIANO YA JINSI MOJA.



2. WA NAWAKE WANAO FANYA BIASHARA YA KUUZA MIILI YAO KWA WANAWAKE WENZAO NCHINI TANZANIA ( LESBIAN PROSTITUTION IN TANZANIA ).



528817_281548501921432_99669590_n.jpg




3. WASICHANA WANAO JAMIIANA NA WASICHANA WENZAO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA WASICHANA PEKEE.





4. WASICHANA WANAO JAMIIANA NA WASICHANA WENZAO KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU NCHINI TANZANIA.

5. WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO KWENYE TASNIA YA MUZIKI WA TANZANIA.



6. WANAWAKE WANAO JAMIIANA NA WANAWAKE WENZAO KWENYE TASNIA YA FILAMU ZA KITANZANIA.


389088_341191032623845_1796495051_n.jpg


7. USAGAJI KWENYE FASIHI YA KISWAHILI YA TANZANIA : Fasihi Ya Kiswahili Kutoka Tanzania Inavyo lielezea suala la usagaji.


396858_341191205957161_837050424_n.jpg


Baada ya kumaliza vipengele hivi, tutaenda kuitazama kwa kina sehemu ya pili ya makala haya ambayo inahusu sababu zinazo wafanya wanawake wa Tanzania kujamiiana na Wanawake Wenzao. Zaidi ya wasagaji wa kitanzania wapatao arobaini na saba wamefanyiwa mahojiano. Endelea kufuatilia uzi huu, au blogu ya http;//www.mungwakabili.blogspot.com ama gazeti la " ULIMWENGU" litakalo anza kuwa mitaani katikati ya mwezi Agosti 2013...
557463_361263900616558_1491031251_n.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom